Nini maana ya Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza (Yakobo 4:9)

Nini maana ya Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza (Yakobo 4:9)

Swali: Biblia inasema katika Yakobo 4:9 kwamba kucheka kwetu kugeuzwe kuwa maombolezo, je Mungu hapendi tuwe tunafurahi? Au maana yake ni nini mstari huu?

Jibu: Turejee

Yakobo 4:9  “Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu”.

 Kicheko kinachozungumziwa hapo ambacho kinapaswa kigeuzwe kuwa maombolezo sio kicheko cha mambo mazuri, kwamba umeona watu wameokoka na ukafurahi na kushangilia na kucheka, kwamba ndio kicheko hicho kibadilike kiwe maombolezo!.

Hapana! Bali kicheko kinachozungumziwa hapo ambacho ni sharti kibadilike na kuwa maombolezo ni kicheko cha mambo mabaya (yaani dhambi). Mtu anapocheka baada ya kupata fedha za dhuluma, kicheko hicho ndicho biblia inachosema kuwa kinapaswa kibadilike kuwa huzuni, Kicheko mtu anachokipata baada ya kumwumiza mwingine au kuiba, au kula rushwa au kudhulumu au kufanya jambo lingine lolote baya hicho kicheko kinapaswa kibadilike na kuwa huzuni.

Maana yake mtu anapogundua makosa yake hapaswi tena kufurahia mabaya anayoyafanya au aliyokuwa anayafanya, badala yake anapaswa aomboleze, mtu aliyekuwa anazifurahia pesa haramu na kuzichekelea pale anapomjua Yesu, anapaswa asiendelee kufurahia maisha anayoishi bali aomboleze kwa kutubu na kujutia alichokuwa anakifanya.

Na kwanini ni muhimu kuomboleza na kutubu kwa mabaya, badala ya kucheka na kufurahia katika mabaya?

Ni kwasababu Bwana Yesu alisema ole wao wachekao sasa maana wataomboleza na kulia..

Luka 6:25 “… Ole wenu ninyi mnaocheka sasa, kwa kuwa mtaomboleza na kulia”.

Kwahiyo ni heri leo kuomboleza  kwaajili ya dhambi na maovu ili tupate rehema na siku za mwisho tuweze kuokolewa na lile ziwa na moto, kuliko leo kucheka na kufurahia mambo mabaya halafu mwisho wa siku tunatupwa katika ziwa liwakalo moto.

Swali ni je! Mimi na wewe leo tunafurahia nini na kuombolezea nini?

Je ni anasa ndizo unazozifurahia?, ni uzinzi na uasherati ndio unaoufurahia?, je ni mali za dhuluma ndizo zinazokupa kicheko?, je ni wizi ndio unaokuburudisha? Je ni kuanguka kwa wengine ndiko kunakokuchekesha.

Kumbuka neno la Mungu litabaki kuwa lile lile siku zote kuwa “ole wao wanaocheka sasa maana watalia”

Tubu ukaoshwe dhambi zako leo kwa kumwamini Yesu Kristo na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana Yesu Kristo.(Matendo 2:38).

Yakobo 4:7  “Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.

8  Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.

9  Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu.

10  Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza”.

Maran atha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

KUWA MWOMBOLEZAJI.

Nini maana ya neno ‘mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena’?

MAZUNGUMZO MABAYA HUHARIBU TABIA NJEMA.

Nini maana ya huu mstari; Mithali 10:22 “Baraka ya Bwana hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo”

Nini maana ya huu mstari Ayubu 23:10 ‘Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu’?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
1 year ago

Very good message you always bless me