Nini maana ya neno ‘mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena’?

Nini maana ya neno ‘mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena’?

SWALI: Biblia inamaana gani inaposema ‘mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena’ (Mithali 24:16)


JIBU: Ili kuielewa vema mstari huo  tuanzie vifungu vya juu yake kidogo.

Mithali 24:15 Ewe mtu mbaya, usiyavizie makao yake mwenye haki; Wala usipaharibu mahali pake pa kupumzika; 

16 Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; Bali wasio haki hukwazwa na mabaya.

Hapo anazungumzia tabia za mtu mbaya anayejaribu kuharibu kazi za mtu mwema (mtakatifu). Kwamba anaweza kudhani kuwa kufanikiwa kwa mipango yake, kutamfanya Yule mtu akate tamaa ya kuendelea mbele, lakini kinyume chake, ni kuwa bado atanyanyuka tena na kuendelea mbele.

Kwamfano, watu Fulani wanaweza kuharibu umoja wa kanisa, kwa kupachika fitna na masengenyo ndani yake, na matokeo yake ikawa ni kanisa  kuvunjika au kugawanyika, lakini kiuhalisia watoto wa Mungu wa kweli, wenye mbegu ya Mungu ndani yao, watasimama tena na kuujenga ule umoja walioupoteza. Lakini wengine wasio wa Mungu, watakimbia, au watakata tamaa na kurudi nyuma, na kufurahia kuanguka kule.

Au jengo la kanisa linaweza likaharibiwa na wapagani au mazingira ya asili, lakini watu wenye mbegu ya Mungu hawakati tamaa watanyanyuka na kulijenga tena upya.

Ndivyo ilivyokuwa kipindi cha wafalme wakati ambapo hekalu la kwanza linabomolewa na Nebukadreza mfalme wa Babeli, Baadhi ya wayahudi hawakumwacha Mungu wao moja kwa moja, bali waliendelea kumtafuta na kumwomba sana (Akiwemo Danieli) hatimaye baada ya miaka 70 wakarudi kulijenga upya tena. Hata baadhi ya wafalme walipotoa tamko la kusitishwa kujengwa kwa hekalu hilo bado walisimamia kusudi lao lilelile mpaka kulimaliza ijapokuwa waliwekewa vikwazo vingi sana.

Halikadhalika Injili ya mitume ilizuiliwa mara nyingi, Kwamfano Paulo anasema shetani alimzuia mara tatu ili asiipeleke injili (1Wathesalonike 2:18). Wakati mwingine alifungwa Lakini hayo hayakumkwaza na kumfanya aache kuihubiri injili, kisa amezuiliwa, bali kila siku maisha yake yalikuwa ni ya utumishi kana kwamba hakuna kikwazo chochote mbele yake, hata alipokuwa gerezani alihubiri kwa nyaraka, ambazo baadhi ya hizo ndio hizi zinazofanyika Baraka kwetu hadi sasa.

Kama mitume wangehesabu vikwazo, vitisho, vifungo, kamwe wasingeweza kuieneza injili ile ulimwenguni kote kwa kasi ile. Hivyo na sisi, tufilisikapo, tupatapo hasara, tufiwapo, tusalitiwapo na baadhi ya ndugu, ikapelekea mpaka huduma kuvurugika, au maisha ya kiroho kudorora, tusife moyo wa kumtumikia Bwana au kuendelea mbele, bali tunaanza tena upya, kana kwamba ndio tumezaliwa tena mara ya pili leo.

Lakini mstari huo haumaanishi, kuanguka katika “dhambi”, kama wengi wanavyodhani. Mtakatifu hana tabia ya kuanguka anguka ovyo kwenye dhambi..Yaana leo adondoke kwenye uzinzi, halafu kesho tena aanguke kwenye uzinzi, kesho kutwa hivyo hivyo, halafu awe bado na nguvu ya kusimama kwa Bwana. Hilo jambo haliwezi kutokea kwa mtu aliyezaliwa mara ya pili.

Kuanguka kwetu ni kuwekewa vikwazo na adui, vilivyo nje ya uwezo wetu, lakini sio vile vilivyo ndani ya uwezo wetu.

Bwana akubariki.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?

Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako (Mithali 27:23)

Nini maana ya Mithali 27:6 “Jeraha utiwazo na rafiki ni amini;

Nini maana ya mhubiri 9:11? si wenye mbio washindao katika michezo?

Nini maana ya Usiwe mwovu kupita kiasi? (Mhubiri 7:17)

Kwanini samaki wasio na mapezi na magamba hawakuruhusiwa kuliwa?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments