Mierebi ni Nini kwenye biblia? (Isaya 15:7)

Mierebi ni Nini kwenye biblia? (Isaya 15:7)

Mierebi ni aina ya miti inayostawi Mahali palipo na maji maji, Mahali pengine popote haistawi. Tazama mwonekano wake kwenye picha juu.

Hivi ni baadhi ya vifungu vinavyolitaja Neno hili;

Mambo ya Walawi 23:40

[40]Nanyi siku ya kwanza mtajipatia matunda ya miti mizuri, na makuti ya mitende, na matawi ya miti minene, na mierebi ya vijitoni; nanyi mtafurahi mbele za BWANA, Mungu wenu, muda wa siku saba.

Isaya 44:2-5

[2]BWANA, aliyekufanya, na kukuumba toka tumboni, yeye atakayekusaidia, asema hivi; Usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu; na wewe, Yeshuruni, niliyekuchagua.

[3]Kwa maana nitamimina maji juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu ya mahali pakavu; nitamwaga roho yangu juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao utakaowazaa;

[4]nao watatokea katika manyasi, kama mierebi karibu na mifereji ya maji.

[5]Mmoja atasema, Mimi ni wa BWANA; na mwingine atajiita kwa jina la Yakobo; na mwingine ataandika juu ya mkono wake, Kwa BWANA, na kujiita kwa jina la Israeli.

Soma pia Ayubu 40:22, na Isaya 15:7

Kama tunavyosoma hapo Bwana aliwaagiza Wana wa Israeli watumie matawi yake kama kitu Cha shangwe katika sikukuu ya vibanda..Pindi wanapokusanyika wayanyanyue juu wamwimbie Bwana nyimbo za furaha. Lakini bado tunaona sifa ya mti huu ni kuwa karibu na vijito vya maji.

Vivyo hivyo na watu wa Mungu Rohoni, Bwana anawaona kama mierebi yake, miti inayostahili kumsifu Bwana..Kwasababu ndani yao mito ya maji ya uzima inatiririka.. lakini wengine ambao hawana Kristo ni sawa na miti mikavu tu.

Na matokeo ya kukosa mito ya uzima ndani yako ni wewe kufanyika makao ya mapepo kwasababu mapepo ndio Yanakaa sehemu isiyo na maji.

Soma

Mathayo 12:43-45

[43]Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate. [44]Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa. [45]Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.

Umeona? Unasubiri nini usimpe Bwana Yesu maisha Yako? Huna Raha, Wala Tumaini, Wala faraja unapokuwa nje ya Kristo. Okoka Leo Bwana ayaponye maisha Yako.

Ikiwa upo tayari kuchukua uamuzi huo wa kuokoka na kufanyika Mwerebi mzuri wa Bwana basi fungua hapa Kwa ajili ya mwongozo huo>>

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Mretemu ni mti gani?

Mti wa Mshita ni mti wa namna gani?

Mti wa MLOZI alioonyeshwa nabii Yeremia 1:12 tafsiri yake ni nini?

Mjusi hushika kwa mikono yake; Lakini yumo majumbani mwa wafalme.

Mimbari ni nini? Je tofauti kati ya Mimbari na madhabahu ni ipi?

NUNUA MAJI YA UZIMA.

Mofa ni nini? na inafunua nini kiroho?(1Samweli 28:24).

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments