Mti wa Mshita ni mti wa namna gani?

Mti wa Mshita ni mti wa namna gani?

Wingu la Mashahidi
Wingu la Mashahidi
Mti wa Mshita ni mti wa namna gani?
/

Swali: Mti wa Mshita uliotengenezea sanduku la Agano ndio upi kwasasa?(Kutoka 25:10)

Jibu: Tusome

Kutoka 25:10 “Nao na wafanye sanduku la MTI WA MSHITA; urefu wake na uwe dhiraa mbili na nusu, na upana wake dhiraa moja na nusu, na kwenda juu kwake dhiraa moja na nusu.

11 Nawe ulifunike kwa dhahabu safi, ulifunike ndani na nje, nawe tia na ukingo wa dhahabu kulizunguka pande zote”.

Mshita ni jamii ya miti ambayo hata sasa ipo, na inapatikana katika sehemu nyingi za dunia, ikiwemo katika bara letu la Afrika, na hata katika Afrika mashariki.  (Tazama picha juu). Mti wa Mshita ni mti unaostahimili ukame zaidi ya miti mingi.

Tabia za mti wa mshita, ni kwamba ni moja ya miti migumu, na vile vile ni mti ambao hauharibiwi  na wadudu wala maji, wala hauingiaa fangasi kirahisi, jambo linaloifanya mbao ya mti huo iweze kutumika kutengenezea baadhi ya vyombo vya kuhifadhia vyakula, na sifa nyingine ya mbao ya mti wa Mshita ni rahisi kupakika rangi, kwasababu uso wake ni mwororo.

Sasa Kwanini Sanduku la Agano lilitengenezwa kwa mti wa Mshita?

Jibu, ni kwasababu ya tabia au sifa za mti huo.

Ndani ya Sanduku la Agano kulihifadhiwa chakula (yaani ile pishi ya mana) kwaajili ya ukumbusho wa vizazi vijavyo vya wana wa Israeli..Hivyo ni lazima chakula hicho kihifadhiwe ndani ya sanduku lililo imara lisiloingia fangasi wala wadudu waharibifu. Mbao nyingine zaidi ya Mshita, hazina sifa hizo!

Vile vile ndani ya Sanduku kulikuwa na zile mbao mbili, ambazo Musa aliambiwa azitengeneze, zilizoandikwa Amri kumi na chanda cha Mungu mwenywe, Mbao hizo ziliwekwa ndani ya Sanduku kuwa ukumbusho wa daima, hivyo ni lazima zihifadhiwe katika Sanduku lililo gumu ambalo haliharibiki haraka..

Na vile vile kulikuwa na ile fimbo ya Haruni iliyochipuka, ambayo ilihifadhiwa nayo pia kama ukumbusho wa utumishi wa kikuhani wa nyumba ya Lawi.. Fimbo hiyo nayo ilipaswa ihifadhiwe ndani ya sanduku imara lisiloruhusu unyevunyevu au maji kuingia.

Na sanduku la Agano linafananishwa na mioyo yetu..  Katika kitabu cha Yeremia 31:31, Biblia ilitabiri kuwa katika Agano jipya tulilopo sisi, sheria za Mungu zimeandikwa mioyoni mwetu.. Mioyo yetu kwa Bwana ni kama mti wa Mshita, Hivyo hatuna budi kuzidi kuiimarisha mioyo yetu, kwa kukaa mbali na dhambi ili tuzidi kuzidumisha sheria za Mungu katika mioyo yetu.

Maran atha!

Mada Nyinginezo:

Mwaloni ni nini? Na je unafunua nini rohoni?

Mwerezi ni nini?

FANYA BIDII ZOTE ULE MATUNDA YA UZIMA.

Kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?

Je Adamu na Hawa, walikuwa hawafanyi mema kabla ya kula tunda?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Roselyn
Roselyn
4 months ago

Barikiwa sana mtu wa Mungu…nimejifunza kwa njia rahisi sana asante