Mretemu ni mti gani?

Mretemu ni mti gani?

Swali: Ule mretemu ambao Nabii Eliya alijilaza chini yake ulikuwa ni aina gani ya mti, na je una muujiza wowote kiroho? (1Wafalme 19:4).

Jibu: Mretemu ni aina ya mti ujulikanao sasa kama “MTARAKWA”. Zipo jamii nyingi za mitarakwa kulingana na mahali na mahali. Mtarakwa unaomea katika bara la Afrika ni tofauti kimwonekano na ule unaomea katika bara la Ulaya, (kutokana na hali ya hewa). Lakini yote inamatawi yanayofanana na tabia zinazofanana, kinachoitofautisha ni unene na urefu.

Mti wa Mtarakwa (au Mretemu) ni mti unaovumilia ukame sana, na kamwe matawi yake hayapotezi rangi yake ya ukijani, hata kama yatapitia ukame mkali.

Ndio maana utaona kipindi Eliya anamkimbia Yezebeli, tayari dunia nzima ilikuwa ni jangwa kwasababu mvua haikunyesha kwa miaka mitatu na nusu, na Eliya anauona mretemu na kukaa chini ya uvuli wake, sasa kikawaida mti uliokauka na ukame hauwezi kuwa na uvuli.

1 Wafalme 19:4 “Lakini yeye mwenyewe akaendelea katika jangwa mwendo wa siku moja, akaenda akaketi CHINI YA MRETEMU. Akajiombea roho yake afe, akasema, Yatosha; sasa, Ee BWANA, uiondoe roho yangu; kwa kuwa mimi si mwema kuliko baba zangu.

5 Naye akajinyosha akalala chini ya MRETEMU; na tazama, malaika akamgusa, akamwambia, Inuka, ule”

Kutokana na sifa hiyo, na jinsi malaika alivyomtembelea Eliya alipokuwa chini ya huo mretemu(au mtarakwa), basi inaaminika kuwa mti huo, una miujiza fulani kiroho.

Vile vile miti hii ya Miteremu/mitarakwa inatumika katika tamaduni nyingi kama miti ya Krismas (Chrismass tree).

Asili ya mti huo kutumika kama alama ya Krismasi ni hadithi ya inayoaminika na baadhi ya watu kuwa kipindi Herode anataka kumwua mtoto Yesu, pale alipotoa amri ya kuuawa kwa watoto wote walio chini ya umri wa miaka miwili, inaaminika kuwa askari wa Herode walipomkaribia Yusufu na Mariamu ili wamwue mtoto, walikuwa karibu na huu mti wa Mteremu, na ghafla ukawafungukia matawi yake yakawaficha, askari walipokuja hawakumwona Yusufu, Mariamu pamoja na mtoto.

Hiyo ndio maana mpaka leo, watu wanautumia mti huo kama alama au nembo  ya Krismas.

Lakini swali ni je!. Ni kweli mtu huo umebeba miujiza yoyote kiroho?.

Jibu ni la!. Mti wa Mretemu/Mtarakwa hauna muujiza wowote kiroho, ni mti tu kama miti mingine, sifa yake ya kuvumilia ukame ndiyo inayowachanganya wengi, lakini kiuhalisia ni mti tu kama miti mingine.

Na zaidi sana, si kweli kwamba mti huo ulimsaidia Mariamu na Yusufu kuwalinda dhidi ya Mauaji ya Bwana Yesu.. Hizi ni hadithi za kutunga, ambazo zimetungwa kwa uerevu wa akili za watu, uliovuviwa na shetani mwenyewe.

Kwasababu Yusufu tayari alikuwa ameshaondoka Bethlehemu kabla ya Herode kuanza mauaji. Hivyo kusema kwamba mti uliwasaidia huo ni uongo wa shetani.

Na si tu mti huu ni wa kawaida, bali hata miti mingine yote haina miujiza yoyote kiroho, kitu pekee ambacho kinaweza kutuletea miujiza chanya katika maisha yetu ni KUISHI MAISHA MAKAMILIFU na kitu pekee kinachoweza kutuharibia maisha yetu ya hapa na yajayo ni MAISHA YA DHAMBI..Na si miti wala kitu kingine chochote.

Hivyo kwa hitimisho, ni kuwa Mretemu ni mti wa kawaida, na hauna muujiza wowote kiroho.

Kama hujaokoka, kumbuka hizi ni siku za mwisho, na Yesu yupo mlangoni kurudi. Mwamini leo, akuoshe dhambi zako, na kukupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Mwaloni ni nini? Na je unafunua nini rohoni?

Mti wa MLOZI alioonyeshwa nabii Yeremia 1:12 tafsiri yake ni nini?

Mti wa Mshita ni mti wa namna gani?

Uasherati wa Kiroho maana yake nini?

ALITOKA HUKO, AKAENDA MAHALI KARIBU NA JANGWA.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
JOACHIM MEGABE
JOACHIM MEGABE
1 year ago

Swali langu jingine, wakati ule wa nabii eliya, kwamba aliomba mvua haikunyesha muda wa miaka mitatu na nusu, mbona mimi nimeona tu kwa miaka mitatu tu?

JOACHIM MEGABE
JOACHIM MEGABE
1 year ago

Bwana asifiwe, naomba kuuliza swali, ukisoma kitabu cha 1Wafalme 13:18-20, kuna nabii hapo alijitokeza kwa nabii mwenzie na kumdanganya mwisho akawa amekiuka yale maagizo ya Bwana,halafu ukiendelea kusoma utaona nabii huyo huyo anamuambia tena huyo nabii mwenzie kwamba neno la Bwana limemuijia na kumuambia kuhusu kosa alilofanya huyo nabii mwenzie mpaka na adhabu akaipata ya kuliwa na simba, naomba ufafanuzi hapo imekaaje hiyo huyo nabii kumdanganya mwenzie?