Nini maana ya Mithali 27:21  inaposema “mtu hujaribiwa kwa sifa zake?”

Nini maana ya Mithali 27:21  inaposema “mtu hujaribiwa kwa sifa zake?”

SWALI: Nini maana ya Mithali 27:21  inaposema “Kalibu ni kwa fedha, na tanuru kwa dhahabu; Na mtu hujaribiwa kwa sifa zake”


JIBU: Kalibu na tanuru hizi ni sehemu za moto, ambapo, madini kama ya shaba, fedha, au dhahabu yanapitishwa na kuyeyushwa  ili kutenganisha uchafu uliogandamana na madini hayo. Hivyo hakuna namna nyingine ambayo unaweza kuifanya dhahabu au fedha ing’ae isipokuwa kuvipitisha kwenye matanuru hayo makali ya moto yaliyotengenezwa, na baadaye yatokee katika uzuri wake.

Vivyo hivyo na hapo anasema, ili kuupima moyo wa Mtu, kama ni kweli ndivyo alivyo au sivyo si katika kitu kingine chochote bali katika SIFA zake?

Sasa sifa zake ni zipi?

Ni vitu ambavyo vinavyoweza kumfanya asifiwe katika hivyo, Kwamfano, labda kipaji chake, cha kuimba. Ukimwona mtu hakengeushwi na kipawa hicho, yaani kiburi hakinyanyuki, staha inadumu, nidhamu na unyenyekevu unakaa naye, ijapokuwa ni maarufu, lakini viwango chake vya kiroho ni vilevile. Basi huyu ni mtu aliyekamilika kweli.

Au mwingine, Bwana kamjalia kupata pesa nyingi hivyo amekuwa tajiri sana na kuwazidi wengi. Lakini utajiri wake, haumfanyi adharau wengine, haumfanyi asimwabudu Mungu, haumfanyi achague watu wa kuishi nao, haumfanyi asiwasaidie wengine. Huyu ujue ni dhahabu safi kwelikweli, tabia yake ya mwanzo ilikuwa ni kweli.

Utakuta Mwingine labda kapata Elimu kubwa kuwazidi wengine, akabadilika tabia, akawa tena hajichanganyi na walio chini yake, kama ilivyokuwa zamani, hana muda wa kupokea simu za watu ambao anawaona hawamsaidii, hana nafasi ya kuhudhuria kwenye makanisa ambayo hayana wasomi, tofauti na alipokuwa hana elimu kubwa aliishi na kila mtu. moto wake umemtambulisha kwa sifa zake.

Vivyo hivyo kila jambo ambalo utasifiwa kwalo, iwe ni uzuri wako, hapo ndipo patakapoeleza tabia zako. Unajiwekaje wekaje, je! Hiyo ndio sababu ya wewe kutembea na vimini barabarani na suruali, au ndio sababu ya wewe kujisitiri.

Hivyo hekima inatupa kipimo sahihi cha kumtambua mtu alivyo rohoni. Sio katika mazungumzo yake, au kutenda kwake sasa, bali katika vitu vitakavyompa Sifa. Hapo paangalie sana. Utakuta  ni mtumishi wa Mungu kweli kweli na huduma yake ilipokuwa changa, alikuwa ni mnyenyekevu, mwombaji, anahubiri kweli ya Neno la Mungu, anawasaidia watu wote. Lakini pindi ilipokuwa na imejulikana sana, au huduma ipo katika daraja lingine, amebadilika, na kuwa kama mtu spesheli kama kiongozi wa nchi, mpaka umwone, lazima uwe na kadi yako ya mwaliko tena wa kiwango Fulani cha fedha, mafundisho anayoyahubiri ni ya kujinadi, au kujisifia yeye. Hapo ndipo panapoeleza tabia halisi ya huyo mhubiri, na sio kule chini alipokuwepo. Kule alikuwa anaigiza tu.

Hivyo, kila mmoja ajichunguze, je! Nitakaposifiwa, au nitakapopandishwa viwango vingine, nitabakia kuwa yeye Yule kama Bwana wetu Yesu alivyokuwa. Nikipata kazi, nitapoa kimaombi? Nikiolewa nitawadharau ambao hawajaolewa?.

 Bwana atusaidie.

Je! Upo ndani ya Kristo?  Kama ni la! Unangojea nini? Tambua kuwa tupo katika dakika za majeruhi, usiishi kama mnyama ambaye anaamka asubuhi anachowaza ni kula tu, ikifika jioni ni kurudi bandani. Wewe umewekewa kusudi la kufanya hapa duniani, na lenyewe ni kuyatenda mapenzi ya Mungu, na sio kula na kunywa na kujenga nyumba. Embu geuka sasa mkabidhi YESU maisha yako, ili parapanda ya mwisho itakapolia uwe na uhakika wa kwenda naye katika unyakuo. Ikiwa upo tayari kutubu dhambi zako leo, basi fungua hapa kwa mwongozo huo>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Kalibu maana yake nini? (Mathayo 6:30).

Wakati wakina Shadraka wanatupwa katika tanuru la moto, Danieli alikuwa wapi?

HEKIMA NI NINI? NA UFAHAMU UNAPATIKANA WAPI?

Nini maana ya Mithali 5:15-18 anaposema Unywe maji ya birika lako mwenyewe?

Fahamu maana ya Mithali 29:4 “Mfalme huithibitisha nchi kwa hukumu; Bali yeye apokeaye rushwa huipindua.

Shetani anaishi wapi, Je! Amefungwa au yupo kuzimu?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments