Je biblia inatuhubiria kucheza Mieleka au kuitazama? (Mwanzo 32:24)

Je biblia inatuhubiria kucheza Mieleka au kuitazama? (Mwanzo 32:24)

Swali: Tunaona Yakobo alishindana mweleka na Malaika wa Mungu (Mwanzo 32:24), je kuna ubaya wowote na sisi kutazama mieleka kwenye Tv?.

Jibu NI La! Biblia haijawahi kutufundisha wakati wowote kuipenda dunia, Zaidi sana imesema tusiipende dunia, wala mambo yaliyomo duniani na kama tukiipenda dunia na mambo yake basi upendo wa Mungu haupo ndani yetu. (1Yohana 2:15).

Na Mieleka ni moja ya mambo ya kidunia, pamoja na mipira!.

Sasa utajiuliza mbona Yakobo alipigana Mieleka katika Mwanzo 32:24?

Yakobo hakuketi na kupanga mechi na yule Malaika, kana kwamba walikuwa wanaburudishana au kupimana nguvu.. La! Haikuwa hivyo.. Kilichotokea ni kwamba Malaika wa Mungu alimtembelea Yakobo katika mwili wa kibinadamu, na baada ya kumaliza kilichompeleka pale, wakati anataka kuondoka, Yakobo alimzuia asiondoke, lengo ni kutaka kupokea Baraka kutoka kwa Malaika yule.

Sasa wakati Malaika anataka kuondoka, Yakobo anamvuta na kumrudisha nyuma mwisho ukageuka kuwa mweleka, lakini si wa lengo la kujiburudisha wala kudhuriana, wala kupimana nguvu bali la kuzuiana!!!

Mwanzo 32:24 “Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri. 

25 Naye alipoona ya kuwa hamshindi, alimgusa panapo uvungu wa paja lake; ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye. 

26 Akasema, Niache, niende, maana kunapambazuka. Akasema, Sikuachi, usiponibariki. 

27 Akamwuliza, Jina lako n’nani? Akasema, Yakobo. 

28 Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda. 

29 Yakobo akamwuliza, akasema, Niambie, tafadhali, jina lako? Akasema, Kwa nini waniuliza jina langu? Akambariki huko.

30 Yakobo akapaita mahali pale, Penueli, maana alisema, Nimeonana na Mungu uso kwa uso, na nafsi yangu imeokoka”.

Lakini Mieleka inayoonekana kwenye Luninga zama hizi za mwisho ni Mapando ya shetani asilimia mia, Ndio maana utaona wanaocheza michezo hiyo wanakuwa wapo nusu uchi!. na wanatangaza vitu vya kiulimwengu.

Hivyo na sisi hatupaswi kupigana Mieleka ya kidunia isiyo na maana, badala yake tupigane Mieleka ya kiroho ambayo matokeo yake ni sisi kubarikiwa. Tung’ang’anie baraka zetu zilizoandikwa katika NENO LA MUNGU, (biblia). Na pia tushidane kwa kumponda yule adui yetu shetani chini ya miguu yetu.

Waefeso 6:12 “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama”

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Kucheza karata ni sahihi kwa Mtu aliye MKRITO?

Je ushabiki wa mpira ni dhambi?

MWINUE YESU KRISTO KATIKA MAISHA YAKO.

Je Mungu anaweza kumdanganya mtu?

Kwanini Yakobo alimshinda Mungu, Je! Mungu huwa anashindwa na wanadamu?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments