Kucheza karata ni sahihi kwa Mtu aliye MKRITO?

Kucheza karata ni sahihi kwa Mtu aliye MKRITO?

JIBU: Kwanza kabisa hebu tujifunze juu ya hili.. “Ni kwanini Shule nyingi za bweni karibia zote, zinakataza watoto kuwa na simu au kucheza karata au magemu au kuangalia movie?”..unafikiri ni kwanini?..Jibu ni rahisi ni kwasababu vitu hivyo vinapotumiwa na wanafunzi vinawasababishia kwa namna moja au nyingine kutokuwa na kiasi na matokeo yake inawapelekea kusahau kilichowapeleka shule na mwisho wa siku ni kufeli tu, Kwani ule muda ambao mtoto angepaswa afikirie masomo yake anajikuta anafikiria ile movie aliyoiangalia jana usiku au zile karata alizokuwa anazicheza au atakazozicheza, na mwisho wa siku hiyo inabadilika na kuwa hasara kubwa kwa mwanafunzi, na kwa shule na kwa Taifa kwa ujumla…Sasa kama wanadamu wanauwezo wa kuwa na hekima kama hiyo ya kupambanua hayo mambo yanayofaa na yasiyofaa…unadhani kwa Mungu itakuaje?..Ni dhahiri kuwa itakuwa ni zaidi ya hapo. Biblia inasema tusiupende ulimwengu:

1 Yohana 2:15 “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.

16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.

17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele”.

Unaona? Kwanini biblia inasema tusiipende dunia?..sio kwamba dunia ni mbaya, sio kwamba michezo ni mibaya, wala sio kwamba kustareheka ni kubaya…hapana vitu vyote hivyo sio vibaya kama vikitumiwa ipasavyo…Ubaya ni kwamba tunaishi duniani kwa muda! tupo darasani kwa kipindi kifupi sana, tukiyafuata hayo mambo ya duniani basi tujue kuwa hatutazingatia mambo ya Mungu, na matokeo yake ni kufeli na hivyo kupata hasara ya nafsi zetu. na Mungu wetu hataki tupotee ndio maana anatuambia tukae mbali na mambo hayo ya ulimwengu… Sisi (watoto wa Mungu) Ni sawa na mwanafunzi walioko shuleni, tena shule za Bweni…Ni wasafiri tu wa hapa duniani, tunatengeneza maisha yetu sasa ili tuwe na maisha bora huko katika umilele unaokuja…

Hivyo kama ni starehe, basi tutazifanya sana katika hiyo mbingu mpya na nchi mpya inayotungojea huko mbeleni, kama ni kufurahi, kama ni kuzurura, kama ni kucheza na kujiburudisha kwa jinsi tupendavyo basi tutafanya sana katika hiyo Yerusalemu mpya ambayo Mungu ametuandalia huko mbeleni, ..…lakini sasa katika ulimwengu huu sio wakati wake…Hayo mambo ni ya wakati wa zamani zijazo za wakati wa ulimwengu ujao, ambapo huko kutakuwa hakuna kusoma tena biblia wala kuhubiri, wala kufunga, wala hakutakuwa na majaribu tena, wala maumivu wala kula kwa jasho, wala kujizuia…hayo mambo hayatakuwepo kule, kule itakuwa ni sehemu ya furaha, ya kufanikiwa na ya uhuru usio na kifani. Ndivyo maandiko yanavyosema.

 Lakini Wengi wanasema ni ushamba kujinyima raha katika ulimwengu huu, lakini hao hao hawajui kuwa ni ushamba mkubwa zaidi kujinyima raha za umilele unaokuja huko mbeleni…jiulize ukifa leo huko utaenda kuwa mgeni wa nani?. Kumbuka Mwanafunzi mwenye busara ni yule anayezingatia kilichompeleka shuleni..sio ushamba mwanafunzi kujizuia kuangalia movie ili atumie muda wake vizuri katika masomo, wala si ushamba mwanafunzi anapojizuia kuzurura zurura huku na huko na badala yake muda wote unautumia kutafakari masomo ili mitihani aje kufaulu vizuri…anajinyima hivyo vyote kwasababu anajua ni kwa faida yake mwenyewe na ni kwa muda mfupi tu, ..anajua siku akimaliza shule na kufaulu, atayafanya hayo sana na zaidi ya hayo… 

Na sisi tunapaswa tuzingatie kwasasa kile kilichotuleta duniani. Sio ushamba kuukataa ulimwengu, sio kila kitu kinachoja mbele yetu tukijaribu tu, vingine vinatupoteza muda, vingine vinatuondoa katika dira ya wokovu, vingine vinaturudisha nyuma… Ni wajibu wetu kuenenda katika hii dunia kwa werevu. Kwahiyo kwa kuhitimisha, mchezo wa karata haufai kwa mtoto wa Mungu, utacheza karata masaa mawili lakini kushika biblia dakika tano huwezi, utaangalia muvi series hata masaa nane lakini biblia dakika 10 huwezi…huoni kuna roho nyuma ya huo mchezo?..roho inayokufanya kutokuzingatia mambo ya msingi ya Imani. Hiyo ni roho inayokupeleka katika kufeli maisha. Hivyo tuwe makini sana.

Ubarikiwe.

Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp


Mada Nyinginezo:

JE! KUSHIRIKI AU KUJIHUSISHA KWENYE MICHEZO NI DHAMBI?.

KISASI NI JUU YA BWANA.

JINSI MWISHO ULIVYOKARIBIA.

MADHARA YA KUUPIZIA MAAGIZO YA MSINGI MUNGU ANAYOKUPA.

TWEKA MPAKA VILINDINI.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
3 years ago

Kama tatizo ni kupoteza muda je kushinda kwenye face book penyewe sio tatizo?