Je ni kweli Tumejengwa juu ya Mitume na Manabii? (Waefeso 2:20)

Je ni kweli Tumejengwa juu ya Mitume na Manabii? (Waefeso 2:20)

Jibu: Tusome,


Waefeso 2:20 “Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni”

Hapo maandiko yanasema tumejengwa juu ya “Msingi wa Mitume na Manabii “na si juu ya “Mitume na Manabii” .. Na pia inasema tumejengwa juu ya “Msingi” na si juu ya Misingi ya mitume na manabii. Ikiwa na maana kuwa Msingi ni mmoja tu, ambao tumejegwa juu yake, (mbele kidogo tutakuja kuuona huo msingi ni nini).


Sasa yapo maswali mawili hapo ya kujiuliza; 1) Hawa Mitume na Manabii ni akina nani na 2) Huo msingi ni nini?


1) Mitume na Manabii:


Mitume na Manabii wanaozungumziwa hapa katika Waefeso 2:20 sio hawa waliopo sasa, Bali ni wale walioandika biblia, kama Musa, Yeremia, Hosea, Ezekieli na Malaki vile vile mitume wale 12 wa Bwana pamoja na wengine kama akina Paulo, ambao waliandika biblia.


Mtu yeyote aliyepo sasa, au atakayekuja kutokea na kujiita mtume au nabii, basi afahamu kuwa andiko hilo la Waefeso 2:20 halimhusu hata kidogo. Na shetani amewapandikiza watu wengi kiburi (watu wanaojulikana kama mitume na manabii wa leo), na kuanza kujivuna kuwa wao ndio Msingi wa kanisa.. Jambo ambalo si la kweli hata kidogo.


2) Msingi


Msingi ambao sisi tumejengwa juu yake ni ule waliokuwa nao Mitume, ikiwa na maana kuwa kile Mitume walichokifanya msingi, ndicho hicho hicho sisi (kanisa la Mungu) tunajengwa juu yake. Sasa ni kitu gani Mitume na Manabii wa kwenye biblia walikifanya msingi?… Hicho si kingine zaidi ya YESU KRISTO MWENYEWE!!!. Huyu ndiye Msingi wa kanisa na ndiye aliyekuwa msingi wa mitume, na ndio msingi wetu sisi na bado ataendelea kuwa msingi siku zote.


1Wakorintho 3:11 “Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, YESU KRISTO”.


YESU KRISTO ndio Mwamba ule ambao yeye mwenyewe alisema kuwa kanisa lake litajengwa juu yake.


Mathayo 16:13 “Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani?
14 Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii.
15 Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?
16 Simoni Petro akajibu akasema, WEWE NDIWE KRISTO, MWANA WA MUNGU ALIYE HAI.
17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.
18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda”.


Umeona? Mwamba unaonenewa hapo sio Petro bali ni yeye YESU MWENYEWE!.. yaani huo Ufunuo Petro alioupata wa YESU KUWA MWANA WA MUNGU Ndio MSINGI, na NDIO MWAMBA ambao kanisa litajengwa juu yake.


Kanisa lolote leo ambao YESU sio kiini cha Imani hiyo, hilo sio kanisa la kweli, vile vile imani yoyote ile isiyomweka YESU kama msingi badala yake inawemweka mwanadamu mwingine au mnyama au sanamu basi imani hiyo ni imani ya Uongo n.k


Mahubiri yoyote yasiyomweka YESU msingi, hayo ni mahubiri kutoka kwa Yule adui.
Mtumishi yoyote Yule, awe mchungaji, mwalimu, mtume, nabii au mwinjilisti asiyemweka YESU kama kiini na kitovu cha Mafundisho huyo si wa kweli, kwa mujibu wa maandiko.
Vile vile mtu yeyote ajiitaye Mkristo na Yesu si msingi wa maisha yake, huyo ni mkristo jina tu wa uongo.
Bwana atusaidie tumweke Yesu msingi wa maisha yetu.


Maran atha!.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Je huduma za mitume na manabii, zinaendelea kufanya kazi hadi sasa?

Nitamjuaje nabii wa Uongo?

UNAWAFAHAMU MANABII WA UONGO?

Wana wa Manabii walikuwa ni watu gani?

Kiti cha Rehema kilikuwaje? (Kutoka 40:20)

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments