Kiti cha Musa ni kipi? (Mathayo 23:2)

Kiti cha Musa ni kipi? (Mathayo 23:2)

Swali: Biblia ina maana gani kusema Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa? Je hiki kiti cha Musa ndio kipi?Jibu: Turejee,

Mathayo 23:2 “Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa”

“Kiti cha Musa” maana yake ni “Nafasi ya Musa”.. Leo hii tukisema mtu kaketi katika kiti cha Uraisi, maana yake ni kuwa “kachukua nafasi ya Uraisi”.

Sasa Musa alikuwa na nafasi gani?

Musa alikuwa na nafasi kuu mbili (2) mbele za wana wa Israeli.

   1) UALIMU.

Mtu wa Kwanza kuwafundisha wana wa Israeli HUKUMU, AMRI NA SHERIA za Mungu alikuwa ni MUSA.

Kumbukumbu 4: 14 “Bwana akaniamuru wakati ule NIWAFUNDISHE maagizo na hukumu, mpate kuzitenda katika nchi ile mtakayoivukia ili kuimiliki.

15 Jihadharini nafsi zenu basi; maana hamkuona umbo la namna yo yote siku ile Bwana aliyosema nanyi kutoka kati ya moto;

16 msije mkajiharibu nafsi zenu, mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa sura yo yote, mfano wa mwanamume au mwanamke”.

Na mahubiri yake yaliendelea kuwa msingi wa marejeo kwa vizazi na vizazi mbeleni.

2) UONGOZI.

Hii ni nafasi ya pili aliyokuwa nayo Musa mbele ya wana wa Israeli:
Maandiko yanasema Mungu alimfanya Musa kuwa “Mkuu sana” mbele ya Misri na mbele ya wana wa Israeli. Kiasi kwamba maamuzi ya mwisho yalikuwa yanatoka kwake, kwa lugha nyepesi alikuwa ni kama Mfalme.

Kutoka 11:3 “…Zaidi ya hayo, huyo Musa ALIKUWA NI MKUU SANA katika nchi ya Misri, machoni pa watumishi wa Farao, na machoni pa watu wake”.

Soma pia Kutoka 18:13-24, utaona nafasi ya Musa katika kuwaamua Israeli.

Sasa baada ya Musa kuondoka (yaani kufa), Mafarisayo na Waandishi wakajiweka katika nafasi yake, maana yake wao ndio wakawa WAALIMU kama alivyokuwa Musa, na pia wakajiweka kuwa VIONGOZI kama alivyoukwa Musa, kiasi kwamba maamuzi ya mwisho yalikuwa yanatoka kwao.

Lakini ni heri kama wangekuwa wameketi kwenye nafasi hiyo ya Musa, na wakawa kama Musa..(yaani wacha Mungu kama Musa, au wapole kama Musa)..

Lakini wao walikuwa ni kinyume chake, walikuwa wanawatawala watu na kuwahukumu kwa sheria ya Musa lakini wao wenyewe ni wanafki mioyoni mwao.. mioyo yao ilikuwa ipo mbali na Mungu ingawa kwa nje wanaonekana ni waamuzi wazuri na viongozi wazuri wenye kusifiwa, lakini ndani yao wamejaa unafiki!.

Na Bwana YESU anatuonya tusiwe kama wao..

Mathayo 23:2 “Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa”

3 basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi

4 Wao hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao.

5 Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao;

6 hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi mbele katika masinagogi,

7 na kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu, Rabi.

8 Bali ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu.

9 Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni.

10 Wala msiitwe viongozi; maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo.

11 NAYE ALIYE MKUBWA WENU ATAKUWA MTUMISHI WENU.

12 Na ye yote atakayejikweza, atadhiliwa; na ye yote atakayejidhili, atakwezwa”.

Je YESU KRISTO ni Bwana na Mwokozi wa maisha yako?..Je una uhakika jina lako lipo katika kitabu cha uzima?.. Kama bado YESU hayupo maishani mwako ni heri ukampokea leo, maana saa ya wokovu na wakati uliokubali ni sasa.
Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

NI KIZAZI KIPI WEWE UPO?

Kiti cha Rehema kilikuwaje? (Kutoka 40:20)

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA

JE! UNAYO NAFASI MBINGUNI?

USIWE NA TAMAA YA CHAKULA KINGINE.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments