Watoao riba ni akina nani? (Mathayo 25:27)

Watoao riba ni akina nani? (Mathayo 25:27)

Swali: Je Bwana alimaanisha nini kusema “ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba” Je alikuwa na maana gani kusema vile?


Jibu: Mathayo 2:27 “basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.

28  Basi, mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi”

Ukisoma habari hiyo kuanzia juu utaona ni mfano uliokuwa unazungumzia watumwa ambao Bwana wao aliwapa talanta, na yule aliyepokea talanta tano, alizalisha nyingine tano, huenda kwa biashara aliyoifungua…na yule aliyepokea talanta mbili naye pia akazalisha nyingine mbili huwenda kutokana biashara aliyoifungua..

Lakini yule aliyepokea Moja, hakuenda kuifanyia kazi badala yake alienda kuificha chini ya ardhi, na siku ya mwisho akamrejeshea Bwana wake talanta ile ile moja aliyoipokea kutoka kwa Bwana wake, Lakini tunasoma Bwana wake akamkemea na kumwambia kuwa ni mtumwa “mbaya na mlegevu”.

Maana yake kama ameshindwa kabisa kwenda kuifanyia kazi basi angalau angeiweka kwa watoao riba, ..maana yake akakopeshe watu ambao wao wataenda kuizungusha ile fedha na hatimaye kumrejeshea iliyo yake na faida yake, lakini huyu mtumwa hakufikiri hata hilo, badala yake alienda kuifukia chini ya ardhi..

Sasa kiroho talanta zinafananishwa na “kipawa au uwezo” wowote ambao mtu kapewa na Mungu, unaomtofautisha yeye na mwingine.

Sasa kama mtu si Mtumishi wa madhabahuni, si mchungaji, si mwalimu, si mwinjilisti wa kwenda huku na kule kuhubiri habari njema… wala haoni kama anaweza kufanya kazi moja wapo ya hizo, lakini Mungu kamjalia kauwezo Fulani cha kifedha,

Basi kuliko kukaa bila kufanya kazi yoyote ya Mungu, ni afadhali fedha zake hizo ziwe chache au nyingi, aziwekeze katika injili (maana yake awape wanaokwenda kuieneza injili huku na kule) ili matunda yatakayopatikana kupitia injili watakaohubiri wengine kwa sapoti yake, basi na yeye awe mshirika wa matunda hayo kwasababu kachangia injili hiyo.. (Hiyo ndio maana ya kuweka fedha kwa watoa riba). Yeye  hajahubiri lakini kapeleka nguvu zake kwa wanaohubiri.

Lakini kama haubiri, haufanyi uinjilisti wowote, si mwalimu, si mchungaji, na hutaji hata moja ya fedha zako kuipeka kwenye injili, mwisho wake utakuwa kama wa huyu aliyeificha talanta yake ardhini.

Luka 16:9  “Nami nawaambia, Jifanyieni rafiki kwa mali ya udhalimu, ili itakapokosekana wawakaribishe katika makao ya milele”.

Bwana atusaidie tutumie talanta zetu vizuri.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

ANGALIA JINSI USIKIAVYO:

talanta ni nini

BASI NIKAOGOPA, NIKAENDA NIKAIFICHA TALANTA YAKO.

TENGENEZA MAMBO YA NYUMBA YAKO.

Azidishaye mali yake kwa riba, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments