Kwanini Bwana achukizwe na mtumwa yule aliyeficha talanta yake ardhini? (Mathayo 25:26-30)

Kwanini Bwana achukizwe na mtumwa yule aliyeficha talanta yake ardhini? (Mathayo 25:26-30)

Swali: Kwani kulikuwa na ubaya gani, wa bwana yule kurudisha talanta ile moja?, kwani hakupoteza kitu wala hajaleta hasara yoyote?..je kulikuwa na sababu gani ya yeye kuhukumiwa vile?.


Jibu: Ili tuweze kuelewa vizuri sababu ya mtumwa yule kuhukumiwa vile, tuisome habari yenyewe kwa uchache..

Mathayo 25:14  “Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita WATUMWA WAKE, akaweka kwao MALI ZAKE.

15  Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri”.

Nataka tuzingatie hayo maneno mawili “Watumwa wake” na “Mali zake”.

Kwa haraka tukiisoma habari hii tunaweza kutafakari kuwa huyu mtu aliwekeza mali zake kwa “rafiki zake” au “ndugu zake”..

Ingekuwa heri kama ingekuwa ni “rafiki zake” au “ndugu zake” kwani hata wasingeleta faida yoyote angeweza kuwaelewa  lakini aliwekeza mali zake kwa “watumwa wake” ambao ni watu anaowalipa mshahara huenda kila siku au kil amwisho wa mwezi.

Sasa ili tuelewe vizuri, tengeneza picha una biashara yako (labda duka) halafu umeajiri mfanya kazi pale na kukubaliana naye mshahara, na ukaondoka na kurudi jioni na kukuta hajafanya kazi yoyote na Zaidi anakuambia fedha zako za mtaji zipo pale pale hajazigusa.

Bila shaka utachukizwa naye..kwanini?..cha kwanza ulitegemea kupata faida ndio maana wewe ukamweka pale, pili mshahara wake unatokana na faida katika hiyo kazi, kwa utendaji wake..

Kwahiyo kama hatafanya kazi yoyote na mwisho wa mwisho wa siku au mwezi atataka mshahara je utamlipa nini?…maana utakapofika mwisho wa mwezi atakudai mshahara, na wewe umeshaingia naye mkataba wa kumlipa..

Kwahiyo ni wazi kuwa ni lazima utakasirika, kwasababu kutokufanya kwake kazi ni hasara kwako, kwasababu mwisho wa siku ni lazima utamlipa, hivyo anakurudisha nyuma hata kama hajagusa mtaji wako, lakini mwisho wa siku utaathirika wewe katika wakati wa kumlipa mshahara..Hivyo ni hasara!!!

Ndicho kilichowatokea yule mtumwa aliyeficha talanta aliyopewa na bwana wake, maana yake ni kweli kairudisha ile talanta kama ilivyo, lakini mwisho wa mwezi atataka mshara (kwasababu yeye ni mwajiriwa na si ndugu/rafiki).. sasa bosi wake atatolea wapi fedha ya kumlipa ikiwa hajazalisha chochote?..

Ndio maana bwana wake akamwambia ni heri hata angeipeleka kwa watoa riba kuliko kuificha ardhini.

Hili ni fundisho kamili kwa wakristo kwamba vipawa na karama na uwezo tuliojaliwa na Bwana basi tutumie katika kumtumikia Mungu pasipo udhuru, kwasababu sisi ni watumwa wake!, ametuweka kwa faida yake…

Bwana atusaidie tusifiche talanta zetu ardhini bali tuzitendee kazi au tuzipeleke kwa watoa riba.

Mathayo 25:27  “basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.

28  Basi, mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi.

29  Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.

30  Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”

Kufahamu kwa mapana maana ya “kupeleka fedha kwa watoa riba”, basi fungua hapa >>>Watoao riba ni akina nani? (Mathayo 25:27)

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

JINSI YA KUISHINDA HALI YA MSONGO WA MAWAZO.

BASI NIKAOGOPA, NIKAENDA NIKAIFICHA TALANTA YAKO.

JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 1)

Nini maana ya.. “Utoapo sadaka mkono wako wa kuume usijue ufanyalo mkono wako wa kushoto”

Talanta ni nini katika biblia (Mathayo 25:14-30)

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments