Kwanini MUNGU alimzuia Daudi asimjengee HEKALU? (1Nyakati 17:12)

Kwanini MUNGU alimzuia Daudi asimjengee HEKALU? (1Nyakati 17:12)

Jibu: Turejee…

1 Nyakati 17:11-12 “Hata itakuwa, siku zako zitakapotimia, uende na babazo, nitainua mzao wako nyuma yako, atakayekuwa wa wana wako; nami nitaufanya imara ufalme wake.

12 Yeye ndiye atakayenijengea nyumba, nami nitakifanya imara kiti cha enzi cha ufalme wake milele”.

Unabii huu unamuhusu BWANA YESU KRISTO, na si SULEMANI. yeye (YESU) ndiye atakayetokea na kuijenga nyumba ya MUNGU (Hekalu) lililo kamilifu na takatifu,  na nyumba hiyo ni MWILI wake (Yohana 2:19-22).

Lakini pamoja na hayo pia Hekalu la damu na Nyama, Mungu alimzuia Daudi asilijenge KWASABABU alimwaga damu nyingi za hatia na zisizo za hatia, na kwasababu hiyo Mungu hakumruhusu aijenge nyumba ile bali mwanae Sulemani.

1  Nyakati 28:3 “Lakini Mungu akaniambia, Wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya jina langu, kwa sababu umekuwa mtu wa vita, nawe umemwaga damu ………………

5 tena katika wana wangu wote (kwani BWANA amenipa wana wengi), amemchagua Sulemani mwanangu ili aketi juu ya kiti cha enzi cha ufalme wa BWANA, juu ya Israeli.

6 Akaniambia, Sulemani, mwanao, ndiye atakayeijenga nyumba yangu na nyua zangu; kwa kuwa nimemchagua awe mwanangu, nami nitakuwa babaye”

Na ni damu za akina na Daudi alizozimwaga?.

   1.DAMU ZA MAADUI.

Daudi alikuwa ni mtu wa vita tangu ujana wake, yeye pamoja na mashujaa wake walikuwa ni watu wa kuua maadui zao kwa upanga, hilo likawa kizuizi kwa Daudi kuijenga nyumba ya Bwana.

   2. DAMU YA URIA.

Damu ya Uria, jemedari aliyoimwaga Daudi, ilikuwa ni kikwazo kikubwa cha Daudi kupata ruhusu ya kuijenga nyumba takatifu ya Mungu atakayokaa..

Kwani laiti Daudi angeijenga nyumba ile pamoja na tendo lake hilo alilolitenda la kumuua Uria na kumchukua mke wake, basi maadui wa Bwana wangeiona hiyo nyumba aliyoijenga na kukumbuka Daudi aliyoyafanya, wangepata sababu ya kukufuru na kukashifu ile nyumba sawasawa na maneno ya Bwana.

2 Samweli 12:13 “Daudi akamwambia Nathani, Nimemfanyia BWANA dhambi. Nathani akamwambia Daudi, BWANA naye ameiondoa dhambi yako; hutakufa.

14 Lakini, kwa kuwa kwa tendo hili umewapa adui za BWANA nafasi kubwa ya kukufuru, mtoto atakayezaliwa kwako hakika yake atakufa”.

Ni lipi tunaloweza kujifunza hapo?

Bwana hakuwahi kupendezwa na mauaji tangu mwanzo, watu wa kale waliruhusiwa kuua kwasababu ya ugumu wa mioyo yao, lakini tangu mwanzo Bwana alikataza mauaji Soma Kutoka 20:13.

Hivyo hatuwezi kuishi sasa kwa kuyaangalia matendo ya Daudi, kama Daudi aliua basi na sisi ndio tuue, kama Daudi alioa wake wengi basi na sisi ndio tuoe wake wengi n.k.

Bali tunamtazama YESU KRISTO sasa aliye Ukamilifu na Utimilifu wa sheria, yeye anasema…

Mathayo 5:38 “Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino;

39 Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili.

40 Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia.

41 Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili”.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Bwana alimaanisha nini kusema “Yeye aapaye kwa hekalu, huapa kwa hilo”? (Mathayo 23:20)

Daudi alikuwa na wake wangapi, na je ni halali kuwa na wake wengi?

Je! Habari iliyo katika 1Nyakati 21:25, na 2Samweli 24:24, ya Daudi kununua kiwanja  inajichanganya?

MAANA ROHO HUCHUNGUZA YOTE, HATA MAFUMBO YA MUNGU.

Nini maana ya hekima ya maskini haisikilizwi? (Mhubiri 9:16)

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments