Ni kipawa kipi hicho tusichoweza kukisifu jinsi ipasavyo?(2Wakorintho 9:15)

Ni kipawa kipi hicho tusichoweza kukisifu jinsi ipasavyo?(2Wakorintho 9:15)

SWALI: Ni kipawa kipi hicho tusichoweza kukisifu jinsi ipasavyo?

2 Wakorintho 9:15

[15]Mungu ashukuriwe kwa sababu ya kipawa chake, tusichoweza kukisifu kama ipasavyo.


 JIBU: Mungu alitupa mwana wake (Yesu Kristo), kama zawadi kwetu, ambaye anakaa ndani yetu kwa Roho wake Mtakatifu. 

Warumi 5:17

[17]Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo. 

Yesu (kupitia Roho Mtakatifu), ni kipawa kikubwa ambacho hatuwezi kukielezea uzuri wake(kukisifu), jinsi ipasavyo.

 Ndani ya Yesu ni hakika tunapata vitu vyote (vya rohoni na mwilini)

Hivyo kulingana na vifungu hivyo ukianzia tokea juu katika sura hiyo ya tisa (9), anaegemea hasaa  katika eneo la kubarikiwa na Mungu katika baraka za mwilini. ambazo huja ndani ya kipawa hichi cha Mungu.

2 Wakorintho 9:11

[11]mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu. 

Ni kweli hatuwezi kueleza kwa maneno haya jinsi gani Yesu alivyoleta ukombozi katika maeneo mengi zaidi ya yale tunayoyadhani, si tu katika roho zetu, bali mpaka miili yetu, dunia yetu, uchumi wetu, familia zetu, magonjwa yetu, wanyama wetu, jamii yetu, ardhi zetu,  n.k. kipawa hichi kila mahali kinatibu.

Hivyo si rahisi kukisifu kwa jinsi ipasavyo. Ndio maana kwa Yesu tumetia nanga, yeye ndio utoshelevu wetu wote, hatuna haja kwa mtu mwingine yeyote zaidi yake, na ndivyo ilivyo. Hekima ya Mungu iliona hilo ndio maana hakutupa sisi wanadamu kitu kingine zaidi ya Yesu Kristo tu.

 Ashukuriwe Mungu kwa zawadi hii. Utukufu heshima na shukrani vimrudie yeye mile na milele. Amina.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>

https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Maana ya 2Wakorintho 9:11 mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote

Kiti cha Musa ni kipi? (Mathayo 23:2)

USINIPE UMASKINI WALA UTAJIRI. (Mithali 30)

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments