SI KWA FAIDA YA MWENYEZI, BALI KWA FAIDA YETU.

SI KWA FAIDA YA MWENYEZI, BALI KWA FAIDA YETU.

Tunapotenda Mema ni kwa faida yetu na si ya Mungu..kadhalika tunapofanya maovu ni kwa hasara yetu sisi na si hasara ya Mungu. Kwa mfano mtu anayezini biblia inasema anatenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe anafanya jambo litakalomwangamiza yeye mwenyewe.. maana yake anakuwa hana tofauti na mtu anayejiua…

Mithali 6:32 “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.33 Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika”

Kadhalika mtu anayeiba au anayeua, HAMKOMOI MUNGU..bali anafanya jambo ambalo litawaumiza wanadamu wenzake na hali kadhalika litakalomwaribu yeye mwenyewe baadaye. Na dhambi nyingine zote ni hivyo hivyo…zina madhara kwetu na si kwa Mungu…Vivyo hivyo tunapotenda mema, mema hayo tunapoyafanya si kwa faida ya Mungu bali kwa faida yetu sisi wenyewe..Bwana anapotuasa na kututaka tutende mema si kwaajili yake yeye, bali kwaajili yetu sisi..ni sawa na mtu anayekizuia kisu katika shingo ya mtu anayetaka kujiua..Ndivyo anavyofanya kwetu pale anapotuzuia tusifanye dhambi..ni kwa faida yetu si yake…endapo akituacha tu basi tutajimaliza na hakuna kitakachosalia…

Kwamfano Biblia inasema wapeni watu vitu nanyi mtapewa…(Luka 6:38) kipimo cha kujaa, na kushindiliwa hata kusukwa sukwa ndivyo watu watakavyowapa vifuani mwenu…kwamaana kipimo kile tupimacho ndicho tutakachopimiwa…Maana yake ni kwamba sio kwamba Mungu anatupa sheria ngumu ili yeye ajifurahishe moyo wake anapotuona tunamtii..hapana anafanya vile ili sisi tupate faida..yeye hatumwongezei chochote kwa wema wetu tunaoufanya…

Hivyo ukitenda mema na kuwapa watu vitu na wewe utapewa vitu siku moja kwa kiwango kile kile ulichowapa wengine…Kwahiyo mema ni kwa faida yetu sisi na si ya Mungu.

Kwahiyo Biblia inapotuonya tusizini, au tusifanye uasherati, au tusiibe, au tusiue, au tuwaheshimu wazazi wetu n.k ni kwafaida yetu ili tupate mema katika ulimwengu huu na ule unayokuja..Na si kwa sababu Mungu anapenda kutuangalia kama kwenye Tv huku duniani tukitenda mema, kwamba ndio chakula chake yeye..Ukifikiri/tukifikiri hivyo..tutakuwa bado hatujamwelewa huyu Mungu tunayemwabudu…

Soma maandiko haya:

Ayubu 35: 5 “Ziangalie mbingu ukaone; Na mawingu yaangalie, yaliyo juu kuliko wewe.

6 Ikiwa umefanya dhambi, umefanya nini juu yake? Yakiwa makosa yako yameongezeka, wamfanyia nini yeye?

7 Ikiwa u mwenye haki, wampa kitu gani? Au yeye hupokea nini mkononi mwako?

8 Uovu wako waweza kumwumiza mtu kama wewe; Na haki yako yaweza kumfaa mwanadamu”.

Umeona? Unapovaa vimini na suruali na kuonywa usivae kikahaba ni kwa faida yako mwanamke….Unapoua kwa kutoa mimba ni kwa hasara yako wewe na yule uliyemuua, …Unapojiongezea maasi juu ya maasi na dhambi juu ya dhambi, humpunguzii kitu Mungu kwasababu yeye haishi kwa dhambi zetu wala kwa haki yetu…Hivyo dhambi zako unazojiongezea juu kila siku ni sawa unasikia njaa na kukata kiungo chako kimoja kimoja kila siku ili ukile upunguze njaa..(hapo unajimaliza mwenyewe).

Unasikia mahubiri kila kona, ni kwasababu Mungu anakupenda na anataka upate faida wewe na si yeye..anataka usipate hasara wewe na si yeye..

Hili neno “hizi ni siku za mwisho” pengine umeshalisikia sasa hii ni mara ya elfu, na limeshakuchosha…lakini kipindi si kirefu hutalisikia tena kwasababu siku zenyewe zitakuwa zimeshatimia…Kristo atachukua walio wake na kila mtu atavuna alichokipanda akiwa hapa duniani. Na watakatifu watanyakuliwa..na dhiki kuu itaanza na siku ya Bwana itashuka ulimwenguni, wakati huo disko unazohudhuria sasa hazitakuwepo tena, bar unazokwenda kulewea hazitakuwepo tena, madili haramu na rushwa unazokula sasa hazitakuwepo tena…viwanda vinavyotengeneza mavazi yako ya kikahaba havitakuwepo tena, hakutakuwa na kurudi nyumbani kulala kutandani, wala kuangalia tv, wala kuingia internet..siku hizo zitahitimisha mambo hayo yote..Na baada ya hayo ziwa la moto litafunguliwa shetani na malaika zake watatupwa kwanza kwa maana lilitengenezwa kwaajili yao.

Kisha wote walio nje ya Kristo watafuata. Walio nje ya Kristo sio wale unaowategemea kwamba ni watu wa dini fulani..bali hata wewe uliye vuguvugu umbaye mguu mmoja upo nje mwingine ndani…ambaye ni mlevi lakini bado una jina la kikristo, ni mwasherani na mtembeaji uchi barabarani lakini bado unasali..wewe ndio mfano wa watakaoachwa wakati huo, na hiyo ni kulingana na maandiko na si mapokeo au mafundisho ya mtu binafsi aliyejiamulia tu kuzungumza.

Siku ya kunyakuliwa leo imekaribia sana kuliko jana na juzi…mwaka huu tumeukaribia unyakuo sana kuliko miaka ya nyuma..Hivyo huu ndio wakati wa kuongeza umakini wetu kuliko vipindi vya nyuma.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

MKARIBIE BWANA ZAIDI ILI UFANYIKE NGUZO.

NIMEOKOKA, ILA MUNGU NDIYE ANAYEJUA NITAKWENDA WAPI.

Chapa zake Yesu ni zipi hizo?

MUNGU WETU, JINSI LILIVYO TUKUFU JINA LAKO DUNIANI MWOTE!

KUTAKUWA NA MATETEMEKO YA NCHI, NJAA NA TAUNI.

KWANINI YESU KRISTO NI WA MUHIMU KWETU SASA?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments