Mtande ni nini? Ni funzo gani lipo nyuma yake?

Mtande ni nini? Ni funzo gani lipo nyuma yake?

Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi.

Waamuzi 16:13 Delila akamwambia Samsoni, Hata sasa umenidhihaki, umeniambia maneno ya uongo; niambie sasa, waweza kufungwa kwa kitu gani? Akamwambia, Ukivifuma hivi vishungi saba vya nywele za kichwa changu katika mtande wa nguo. 

14 Basi akazifunga kwa msumari, akamwambia Samsoni, Wafilisti wanakujia. Naye akaamka usingizini, akaung’oa ule msumari, na ule mtande. 

15 Mwanamke akamwambia, Wawezaje kusema, Nakupenda; na moyo wako haupo pamoja nami? Umenidhihaki mara hizi tatu, wala hukuniambia asili ya nguvu zako nyingi.

Mtande ni kifaa maalumu kinachotumika kufumia nyuzi za nguo, kwa kuzisokota pamoja ili kuunda nguo. Tazama mfano wa picha.

Hivyo nyuzi za nguo zilipitishwa katikati ya kamba hizo ngumu za mtande, kisha kuvutwa na kukazwa na mfumaji.

Katika habari hiyo tunaona Delila kazi yake huwenda ilikuwa ni ya ufumaji. Kwasababu ya uwepo wa kifaa hicho katika nyumba yake. Lakini katika harakati zake za kutaka kujua asili ya nguvu za Samsoni, biblia inatuambia, Samsoni alimdanganya kwa kumwambia ikiwa atavifuma vishungi vyake saba vya nywele katika mtande ule, basi, hatakuwa na nguvu za kujinasua, mahali pale.

Delila kusikia vile akaamini ni kweli, kwasababu kwa kawaida mtu ukishikwa tu nywele zako, si rahisi kuleta vurugu kwasababu utakuwa unajiumiza mwenyewe. Delila akizingatia kuwa alijua pia namna ya kufuma nyuzi vizuri. Hivyo alijihakikishia kuwa hilo linawezekana. Na cha kuongezea akapigilia na msumari kabisa, ili atakapojaribu kuzivuta nyewe zake, kutoka pale ashindwe. Kisha wafilisti waje kumchukua.

Lakini bado tunaona hilo halikuwezekana. Samsoni aling’oa misumari ile na kuuvunja mtande ule, Delila alipomwamsha.

Ni nini Tunajifunza katika habari hiyo kama waaminio?

KATIKA USINGIZI MUNGU ANAUMBA, NA SHETANI NAYE ANANASA.

Jiulize kwanini majaribio hayo yote Delila aliyafanya wakati ambao Samsoni amelala?. Alijua kabisa wakati akiwa macho Samsoni hawezi kukubali. Lakini pia swali lingine watu wanalojiuliza, iweje Samsoni, asisikie lolote wakati anatendewa vitendo vile. Kwamfano mpaka Delila anachukua nywele zake na kuziingiza kwenye mtande na kuzibana na kuzipigia misumari, asisikie chochote, ni usingizi wa namna gani?

Ndugu Mitego ya shetani, si rahisi kuigundua, kwasababu anaoutashi wa kuiweka kiasi cha kukufanya wewe usiwe mwepesi kuitambua, au kuisikia. Utashutukia tu umeshanaswa. Hivyo kama mwaminio ni kukimbia usingizi wowote wa kiroho kwa hali zote. Kwa kumtazama na kumfuata Yesu wakati wote. Unapomtazama Yesu, na kumtii kwa kuyakimbia machafu ya dunia. Hapo hujalala kiroho.

Lakini Pia katika usingizi Mungu pia hufanya jambo, na hilo si lingine zaidi ya kuumba. Utalithibitisha hilo kipindi kile alipomuumba Adamu, Mungu anasema.

Mwanzo 2:21 Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake, 

22 na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu. 

23 Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.

Umeona? Ukitulia kwa Bwana, akapumzika kwa Bwana, ukalala kwake. Jiandae kuumbiwa jambo lako bora kuliko yote katika maisha yako. Kama vile Mungu alivyomuumbia Adamu, msaidizi bora kuliko wote.

Kulala kwa Bwana ni kumpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yako, akupe ondoleo la dhambi. Kisha kuamua kuacha mambo yote ya kidunia na kumfuata yeye kwa uaminifu kwa kulitii Neno lake baada ya hapo. Na hapo ndipo unakuwa umelala kwake.

Hivyo chagua leo “Kuumbwa” badala ya “Kunaswa”. Mpokee Yesu sasa, ikiwa upo tayari kufanya hivyo. Basi fungua hapa kwa mwongozo huo wa sala ya Toba. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

KITENDAWILI CHA SAMSONI

JE! NYWELE ZAKO ZINAOTA AU ZIMESIMAMA?

Je Bwana Yesu alikuwa na nywele ndefu?

Rubani ni nani katika biblia? (Ezekieli 27:8)

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments