KUUMBWA TU, HAITOSHI YAPO MAMBO MENGINE MAWILI

KUUMBWA TU, HAITOSHI YAPO MAMBO MENGINE MAWILI

Nakusalimu katika jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo. Karibu tujifunze maneno ya Mungu ya uzima.

Kama kichwa cha somo kinavyosema. “Kuumbwa tu haitoshi”. Ikiwa na maana yapo mengine yanapaswa yafanyike ili uumbaji huo ukamilike.

Ukisoma kitabu cha Mwanzo mstari wa kwanza kabisa wa kitabu kile unasema.

Mwanzo 1:1Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. 

Lakini cha ajabu ni kuwa uumbaji ule haukuukamlisha ulimwengu wetu, ndio maana ukisoma vifungu vinavyofuata anasema..

Mwanzo 1:2a “ Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji;…”

Dunia Ilikuwa ni Utupu, na ukiwa.  Na yenye giza, kitu cha kutisha. Ndio hapo Mungu anachukua hatua nyingine kuu MBILI (2), ili kuikamilisha. Ya kwanza ni “ROHO WA MUNGU” kutua juu yake, na ya pili kutamka “NENO” lake.

Baada ya hapo ulimwengu ukaanza kuumbika vizuri, na kuwa makao ya mwanadamu, pamoja na kila kiumbe kilichohai kilichoumbwa na mwenyezi Mungu, kama alivyokusudia yeye.

Mwanzo 1:2b…Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.  3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.  4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza

Kwamba kiumbe chochote kilichoumbwa, Kikikosa Roho wa Mungu, na Neno la Mungu. Kiumbe hicho ni Ukiwa na utupu haijalishi kitakuwa hodari, kikubwa, kina utashi  kiasi gani.

Ni kufunua nini?

Mimi na wewe tumeumbwa na Mungu tukaitwa wanadamu, ni vizuri. Lakini hiyo haitoshi. Bado hatujakamilika kama Neno La Mungu halijafunuliwa ndani yetu. Na Neno hilo si mwingine zaidi ya YESU. Yeye ndio ile sauti ya Mungu tangu pale mwanzo, iliyosema na iwe NURU. Ambayo baadaye ikaja  kufanyika mwili, likakaa na sisi;

Yohana 1:1  “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.

2  Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.

3  Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.

4  Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, NAO ULE UZIMA ULIKUWA NURU YA WATU. 5  NAYO NURU YANG’AA GIZANI, WALA GIZA HALIKUIWEZA”

Maana yake ni kuwa kama huna KRISTO YESU maishani mwako. Wewe ni bure.

Vilevile na Roho wake MTAKATIFU kuwa juu yako.

Warumi 8:9  Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote ASIPOKUWA NA ROHO WA KRISTO, HUYO SI WAKE.

Ndio maana kwanini upo umuhimu wa mtu kuzaliwa mara ya pili. Kwa kumpokea Kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yake, ili apate msamaha wa dhambi. Lakini pia kupokea Roho wake Mtakatifu.

Ukikamilisha hayo mawili wewe hapo unakuwa mtu KAMILI na HALISI, aliyeumbwa na Mungu. Unayeweza kumzalia Mungu matunda yote anayotaka.

Okoka ndugu, Fahamu kuwa hakuna maisha nje ya Kristo,  hizi ni siku za mwisho. Kristo anakaribia kurudi, ulimwengu upo ukingoni. Umejiandaaje na karamu ya mwanakondoo mbinguni? Ukamilifu wako upo wapi?

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

NJIA YA WOKOVU NDANI YA KITABU CHA WARUMI.

Nitajuaje kuwa nimesamehewa dhambi zangu?

AGIZO LA TOBA LINAENDANA NA UBATIZO!.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments