JIBU: Picha nyingi zinazochorwa kumweleza Yesu, takribani nyingi ya hizo zinamwonyesha ni mtu mwenye nywele ndefu. Lakini Je uhalisia wake ni upi, ni kweli alikuwa na nywele ndefu au fupi?
Maandiko yanaeleza utamaduni wa wayahudi, kwa wanaume ilikuwa kuacha nywele zirefuke kama zile za mwanamke ni aibu kwa mtu huyo. Anajivunjia heshima kubwa.
1Wakorintho 11:14 “Je! Hayo maumbile yenyewe hayawafundishi ya kwamba mwanamume akiwa na nywele ndefu ni aibu kwake? 15 Lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni fahari kwake. Kwa sababu amepewa zile nywele ndefu ili ziwe badala ya mavazi”
Hivyo hakukuwa na mtu aliyekuwa na nywele ndefu isipokuwa tu mtu aliyeitwa mnadhiri wa Mungu.
Lakini Je! Yesu alikuwa ni Mnadhiri ?
Kabla ya kufahamu kama Yesu alikuwa mnadhiri au la! Tufahamu kwanza mnadhiri alikuwa ni nani, na sheria ya mnadhiri ilikuwaje
Mnadhiri ni mtu aliyetengwa au aliyejitenga mwenyewe/ aliyejitoa wakfu kwa Mungu, kufuata na sababu binafsi, aidha kwa sababu ya shukrani yake ya kutendewa jambo Fulani kama vile kuponywa ugonjwa, au kupatiwa mtoto, au kupata kitu Fulani kwa Mungu alichokuwa anamwomba. Hivyo katika agano la kale, kulikuwa na sheria ya mnadhiri. Na mnadhiri alikuwa yoyote Yule aidha mwanamke au mwanaume.
Kulingana na Hesabu 6:1-8
Matendo 18:18 “Baada ya hayo Paulo akazidi kukaa huko siku nyingi, kisha akaagana na ndugu akaabiri kwenda Shamu; na Prisila na Akila wakaenda pamoja naye, alipokwisha kunyoa kichwa chake huko Kenkrea; maana alikuwa ana nadhiri”
Sasa tukirudi kwa Bwana Yesu.
Je! Na Yeye alikuwa ni mnadhiri?
Jibu ni hapana, kwasababu Bwana alikunywa mzao wa mzabibu.
Mathayo 26:29 Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.
Kuonyesha kuwa hapo kabla alikuwa anakunywa.
Soma pia Mathayo 11:19, Na Yohana 2:1-12, inatupa picha alitumia mzao wa mzabibu. Halikadhalika aligusa maiti, (Marko 5:41), na zaidi ya yote Bwana hakufungwa na sheria za torati.
Hivyo kwa kifupisho ni kwamba Bwana Yesu hakuwa na nywele ndefu, yawezekana alikuwa na nywele nyingi lakini hazikuwa ndefu kama za mwanamke, mfano wa aonekanavyo kwenye baadhi ya picha zinazochorwa.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
JE! NYWELE ZAKO ZINAOTA AU ZIMESIMAMA?
WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.
Je! sheria ilikuwaje dhaifu kwasababu ya mwili? (Warumi 8:3)
NGUVU YA MNADHIRI WA BWANA.
MAUTI NA KUZIMU ZIKAWATOA WAFU WALIOKUWAMO NDANI YAKE.
Nini maana ya Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza (Yakobo 4:9)
Fahamu maana ya Mithali 29:4 “Mfalme huithibitisha nchi kwa hukumu; Bali yeye apokeaye rushwa huipindua.
Rudi nyumbani
Print this post