Je Yuda alienda wapi, ni mbinguni au jehanamu?

Je Yuda alienda wapi, ni mbinguni au jehanamu?

Hili ni moja ya maswali yanayoleta mkanganyiko miongoni mwa wakristo wengi? Baadhi wanaamini kile kitendo tu cha yeye kujutia makosa yake mpaka kupelekea kutoona faida ya kuishi hadi kwenda kujinyonga ni toba tosha, baadhi wanaamini tayari alikuwa ni mtume aliyechakuliwa na Yesu, hivyo hata iweje hawezi kwenda kuzimu, kwasababu Mungu hachagui vilivyo dhaifu. Lakini baadhi bado wanashikilia kuwa alikwenda kuzimu, kwasababu alikuwa mwizi na mwisho wa kifo chake ilikuwa ni kujinyonga. Na hiyo ni uthibitisho kuwa alipotea.

Lakini tuangalie maandiko yanatupa alama gani kuhusiana na hatma ya Yuda, ndipo tutakapoitimisha kwamba Yuda alikwenda wapi.

Bwana Yesu alisema maneno haya kwa Yuda;

Mathayo 26:24  Mwana wa Adamu aenda zake, kama alivyoandikiwa; lakini ole wake mtu yule ambaye amsaliti Mwana wa Adamu! Ingekuwa heri kwake mtu yule kama asingalizaliwa.

Pa kutilia umakini ni hilo Neno alilohitimisha nalo,  “Ingekuwa heri kwake mtu yule kama asingalizaliwa”.linatupa picha mbaya kwamba mtu huyo alikuwa  hana faida yoyote duniani, maisha yake ni kama bure.

Lakini pia, kuna maneno mengine ambayo Bwana Yesu aliyasema katika sala yake; Alisema..

Yohana 17:12  Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.

Kuonyesha kuwa Yuda alipotea.

Lakini andiko lingine, tunalisoma katika kitabu cha matendo ya mitume, wakati mitume wanapiga kura kuchagua mtume atakayesimama mahali pa Yuda. Nao pia walisema maneno haya;

Matendo 1:24  Kisha wakaomba, wakasema, Wewe, Bwana, ujuaye mioyo ya watu wote, tuonyeshe ni nani uliyemchagua katika hawa wawili, 25  ashike mahali katika huduma hii na utume huu, alioukosa Yuda, aende zake mahali pake mwenyewe. 26  Wakawapigia kura; kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja.

Utaona hapo anasema “aende zake mahali pake mwenyewe”. Ikimaanisha kuwa Yuda hakwenda mbinguni bali mahali pake, na huko si kwingine zaidi ya  kuzimu.

Hivyo kwa vifungu hivyo vyote, hatuoni mahali popote maandiko yanatupa viashiria kuwa Yuda alikwenda mahali pazuri, ukizingatia kuwa katika hatua zake za mwisho hadi kujinyonga, biblia inatuambia aliingiwa na “shetani”. Maana yake ni kuwa shetani alifanya kiti cha enzi ndani yake, hivyo maamuzi yote aliyokuwa anayafanya yalisukumwa na yule mwovu, sio Mungu. Kwahiyo hakuna kitendo cha ki-Mungu alichokifanya Yuda tangu wakati ule.

Hili ni fundisho kubwa sana, hususani kwa watumishi wa Mungu. Bwana kukuita haimaanishi kuwa huwezi potea. Au huwezi ingiliwa na shetani. Petro aliteleza mara kadhaa, na alivamiwa na shetani kinywani mwake, lakini hakukubali kumpa adui nafasi, vivyo hivyo na wewe, hupaswi kusema mimi nina kanisa kubwa, mimi ninahubiri, mimi nimetokewa na Yesu. Kumbuka Yuda aliishi na Yesu kwa zaidi ya miaka mitatu, sio kutokewa nusu saa, lakini alianguka, kwasababu aliipa dhambi nafasi katika maisha yake.

Nasi pia tunapaswa tusimame, dhambi isichukue nafasi yoyote mioyoni mwetu. Kwasababu hiyo inaanza kama tamaa, kisha inachukua mimba, kisha inazaa mauti. Kaa mbali na dhambi.

Bwana atusaidie..

Je! Umeokoka? Je unahabari kuwa hizi ni siku za mwisho, na Yesu yupo mlangoni kurudi?. Umejiandaaje, unaishije, unatazamia nini baada ya haya maisha? Ni heri utubu dhambi zako sasa, umrejee Bwana, usamehewe dhambi zako, Kumbuka adui anakuwinda sana, usiishi maisha kama ya wanyama, wewe ni wa thamani, mbele za Mungu wako.  ikiwa upo tayari kufanya hivyo, basi waweza fungua hapa kwa msaada wa mwongozo wa sala ya Toba >>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mada Nyinginezo:

Je ni kweli Yuda hakuwa na dhambi kwa kumsaliti Bwana, kwasababu tayari ilikuwa imeshatabiriwa?

JINSI BWANA ALIVYOWACHAGUA MITUME WAKE.

YUDA ISKARIOTE! MTUME ALIYECHAGULIWA NA BWANA YESU.

Kwanini Bwana Yesu alitokea katika ukoo wa Yuda?

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 1

Ni kwa namna gani Yesu ni Simba wa Yuda?

MAJARIBU MATANO (5) YA MKRISTO.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments