Hiyo yote ni kuonyesha ni jinsi gani Bwana asivyokuwa mbaguzi, aliwachagua watu mbalimbali aliwachagua matajiri, aliwachagua maskini, aliwachagua wenye elimu aliwachagua wasio na elimu, aliwachagua wanafki, aliwachagua wapigania dini.. wote hao, aliwaita sawa sawa wawe mitume wake..Hata na leo hii anaita watu wote, wewe ni fisadi anakuita,wewe ni mpenda fedha ambaye ilifikia hatua ukamtoa mama yako kafara au mtoto wako kwa waganga kwa ajili ya kupata mali, bado KRISTO anakuita leo, wewe ni muuza karanga anakuita, wewe ni mwanasiasa anakuita, wewe ni bilionea bado anakuita uwe mwanafunzi wake, wewe ni tapeli anakuita, wewe ni mlemavu anakuita. Vyovyote vile ulivyo anakuita. Kinachojalisha ni jinsi utakavyomaliza na sio jinsi ulivyosasa.