Kwanini kuwe na kitabu Cha kumbukumbu la Torati na kwanini kiitwe vile?

Kwanini kuwe na kitabu Cha kumbukumbu la Torati na kwanini kiitwe vile?

Kitabu hiki katika lugha ya kiebrania kinasomeka kama “Devarim” ambayo tafsiri yake ni “Maneno”

Na ndio maana mstari wa kwanza kabisa un itaanza Kwa kusema. “Haya ndiyo maneno”

Kumbukumbu la Torati 1:1

[1]Haya ndiyo maneno Musa aliyowaambia Israeli wote ng’ambo ya Yordani barani, katika Araba lililoelekea Sufu, kati ya Parani, na Tofeli, na Labani, na Hazerothi, na Dizahabu.

Lakini katika tafsiri ya kigiriki Cha kale (septuagint),  kilisomeka kama “deuteronomioni” chenye maana ya “Mrudio wa sheria” ambapo Kwa sisi kinasomeka kama “kumbukumbu la sheria/torati”. 

Ni kitabu Cha Tano ambacho kiliandikwa na Musa karibia na mwisho wa Ile miaka 40, wakati walipokuwa ng’ambo ya Yordani katika nchi ya Moabu.

Lengo la kuandikwa kitabu hicho ni kukumbushwa sheria na maagizo ya Mungu, kwasababu kundi kubwa la Wana wa Israeli lililopokea sheria Kule mlima Sinai mwanzoni, lilifia jangwani, hivyo kile kizazi kipya Hakikuwa na msingi imara juu ya sheria za Mungu. Na ndio hapa Musa anaagizwa na Mungu awakumbushe Wana wa Israeli sheria yake.

Kitabu hiki kimeanza kuwakumbushia safari Yao Toka Misri, pia kikagusia jukumu lao la kumpenda Mungu na kuzishika sheria zake. Ikafuatana na baraka na laana ambazo zitampata mtu katika kutii au kutokutii, na mwisho kifo cha Musa.

Je ni Nini tunajifunza kuwepo kwa kitabu hiki ? 

Bwana anataka na sisi tuweke kumbukumbu la agano lake mioyoni mwetu, Kwa vizazi vijavyo tupende kuwafundisha vizazi vinavyochipukia Neno la Mungu, tusiwaache tukadhani wataelewa tu wenyewe kisa biblia ipo, bila kukumbushwa Kwa kufundishwa.

Musa alifanya vile ndio maana kizazi kile kikawa imara baada ya pale.

Na sisi tuwe watu wenye tabia hii, Sio kwa watoto tu hata Kwa kondoo wa Bwana kanisani. Mara Kwa mara tuwakumbushe maagizo ya Mungu.

Kwa maelezo ya ziada kuhusu kitabu hichi pitia hapa >>> https://wingulamashahidi.org/2019/05/13/vitabu-vya-biblia-sehemu-ya-2/

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618. Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mada Nyinginezo:

Vitabu vya Deuterokanoni ni vya ki-Mungu?

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1

Mtiririko wa vitabu vya biblia kwanini upo vile?

Je! Mwendo wa Sabato ulikuwaje kibiblia?(Matendo 1:12)

NJIA YA WOKOVU NDANI YA KITABU CHA WARUMI.

Nini maana ya “Atamwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake”. (2Wathesalonike 2:8).

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments