Je! Mwendo wa Sabato ulikuwaje kibiblia?(Matendo 1:12)

Je! Mwendo wa Sabato ulikuwaje kibiblia?(Matendo 1:12)

Neno hili limetajwa mara moja katika biblia, kwenye kitabu cha;

Matendo 1:12 “Kisha wakarudi kwenda Yerusalemu kutoka mlima ulioitwa wa Mizeituni, ulio karibu na Yerusalemu, wapata mwendo wa sabato”.

Ni mwendo ambao ulitengwa maalumu wa mtu kusafiri siku ya sabato, ambao urefu wake ulikuwa ni dhiraa elfu mbili (2000), ambao ni sawa na Kilometa moja kwa makadirio.

Kutoka mlima wa mizetuni mpaka mjini Yerusalemu, ni umbali uliokuwa  ndani ya hiyo kilometa moja, ndio huo walisafiri mitume wa Bwana siku hiyo.

Lakini Je! Agizo hilo tunalipata wapi katika agano la kale?

Hakuna andiko la moja kwa moja katika torati ya Musa linaloeleza kuwa mwendo wa sabato, ulipaswa uwe ndani ya hizo dhiraa elfu mbili. Bali Marabi wa kiyahudi baadaye walidhani hivyo kulingana na uhalisia wa maandiko haya.

Kutoka 16:29 “Angalieni, kwa kuwa Bwana amewapa ninyi hiyo Sabato, kwa sababu hii huwapa siku ya sita chakula cha siku mbili; kaeni kila mtu mahali pake, mtu awaye yote asiondoke mahali pake kwa siku ya saba

Kwamba anaposema Usiondoke mahali pako, anamaanisha ndani ya mipaka ya mji wako, hii ikiwa na maana ukiwa ndani ya mipaka uliruhusiwa kutembea, utakavyo. Na kama ikitokea unatoka, basi hupaswi kusafiri Zaidi ya hizo dhiraa elfu 2000.

Na hiyo waliirithi kufuatana na sheria ya malisho ya nje ya mji ambayo walipewa walawi katika..

Hesabu 35:4 “Na yale malisho ya miji mtakayowapa Walawi, ukubwa wake utakuwa tangu ukuta wa mji kupima kiasi cha dhiraa elfu pande zote.  5 Nanyi mtapima hapo nje ya mji upande wa mashariki dhiraa elfu mbili, na upande wa kusini dhiraa elfu mbili, na upande wa magharibi dhiraa elfu mbili, na upande wa kaskazini dhiraa elfu mbili, huo mji ulio katikati. Hayo ndiyo yatakayokuwa kwao malisho ya miji”.

Hivyo kwa kurejea sheria hizo, wakahitimisha kuwa mwendo wa mtu kusafiri nje ya mji siku ya sabato ni hizo dhiraa elfu mbili(2000) au kilometa moja . Ndio Wakauita mwendo wa Sabato. Lakini hakukuwa na sheria ya moja kwa moja inayoeleza mwendo huo ulipaswa uwe katika vipimo hivyo.

Lengo la kufanya vile ni kuwafanya watu wasitawanyike mbali na eneo la kuabudia, ndani ya mji, siku hiyo ya Bwana.

Hata sasa. Ni lazima Kila mmoja wetu awe na mwendo wake wa sabato katika siku ya Bwana..kumbuka jumapili ni siku ya Bwana, hupaswi kwenda mbali na uwepo wa Mungu, siku hiyo sio siku ya kufanya biashara, sio siku ya kwenda kwenye mihangaiko isiyokuwa na lazima, Bali ni siku maalumu Kwa ajili ya ibada..penda kuwepo kanisani, mikutanoni, kwenye semina, kwenye mafundisho redioni,mitandaoni, kwenye vitabu vy ona kiroho.n.k.

Shalom

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

MWENDO UNAOSHANGAZA SANA!

IMESALIA RAHA YA SABATO KWA WATU WA MUNGU.

Je ni kweli ilikuwa desturi ya Bwana kuishika sabato?(Luka 4:16)

Sabato halisi ni lini, Je! ni Jumapili au Jumamosi?, Ni siku gani itupasayo kuabudu?

EPUKA KUCHELEWA IBADA.

Nini maana ya ombeni kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi wala siku ya sabato?

NI NINI KITAKACHOTUFANYA TUPIGE MBIO BILA KUPUNGUZA MWENDO?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
11 months ago

Jumapiri.ni.siku.ya.bwana.imeandikwa.wapi?