EPUKA KUCHELEWA IBADA.

EPUKA KUCHELEWA IBADA.

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA MAENEO YA IBADA: Sehemu ya 2


EPUKA KUCHELEWA IBADA.

Jambo la kuchelewa ibada sio tu linamvunjia Mungu heshima yake, lakini pia linaweza kukupelekea mauti. Utajiuliza hili linawezekanikaje. Embu tufuatilie kisa hiki cha Anania na mkewe Safira, kisha tuone ni jambo lipo nyuma yake.

Matendo ya Mitume 5:1  “Lakini mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza mali,

2  akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume.

3  Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja?

4  Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu.

5  Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya.

6  Vijana wakaondoka, wakamtia katika sanda, wakamchukua nje, wakamzika.

7  Hata MUDA WA SAA TATU BAADAYE MKEWE AKAINGIA, naye hana habari ya hayo yaliyotokea.

8  Petro akamjibu, Niambie, Mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo? Akasema, Ndiyo, kwa thamani hiyo.

9  Petro akamwambia, Imekuwaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe.

10  Mara akaanguka miguuni pake akafa; wale vijana wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mumewe.

11  Hofu nyingi ikawapata kanisa lote na watu wote walioyasikia haya”.

Katika habari hiyo tunaona mke wa Safira hakuwepo ibadani wakati ibada inaanza, alikuja kutokea SAA TATU baadaye. Hii ikiwa na maana kwamba kama ibada inaanza saa tatu kamili asubuhi yeye alifika saa sita mchana.. Na matokeo yake hakuelewa chochote kilichotokea kwamba tayari mume wake alishakufa saa nyingi na kuzikwa.

Tengeneza picha angekuwepo pale muda ule ule, ingekuwa rahisi yeye kutubu, alipomuona mume wake ameanguka na kufa, lakini hakuwepo, alidhani kama ilivyokuwa jana, ndivyo ilivyo na leo. Hata sasa wapo watu ambao Mungu anawaua kiroho, kwa kuiendekeza tabia hii. Hawapo kwenye vipengele vingi vya maombi, hawajua kuwa wakati mwingine Mungu anaachilia rehema, mwanzoni kabisa mwa ibada, lakini wao wanakosa halafu wanakuja baadaye kushiriki na wale wengine bila kutakaswa dhambi zao, mwisho wa siku wanapigwa na Mungu.

Ndugu zipo Baraka mtu anazozipata kila mwanzo na kila mwisho wa ibada, nilisiliza ushuhuda wa mpendwa mmoja, anasema alionyeshwa kuna malaika maalumu wanaogizwa na Bwana wasimame, kila mwanzo na kila mwisho wa ibada, kazi yao mahususi ni kutoa Baraka.

Hivyo mtu anapochelewa ibadani tayari ameshapoteza Baraka zake, na vilevile mtu anayeondoka kabla ya ibada kuisha jambo ni lile ile. Na ndivyo ilivyo wewe sio mgeni rasmi kwa Mungu..Mungu ndiye anayepaswa awe mgeni rasmi kwako, anatukuta tayari tupo ibadani tunamsubiria yeye. Mungu ni zaidi ya raisi, ni zaidi ya mfalme yeyote. Kama unakuwa mwaminifu na ratiba ya kazini kwako, ambayo inakupasa kila siku uwahi kuamka ufike, kwanini usiwahi ibadani, unachelewa bila sababu yoyote ya msingi?

Unapokosa, kipengele kimoja wapo, ni sawa na umekosa ibada nzima, hata 1000, haiwezi kuitwa elfu moja kama haijakamilika.. haijalishi utakuwa na kiwango cha  999.99 kinachoikaribia.. Kama senti moja itakosekana bado itaitwa tu mia tisa, na sio elfu moja.

Na ndivyo ilivyo ibada yoyote ya Mungu, kama, utakosa kile kipengele cha kwanza cha kufungua ibada, usidhani kuwa siku hiyo ulifanya ibada yoyote. Mungu anaona umepunguka. Anasema yeye ni alfa na omega, mwanzo na mwisho. Maana yake ni kuwa ili akamilike kwako ni lazima mwanzo wako uwe naye pia na mwisho wako.

Jijengee desturi nusu saa kabla ya ibada yoyote kuanza uwe umeshafika maeneo ya uweponi mwa Bwana. Kwa kufanya hivyo kamwe hutakaa uchelewe. Na utapokea Baraka nyingi badala ya laana.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

KATAA KUWA EUTIKO, WA KUSINZIA IBADANI.

Nini maana ya kumwabudu Mungu katika Roho na kweli?

Nini maana ya “saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada?”

Ni muda gani Bwana Yesu alisulibiwa. Je! Ni saa 3 au saa 6?

Kwanini Mungu aseme “Alaaniwe azuiaye upanga wake usimwage damu” (Yeremia 48:10).

Je! Mtu ambaye hajaoa anaruhusiwa kulichunga kundi?

ALAMA ZA BENDERA YA ISRAELI ZINAWAKILISHA NINI?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments