Nini maana ya kumwabudu Mungu katika Roho na kweli?

Nini maana ya kumwabudu Mungu katika Roho na kweli?

JIBU: Kwanza ni muhimu kufahamu nini maana ya neno “kuabudu”. Leo hii ukizungumzia neno kuabudu, haraka haraka katika vichwa vya wengi, italenga katika “kuimba nyimbo za kuabudu”. Lakini kiuhalisia kumuabudu Mungu sio kuimba nyimbo za kuabudu. Bali neno “kuabudu”, limetokana na neno “Ibada”. Kwahiyo “kufanya ibada” ndio “kuabudu”. Kwa urefu juu ya kuabudu unaweza kufungua hapa >> Kuabudu ni nini?

Mtu anayefanya ibada za mashetani, hapo anaabudu mashetani, kadhalika mtu anayefanya ibada kwa Mungu wa mbingu na nchi, hapo anamwabudu Mungu wa mbingu na nchi. Hizo nyimbo zinazokuja za kumsifu Mungu na kumwimbia wakati wa ibada, ndio zinazoitwa Nyimbo za kuabudu.

Kwamsingi huo basi, Neno la Mungu linasema katika..

Yohana 4:23  “Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika ROHO NA KWELI. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.

24  Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”

Maana yake ni kwamba, saa inakuja ambayo watu watakaomfanyia Mungu ibada, na ibada hiyo wataifanya katika roho na kweli.

Sasa nini maana ya… “katika roho na kweli” ?

Tusome.

Yohana 16:12 “ Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa.

13  Lakini yeye atakapokuja, HUYO ROHO WA KWELI, atawaongoza AWATIE KWENYE KWELI YOTE; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake”

Hapo anasema Roho Mtakatifu atakapokuja atatuongoza atutie katika kweli yote. Hivyo tukishampokea Roho Mtakatifu ndani yetu, na huyo Roho akatuongoza na kututia kweli kweli yote, na baada ya kuipata hiyo kweli, tukaenda tukafanya ibada katika hiyo kweli, tuliyoipata kutoka kwa Roho Mtakifu aliye ndani yetu, basi hapo tutakuwa tumemwabudu Mungu katika “Roho na kweli”.

Kwahiyo kumwambudu Baba katika Roho na Kweli ni kufanya ibadaa huku tukiwa tumempokea Roho Mtakatifu na kweli ipo ndani yatu.

Sasa kweli ni nini?

Biblia imetupa jibu katika kitabu cha Yohana..

Yohana 17:16 “Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.

17 Uwatakase kwa ile kweli; NENO LAKO NDIYO KWELI.”

Umeona hapo?. Neno la Mungu ndio “kweli”. Kwahiyo kumwabudu Baba katika roho na kweli, ni “kumfanyia Mungu ibada katika Roho Mtakatifu na katika Neno lake”.

Je wewe leo unamwabudu Mungu katika Roho na Kweli?. Fahamu huwezi kuijua kweli kama hauna Roho Mtakatifu ndani yako, na biblia inasema wote wasio na Roho Mtakatifu hao sio wake (Warumi 8:9).

Hivyo ni lazima kumpokea Roho Mtakatifu kwanza ndipo, aweze kukuongoza katika kweli yote. Si ajabu leo watu hawawezi kulielewa Neno kwasababu Hawana Roho ndani yao, ndio maana utaona mtu anakwenda kumfanyia Mungu ibada kanisani, huku yupo nusu tupu, kava kimini, au suruali, au kavaa hereni, au kanyoa kama jogoo na wala hasikii kuhukumiwa ndani yake. Ni kwanini?. Ni kwasababu hana Roho Mtakatifu ndani yake ambaye angeugua ndani yake kumshuhudia hicho anachofanya sio sahihi, na kumwongoza katika Kweli yote.

Hivyo Roho Mtakatifu ni muhimu na ni ahadi kwa kila mwamini aliyempokea Yesu (Matendo 2:38), Na kumpokea Roho Mtakatifu sio kunena kwa lugha!.. Lugha sio ishara pekee ya Mtu aliyempokea Roho Mtakatifu,  Mtu anaweza asinene kwa lugha na bado akawa amempokea Roho Mtakatifu, na pia mtu anaweza kunena kwa lugha na asiwe na Roho Mtakatifu bali ni roho nyingine. (Kama utahitaji kufahamu zaidi juu ya Roho Mtakatifu na uthibitisho wake basi unaweza kutujuza inbox, au kwa namba hizi 0789001312/0693036618).

Kumbuka hizi ni siku za mwisho, Kristo yupo mlangoni anabisha mioyoni mwa wengi, wakati wowote parapanda ya mwisho italia, na wafu watafufuka, wale waliokufa katika Bwana, wataungana na wale walio hai, walio na Roho Mtakatifu, na kwa pamoja watakwenda mawinguni katika karamu ya mwanakondoo..

Je utakuwa wapi siku hiyo?

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Nini maana ya kuabudu?

JE! NI LAZIMA WATU WOTE WANENE KWA LUGHA?

ZIFAHAMU KAZI TATU ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA ULIMWENGU.

JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?

UTENDAJI KAZI MWINGINE WA ROHO MTAKATIFU USIOUFAHAMU.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Lindah
Lindah
1 year ago

Salamu za Bwana wetu Yesu krsito ziwafikie. Nimeupitia huu ujumbe na nimesaidika pakubwa sana..bila shaka naenda Kuushiriki na wengine. Mbarikiwe sana mnapoaendelea na hii Huduma ya baraka na Nina Nia ya kufahamu na kuelimika zaidi kupitia kwenye jumbe zenu. Bwana wa Amani awazidishie neema.