Naivera ni nini? Kwanini Daudi aliihitaji alipomtafuta Mungu?

Naivera ni nini? Kwanini Daudi aliihitaji alipomtafuta Mungu?

Kibiblia Naivera imemaanisha vitu viwili, cha kwanza, ni aina ya vazi maalumu  lililotengenezwa  kwa mfano wa Aproni(yale mavazi ya wapishi) kwa ajili ya ibada za kikuhani, au kwa ajili ya kujisogeza mbele za Mungu.

Kwamfano, Mungu alimuagiza Musa, atengeneza mavazi ya kikuhani, kwa ajili ya Haruni, na watoto wake, na mojawapo ya vazi hilo ilikuwa ni hiyo Naivera, Unaweza kutazama picha juu

Kutoka 28:4 “Na mavazi watakayoyafanya ni haya; kifuko cha kifuani, na naivera, na joho, na kanzu ya kazi ya urembo; na kilemba, na mshipi; nao watawafanyia Haruni nduguyo, na wanawe, mavazi matakatifu ili anitumikie katika kazi ya ukuhani”.

Ukisoma pia Kutoka 28:6-14, utaona inatoa maelezo hayo kwa urefu jinsi vazi hilo linavyopaswa kuundwa.

Nabii  Samweli pia aliivaa Naivera, alipokuwa akitumika hemani pa Bwana.

1Samweli 2:18 “Lakini Samweli alikuwa akitumika mbele za Bwana, naye alikuwa kijana, mwenye kuvaa naivera ya kitani”.

Lakini utaona pia baadaye Naivera, ilikuja kuvaliwa na watu ambao hawakuwa makuhani, kama vile  Daudi, sehemu mowajawapo ni wakati ule analitoa sanduku la agano kutoka katika nyumba ya Obed-edomu, mpaka mjini pake, siku ambayo alimchezea Mungu, mpaka nguo zikamtoka, alikuwa amevaa Naivera.

2Samweli 6:13 “Hata ikawa, watu waliolichukua sanduku la Bwana walipokwisha kwenda hatua sita, akachinja ng’ombe na kinono.

14 Daudi akacheza mbele za Bwana kwa nguvu zake zote; na Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani.

15 Basi Daudi na nyumba yote ya Israeli wakalileta sanduku la Bwana kwa shangwe, na kwa sauti ya tarumbeta”.

Jambo hilo hilo utalisoma pia katika 1Nyakati 15:26-28

“26 hata ikawa, Mungu alipowajalia Walawi waliolichukua sanduku la agano la Bwana, wakachinja ng’ombe saba, na kondoo waume saba.

27 Naye Daudi alikuwa amevaa joho ya kitani safi, na Walawi wote waliolichukua sanduku, na waimbaji, na Kenania msimamizi wa uchukuzi, na waimbaji; naye Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani.

28 Ndivyo Israeli wote walivyolipandisha sanduku la agano la Bwana kwa shangwe na kwa sauti ya tarumbeta, na kwa baragumu, na kwa matoazi, wakipiga sauti kuu kwa vinanda na vinubi.

Na si hapo tu utaona wakati mwingine, Daudi alipokuwa akikimbizwa na adui yake Sauli, alipofika kwa yule kuhani aliyeitwa Abiathari aliichukua ile Naivera iliyokuwa mkononi mwake akaivaa ndipo akamuuliza Mungu juu ya hatma yake,

Soma 1Samweli 23:6-12, utaipata habari hiyo.

 Pia wakati mwingine ni pale alipokuwa anawafukizia maadui zake waliochukua mateka vitu vyao na wake zao utaona Daudi alifanya jambo hilo hilo kumuuliza Mungu, kwa njia hiyo hiyo ya kuivaa Naivera. (Soma 1Samweli 20:7-8)

Hivyo Naivera lilikuwa ni vazi  maalumu lililotumika kwa ajili ya kumkaribia Mungu, au kuuliza kwa Mungu.

Pili Naivera, katika biblia  inatajawa kama vitu cha kuabudiwa, mfano wa  kinyago Fulani,.

Katika maandiko utaona kuna wakati  Gideoni, aliwaagiza wana wa Israeli watoe vitu vyao vya thamani, ili kuiunda, jambo ambalo lilikuwa kikwazo kwake na kwa Israeli nzima.

Waamuzi 8:25 “Wakajibu, Tutakupa kwa mioyo. Basi wakatandika nguo chini, wakatia humo kila mtu pete za masikio ya mateka yake.

26 Na uzani wa hizo pete za dhahabu alizozitaka ulipata shekeli za dhahabu elfu moja na mia saba; mbali na makoja na vidani, na mavazi ya rangi ya zambarau waliyokuwa wameyavaa hao wafalme wa Midiani, tena mbali na mikufu iliyokuwa katika shingo za ngamia zao.

27 BASI GIDEONI AKAFANYA NAIVERA KWA VITU VILE, AKAIWEKA KATIKA MJI WAKE, mji huo wa Ofra; nao Israeli wote wakaenda na kuiandama kwa ukahaba huko; nayo ilikuwa ni tanzi kwa Gideoni na kwa nyumba yake”.

Je! Na sisi leo hii tunapaswa tuvae Naivera  kila tunapomkaribia Mungu, kama walivyofanya watu wa agano la kale?.

Jibu ni hapana, Naivera yetu kwasasa ni Kristo tu, ukiwa na Kristo moyoni mwako, tayari ni vazi tosha la kukusogeza mbele za Mungu kuliko vazi lingine lolote unaloweza kulivaa katika mwili. Lakini Kristo hawezi kuwa vazi lako, ikiwa hujatubu kwa kumaanisha kabisa  kuacha dhambi zako na kubatizwa, na kuishi Maisha ya utakatifu yanayompendeza hapa duniani.

Hivyo tubu dhambi zako mgeukie Bwana Yesu naye atakuokoa,  kumbuka yeye mwenyewe alisema maneno haya;

Ufunuo 16:15 “(Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Nini maana ya Dirii, Chepeo na Utayari?

URIMU NA THUMIMU NI NINI KATIKA BIBLIA?

Nguo za magunia katika biblia ni zipi?

Je! Daudi hakuwa mtoto wa ndoa wa Yese? (Zab 51:5)

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 10 (Kitabu cha Zaburi).

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
8 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Mantiz
Mantiz
1 year ago

Umetisha

Mangala Tambatamba Augustin
Mangala Tambatamba Augustin
1 year ago
Reply to  Mantiz

Nampenda Yesu kristu katika maisha yangu

ELIZABETH
ELIZABETH
2 years ago

MUNGU akubariki sana Mtumishi Sasa nimeelewa maana ya naivera

Cathy
Cathy
2 years ago

Asante kwa ufafanuzi mzuri wa vazi la naivera na matumizi yake kikuhani. Ni kweli, kwa sasa wote tuliookoka ni makuhani mbele za Mungu na vazi letu ni Yesu Kristo mwenyewe. Jina lake na dami yake vyatosha kutusogezesha mbele ya BWANA.
Mbarikiwe sana kwa masomo mazuri.

Luja
Luja
1 year ago
Reply to  Admin

Ubarikiwe sana, sasa nimeelewa maana ya naivera. Asante sana kwa ufafanuzi mzuri