Nini maana ya Dirii, Chapeo na Utayari?

Nini maana ya Dirii, Chapeo na Utayari?

Chapeo:

Chapeo ni kofia ngumu ya chuma waliyokuwa wanavaa watu waliokuwa wanakwenda vitani. Tazama picha chini.

chepeo ni nini

Kwa lugha ya kiingereza ni “Helmet” . Kwa nyakati hizi, shughuli nyingi na michezo mingi jamii ya kofia hizo zinatumika, kwamfano wanaondesha pikipiki ni lazima wavae helmet (yaani chepeo), kwa usalama wa safari yao hiyo, kwasababu kwa bahati mbaya ikitokea wakipata ajali, sehemu ya kichwa haitadhurika kutokana na kofia hiyo ngumu waliyoivaa. Kadhalika na sehemu nyingine nyingi, chepeo zinatumika. Na pia chepeo za askari wa zama hizi, sio sawa na za askari wa zamani, hizi za nyakati zetu zimetengenezwa kwa kwa utashi zaidi mara nyingi ya zile, ambapo hata askari akipitia mahali penye hewa ya sumu si rahisi kudhurika.

askari wa sasa

Na sisi wakristo katika roho ni maaskari wa Kristo, nasi pia hatuna budi kuzivaa chepeo vichwani mwetu, hiyo itatusaidia chochote kile kitakachorushwa na adui shetani katika roho, dhidi yetu, visiweze kuvidhuru vichwa vya roho zetu, na hata pia tukianguka kwa bahati mbaya katika vita hivi vya imani, tusiweze kudhurika, maana yake tusife moja kwa moja, bali tuweze kusimama tena, kwasababu vichwa vyetu vimehifadhiwa. Na pia vita vyetu sisi ni vikali zaidi ya watu wa vizazi vya nyuma hivyo hatuna budi, kuvaa chepeo zinazoenenda na vita vyetu..Na chepeo hizo ni “Wokovu ule wa kimaandiko kabisa ambao haujachanganywa na chochote”.

DIRII:

Dirii ni vazi la chuma wapiganaji wa zamani walilokuwa wanavikwa katika maeneo ya kifua, ambapo vazi hilo litamkinga mwanajeshi yule dhidi ya mikuki ambayo itarushwa kwa bahati mbaya, na kumfikia maeneo ya kifua au tumbo, hapo vazi hilo la chuma, litamkinga askari yule yule asijeruhiwe.

dirii ni nini

Katika zama zetu hizi, vita vya mikuki havipo tena, vipo vita vya kutumia risasi na bunduki, hivyo dirii za siku hizi, zinatengenezwa mahususi kwa kuzuia risasi zisipenye kwenye kifua au tumbo la mtu, kwa lugha ya kiingereza wanaziita “bullet proof vest”. Tazama picha chini..

bullet proof

Na sisi pia wakristo ni askari wa Bwana, na tupo vitani, Dirii tunayoivaa sisi sio vyuma vya damu na nyama bali ni Dirii ya Haki, ambayo tunaipata katika mistari ifuatayo..(Warumi 2:13, Warumi 3:21-22, Waebrania 10:38, Mathayo 6:33). Na kama vile jinsi vita vinavyobadilika kulingana na Nyakati, vivyo hivyo na vita vyetu sisi watu wa siku za mwisho, ni vikali zaidi kuliko vya watu wa kwanza, hivyo hatuna budi kila siku kuzihakiki dirii zetu kama zinatosha kuzuia silaha za Adui yetu shetani, kama hazitoshi basi hatuna budi kutafuta zinazotosha, na tunazitafuta kwa kulisoma Neno Sana na kulielewa.

UTAYARI:

Utayari unaozungumziwa hapo ni Aina ya vazi la chuma, linalovaliwa katika miguu…Dirii inavaliwa kifuani lakini Utayari unavaliwa miguuni…vazi hili linavikwa katika kila mguu, lengo lake ni kukinga upande wa mbele wa mguu usiweze kujeruhiwa..Kwasababu askari akishajeruhiwa miguu yake hataweza kupambana tena vita hata kama atakuwa na uzoefu mwingi kiasi gani. Tazama picha chini..

utayari

Na sisi kama Askari wa Kristo, ni lazima tuvae utayari miguuni mwetu, ambao tunaupata kwa njia ya injili ya amani.

Hizi ni silaha chache tu za kujikinga, lakini zipo pia silaha moja ya kushambulia ambayo ni UPANGA WA ROHO, Kwa urefu juu ya Silaha hizi kwa Mkristo na namna ya kuzitumia, unaweza kufungua hapa >> Mapambano dhini ya shetani

Na kama bado hujaokoka, na ungependa kufanya hivyo leo, basi usingoje kesho, hapo hapo ulipo Kristo yupo..Hivyo dhamiria kutubu kwa dhati leo, na Kristo atakukubali, kwasababu alisema wote wamjiao, hatawatupa nje kamwe. Hivyo kama utaweza kupiga magoti na kutubu wewe mwenyewe binafsi ni vizuri, lakini kama utahitaji msaada unaweza kufungua hapa >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Au ukapiga namba hizo hapo chini..

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

MAPAMBANO DHIDI YA SHETANI.

MAISHA ULIYOPITIA NYUMA NI USHUHUDA TOSHA WA WEWE KUMTUMIKIA MUNGU:

USIRUHUSU MUNGU AWEKE UADUI KATI YAKO NA WATU WAKO.

NEHUSHTANI (NYOKA WA SHABA).

JE! WEWE NI MWAKILISHI MWEMA?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments