SWALI: Ni muda gani Bwana Yesu alisulibiwa. Je! Ni saa 3 asubuhi kama tunavyosoma kwenye Marko, au saa 6 mchana kama tunavyosoma katika Yohana.
JIBU: Tusome vifungu vyenyewe.
Marko 15:24 “Wakamsulibisha, wakagawa mavazi yake, wakayapigia kura kila mtu atwae nini. 25 Basi ilikuwa saa tatu, nao wakamsulibisha”.
Marko 15:24 “Wakamsulibisha, wakagawa mavazi yake, wakayapigia kura kila mtu atwae nini.
25 Basi ilikuwa saa tatu, nao wakamsulibisha”.
Yohana 19:14 “Nayo ilikuwa Maandalio ya pasaka, yapata saa sita. Akawaambia Wayahudi, Tazama, Mfalme wenu! 15 Basi wale wakapiga kelele, Mwondoshe! Mwondoshe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Je! Nimsulibishe mfalme wenu! Wakuu wa makuhani wakamjibu, Sisi hatuna mfalme ila Kaisari”.
Yohana 19:14 “Nayo ilikuwa Maandalio ya pasaka, yapata saa sita. Akawaambia Wayahudi, Tazama, Mfalme wenu!
15 Basi wale wakapiga kelele, Mwondoshe! Mwondoshe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Je! Nimsulibishe mfalme wenu! Wakuu wa makuhani wakamjibu, Sisi hatuna mfalme ila Kaisari”.
Shalom.
Sababu ya utofauti wao ni kuwa uandishi wa Marko ulitumia mfumo wa saa za kiyahudi, wakati uandishi wa Yohana ulitumia mfumo wa saa za Kirumi.
Mfumo wa kiyahudi, kwa kawaida siku mpya huwa zinaanzia saa 12 asubuhi, Ndio maana kuna mahali Bwana Yesu alisema “Je! Saa za mchana si kumi na mbili? (Yohana 11:9)”
Inapoanza saa 1 ndio saa ya kwanza, inapofika saa mbili ndio saa ya pili, vivyo hivyo na saa ya tatu na kuendelea. Hivyo katika Marko, inatuambia Bwana Yesu alisulibiwa taa tatu asubuhi. Na ndio maana katika Marko tunaona Bwana Yesu alisulibiwa saa 3 asubuhi.
Lakini sasa tukirudi kwenye mfumo wa muda wa kirumi ambao, Yohana aliutumia, anatuambia muda wa saa 6 wayahudi ndio walimleta kwa Pilato, ni rahisi kudhani maandiko yanajipinga lakini hapana, kwa mfumo wa muda wa kirumi, saa moja ilikuwa inaanza saa 6 usiku. Kama ilivyo sasa.
Hivyo Walipomkamata na kumpeleka kwa Pilato, ni kwamba saa 6 zilikuwa zimeshapita tangu siku ilipoanza, ambayo ni sawa na saa 12 asubuhi. Hivyo shamra shamra zote, mpaka kumpiga mijeledi na kumtwika msalaba wake na kumpeleka Goligotha, ilikuwa imeshafika saa 3 asubuhi, ndipo akasulibiwa. Sawa sawa na maandiko ya Marko.
Kwa hiyo kwa kuhitimisha ni kuwa, Bwana wetu Yesu Kristo alisulibiwa saa 3 asubuhi,akafa saa 9 alasiri, na katika huo muda kuanza saa 6 mchana mpaka saa 9 alasiri ndio kulikuwa na lile giza, kisha akakata roho. Lakini Bwana Yesu hakusulibiwa saa 6 mchana.
Luka 23:44 “Hapo ilikuwa yapata saa sita, kukawa giza juu ya nchi yote hata saa kenda, 45 jua limepungua nuru yake; pazia la hekalu likapasuka katikati. 46 Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu. 47 Alipokwisha kusema hayo alikata roho. Yule akida alipoona yaliyotukia, alimtukuza Mungu, akisema, Hakika yake, mtu huyu alikuwa mwenye haki”.
Luka 23:44 “Hapo ilikuwa yapata saa sita, kukawa giza juu ya nchi yote hata saa kenda,
45 jua limepungua nuru yake; pazia la hekalu likapasuka katikati.
46 Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.
47 Alipokwisha kusema hayo alikata roho. Yule akida alipoona yaliyotukia, alimtukuza Mungu, akisema, Hakika yake, mtu huyu alikuwa mwenye haki”.
Bwana akubariki.
Je! Umeokoka? Je! Una habari kuwa tunaishi katika kizazi ambacho kinaweza kushuhudia tukio la kurudi kwa pili kwa Bwana Yesu Kristo, duniani? Kama bado unashikilia udhehebu au udini, fahamu kuwa Kristo haji kunyakuwa watu wa namna hiyo. Atakuja kunyakuwa watu waliozaliwa kweli mara ya pili, kwa maji na kwa Roho na kusimama katika utakatifu. Hao ndio watakaokwenda kwenye unyakuo. Na kundi hilo litakuwa ni dogo sana, kama biblia inavyotabiri ,lakini wengine wote waliosalia wataingia katika dhiki kuu ya mpinga-Kristo.
Swali nj je! Wewe utakuwa miongoni mwa hilo kundi dogo litakalokwenda kumlaki Bwana mawinguni? Jibu, unalo, injili umesikia, na uzuri ni kwamba wokovu unapatikana bure, ukiukosa ni umejitakia mwenyewe kwa akili zao.
Maran Atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
UNYAKUO.
KWASABABU MUDA TULIOBAKIWA NAO SI MWINGI.
Bwana Yesu alimaanisha nini kusema “Saa yangu haijawadia?”
BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?
YAFAHAMU MAPENZI KAMILI YA MUNGU KWA MAADUI ZAKO.
Rudi nyumbani
Print this post