Kutazama Nyakati mbaya ni kufanyaje?.

Kutazama Nyakati mbaya ni kufanyaje?.

Kumbukumbu 18:10 “Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, WALA MTU ATAZAMAYE NYAKATI MBAYA, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,

11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu”.

Kutazama Nyakati mbaya kunakozungumziwa hapo ni “KWENDA KUTAFUTA SABABU YA ISHARA FULANI AMBAZO ZINAAMINIKA KUWA NI MBAYA”.. Mfano wa mtu akipishana na mbwa mweusi, au paka mweusi njiani au akimwona bundi juu ya bati lake, huwa inaaminika kuwa ni ishara mbaya au ya jambo fulani baya linalokuja.. Au mtu akijikwaa anaamini kuwa kuna mtu anamzungumzia vibaya…Hivyo mtu kama huyo unakuta anaenda kwa mganga, au kwa mnajimu, kutafuta maana ya ishara hiyo,  au mbaya anayemfuatilia, sasa mtu huyo ndiye anayetafsirika  kama “mtu atazamaye Nyakati mbaya”

Katika biblia Bwana Mungu aliwakataza wana wa Israeli, tabia ya kutazama nyakati mbaya. Kwasababu kwasababu ni imani potofu, ambayo inamwelekeza mtu kamwamini na kumwabudu shetani.

Kumbukumbu 18:13 “Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako.

14 Maana mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanaoshika nyakati mbaya na kutazama bao; bali wewe, Bwana, Mungu wako, hakukupa ruhusa kutenda hayo”.

Jambo hilo hilo Mungu analikataa hata sasa, kwasababu yeye ni Yule Yule jana na leo na hata milele (Waebrania 13:8).

Ukiwa ndani ya Kristo, viumbe na wanyama si kitu kwako, bundi na popo kwako watakuwa ni ndege wa kawaida, huna haja ya kuwaogopa wala kuwatazama hao kama ishara ya jambo fulani lijalo…. Ishara ya mambo mabaya yajayo ni dhambi maishani mwetu!.

Ukiwa msengenyaji, au mwasherati,  au ulevi, au  muabuduji wa sanamu basi hiyo ndio ishara tosha ya Majanga yajayo!.. Lakini tukiwa wasafi na dhamiri zetu zikiwa safi mbele za Mungu, hatuna haja ya kutafuta kuangalia nyakati mbaya kwasababu hakuna mabaya yoyote yatakayotujia, tunakuwa tunalindwa na kuzungukwa na Nguvu za Mungu.

Lakini ukitoka kwenda kwa mganga kutafuta hatima ya kesho yako, kutokana na ishara uliyoiona, ambayo unaamini kuwa ni ishara mbaya, basi fahamu kuwa unafanya machukizo mbele za Mungu, na siku ya mwisho utasimama hukumuni.

Bwana atusaidie tuepukane na hayo yote.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Kutazama bao ni kufanya nini?

MUNGU ATAKUUA UKIWA MBAYA MACHONI PAKE.

NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.

UTAYAFIKIAJE MANENO SAFI YA MUNGU?

Je ushabiki wa mpira ni dhambi?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Gratian Katunzi
Gratian Katunzi
1 year ago

Ubarikiwe na Bwana, masomo yako ni yananipa mwanga kila kukicha, nazidi kujifunza na kumjua Mungu ipasavyo, Mungu nawe akutunze wewe na nyumba yako pia.