Vitabu vya Deuterokanoni ni vya kiMungu?

Vitabu vya Deuterokanoni ni vya kiMungu?

Swali: Deuterokanoni ni nini?  na je vitabu vya Deutorokanoni ni vitabu vya kiMungu? (ambavyo vimevuviwa na Roho Mtakatifu) na vyenye kufaa kwa mafundisho.?

Jibu: Deuterokanoni ni vitabu vingine saba (7) ambavyo vimeongezwa na kanisa Katoliki juu ya vitabu 66 vya Biblia takatifu, na hivyo kufanya jumla ya vitabu 73 katika biblia ya kikatoliki. Maana ya neno “Deuterokanoni” ni “Orodha ya pili” ambayo imekuja baada ya orodha ya kwanza yenye vitabu 66

Na ordha hiyo ya vitabu vya Deuterokanoni ni..

1. Tobiti

2. Yudith

3. Wamakabayo I

4. Wamakabayo II

5. Hekima

6. Yoshua bin Sira

7. Kitabu cha Baruk.

Vitabu vya Deuterokanoni, viliandikwa baada ya nabii wa Mwisho (Nabii Malaki) kupita!.. Na vitabu hivi hapo kabla havikuhesabiwa kuwa vitabu vitakatifu  na pia wakristo!!..na wala havikuwekwa katika orodha ya vitabu vitakatifu au vya mafundisho ya kiMungu.

Vilikuja kuongezwa katika orodha ya vitabu vitakatifu na Papa Damasus 1 katika karne ya 4.

Lakini swali ni je!.. Vitabu hivi ni vitabu vitakatifu? Na kama sio kwanini?

Jibu ni kwamba vitabu hivi si vitabu vitakatifu wala vilivyovuviwa na Roho Mtakatifu, kwasababu zifuatazo.

Vinakinzana na vitabu vingine vitakatifu.

Kamwe Mungu hajichanganyi, na wala Neno lake halijichanganyi..lakini vitabu hivi vina mafundisho ambayo yanakinzana na mafundisho ya kweli ya Roho mtakatifu yaliyopo ndani ya vitabu 66. (Vitabu 66 havipingani hata kimoja, bali vyote vinakubaliana katika jambo moja, kwasababu vimevuviwa na Roho huyo huyo mmoja), lakini vitabu vya Deuterokanoni vinapingana na vitabu hivi vingine 66.

Kwamfano kitabu cha 2 Wamakabayo 12:43-45 kinafundisha Maombi kwa Wafu, na mafundisho ya toharani, jambo ambalo halionekani katika vitabu vingine 66 vya biblia.

Hakuna mahali popote katika biblia, panaonyesha kuwa wafu waliombewa au wanaombewa.. Zaidi sana biblia inasema katika Waebrania 9:27 “ kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu”.

Kwahiyo kitabu hiki si cha kiMungu, kwasababu Mungu kamwe hawezi kujichanganya..huku aseme hivi, na kule aseme vingine..

Na pia vitabu hivi, kuna sura zinazofundisha “Ulevi”, “Uchawi” na “Mazungumzo ya uongo”. Kwahiyo kwa ufupi si vitabu vya kiMungu, bali ni vya adui, shetani..ambavyo lengo lake ni kuwapeleka watu mbali na Mungu.

Biblia yenye vitabu 66, ndio biblia pekee ambayo mwanzo wake hadi mwisho wake imevuviwa na Roho Mtakatifu, na Ndio Neno la Mungu pekee, lakini hiyo yenye vitabu vya Deuterokanoni na nyingine yoyote yenye vitabu Zaidi ya hivyo ni ya kishetani, na si ya kuisoma wala kusikiliza mahubiri yanayotumia vitabu hivyo.

1Timotheo 4:1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani”

Bwana Yesu akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

HEKIMA YA KIMUNGU, INAINGIAJE MIOYONI MWETU?

Biblia ina vitabu vingapi?

KITABU CHA UZIMA

Je! tunapaswa kukiamini Kitabu cha Henoko?

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1

Rudi nyumbani

Maran atha!

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
GERVAS
GERVAS
11 months ago

NI KITABU KIPI HICHO KILICHO RUHUSU UONGO NA UCHAWI