Je ni Mungu au Malaika?

Je ni Mungu au Malaika?

Swali: Je biblia inajichanganya katika Zaburi 8:4-5 na Waebrania 2:6-7. Maana sehemu moja inataja ‘Mungu’, na sehemu nyingine ‘Malaika’.


Jibu: Turejee.

Zaburi 8:4 “Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie?

5 Umemfanya mdogo punde KULIKO MUNGU; Umemvika taji ya utukufu na heshima”.

Tusome tena Waebrania 2:6-7..

Waebrania 2:6 “Mwanadamu ni nini hata umkumbuke, Ama mwana wa binadamu, hata umwangalie?

7  Umemfanya mdogo punde kuliko MALAIKA, Umemvika taji ya utukufu na heshima, Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako”.

Katika Waebrania mwandishi ana nukuu maneno kutoka katika Zaburi, lakini ni kama ana nukuu kitu tofauti na kilichoandikwa kule, kwamaana yeye anataja Malaika na wakati mwandishi wa Zaburi alitaja Mungu.. Sasa swali biblia inajichanganya?.

Jibu ni La! Biblia haijichanganyi wala haijakosewa.. Isipokuwa fahamu zetu na pambanuzi zetu ndizo zinazojichanganya.

Sasa ili tuelewe ni vizuri kuzielewa kwanza lugha za kibiblia..

Si kila mahali panapotajwa Mungu, panamaanisha Mungu-muumba, La! Sehemu nyingine panamaanisha Ufalme wa Mungu (yaani jeshi la Mbinguni yaani Malaika na vyote vilivyopo kule)…Na sehemu mojawapo ambayo iliyotajwa Mungu ikimaanisha Jeshi la Mbinguni ni hii Zaburi 8:5 “…Umemfanya mdogo punde KULIKO MUNGU”.

Mungu inayotajwa hapo inamaanisha Ufalme wa Mungu (yaani jeshi la Malaika) na si MUNGU aliye Muumbaji, ambaye ni MMOJA.

Ni sawa na jina ISRAELI katika biblia,…kuna mahali linamaanisha mtu mmoja (ambaye ni Yakobo mwana wa Isaka, Mwanzo 35:10).. Lakini pia jina hili kuna mahali linamaanisha TAIFA (Ufalme, Kutoka 5:2).

Au “Yuda”, kuna mahali anatajwa kama Mtu (Mwana wa Yakobo), lakini pia kama Taifa.

Vivyo hivyo na Mungu, cheo hicho kinaweza kufunua “Ufalme” au nafasi ya MUNGU MWENYEWE kama Muumba.

Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba mwandishi wa kitabu cha Waebrania hajapishana na mwandishi wa Zaburi.

Kujua kwa mapana ni ufunuo uliopo nyuma ya andiko hili.. “Amefanyika bora kuliko Malaika” basi fungua hapa >>>AMEFANYIKA BORA KUPITA MALAIKA!

Bwana akubariki.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Ielewe kwa kina Waebrania 13:5 maana yake.

MUNGU MWENYE HAKI.

UTAJI ULIOKUWA JUU YA USO WA MUSA.

JE! UNA MHESHIMU MUNGU?

Mwandishi wa kitabu cha Zaburi ni nani?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments