Mbaruti ni mmea gani? (Mathayo 7:16)

Mbaruti ni mmea gani? (Mathayo 7:16)

Mbaruti ni nini?.(Mibaruti ni mimea ya aina gani) na umebeba ujumbe gani kiroho?.


Jibu: Turejee,

Mathayo 7:16 “Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?”

Soma pia 2Wafalme 14:9, 2Nyakati 25:18 na Hosea 10:4.

Mbaruti/Mibaruti ni jamii ya mimea yenye maua, ambayo mara nyingi inajiotea maporini. (Mimea hii inatoa matunda ambayo ina miiba inayoizunguka pande zote, kuifanya kutolika na wanyama walao nyasi). Tazama picha juu..

Katika biblia Bwana YESU alinukuu mimea huu wa mbaruti katika swali lililowahusu manabii wa uongo.. Aliuliza je watu huchuma tini katika mibaruti?,.. Maana yake ni jambo lisilowezekana kupata matunda ya “Tini“ kutoka katika jamii ya mimea hiyo ya maua ya mibaruti.

Vile vile akasema haiwezekani kuchuma zabibu kutoka kwenye miti ya miiba…

Kuonyesha kuwa Manabii wa uongo wanatoa matunda yenye MIIBA MIIBA!!.yasiyofaa kwa kuliwa bali yanaumiza na kuchoma!.

Moja ya matunda wanayotoa ni tamaa za fedha, (wakizitamani na kuwafundisha watu hizo)..ambazo biblia inasema wanaozama huko wanajichoma kwa maumivu mengi..

1Timotheo 6:10 “Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi”.

Manabii wa uongo kamwe hawahubiri wala kufundisha Toba na Utakatifu, wala safari ya kwenda mbinguni hawaihubiri kwasababu huko hawaendi!.na wao si wasafiri wa kwenda huko, hivyo mioyo yao ipo hapa hapa duniani na wanahubiri vitu vya duniani, pasipo kuweka mambo katika uwiano.

Mathayo 7:15 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.

16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?

17 Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.

18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.

19 Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. 7.20 Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua”

Bwana atusaidie.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

NI SAHIHI KABISA, HUU SI WAKATI WA TINI!

SHAMBA HUWA HALIMTAMBUI WALA KUMSUBIRIA MKULIMA.

UMEIZALIA MATUNDA MIAKA 4 YA NEEMA ULIYOPEWA?

Kwanini Bwana Yesu alivikwa taji ya miiba?

USIPOTEZWE NA MANENO YA MANABII WA UONGO.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments