SWALI: Mwandishi wa kitabu cha Zaburi ni nani? Ni mpangalio wake upoje kulingana na mwandishi?
JIBU: Kitabu Cha Zaburi hakikuandikwa na mtu mmoja, Bali ni mjumuisho wa waandishi mbalimbali. Kitabu hiki ndio kilichoandikwa na waandishi wengi kuliko vyote kwenye biblia.
Kiliandikwa katika nyakati mbalimbali Kwa kipindi Cha miaka elfu moja na zaidi..kitabu hiki kimebeba mashahiri, maombolezo, nyimbo na maombi.
Mfalme Daudi ndiye aliyeandika Kwa sehemu kubwa kitabu hichi;
Jumla Zaburi zilizojuliakana kuwa zimeandikwa na Daudi ni 73. Lakini pia zipo nyingine 2 ambazo hazikutajwa moja Kwa moja lakini waandishi wengine katika nyaraka zao walinukuu baadhi ya maneno kwenye Zaburi, na kusema ni ya Daudi.
Ambazo ni Zaburi 2 ambayo sehemu ya maandishi hayo yanatajwa katika Matendo 4:25,
Na Zaburi 95 Waebrania 4:7
Hivyo kudhaniwa kuwa Daudi aliandika Zaburi 75;
Hizi ndio orodha ya hizo Zaburi 73 alizoziandika yeye;
3-9
11-32
34-41
51-65
68-70
86
101
103,
108-110
122
124
131
133
138-145
2. SULEMANI
Mwandishi mwingine ni Sulemani yeye aliandika Zaburi mbili tu..ambazo ni Zaburi 72 na Zaburi 127″
3. ETHANI na HEMANI
Nyingine zimeandikwa na Ethani na Hemani, Hawa ni watu ambao waliokuwa na hekima nyingi mfano wa Mfalme Sulemani, wanatajwa katika vifungu hivi;
1 Wafalme 4:30-31
30 Hekima ya Sulemani ikapita hekima ya wana wote wa mashariki, na hekima zote za Misri.31 Kwa kuwa alikuwa na hekima kuliko watu wote; kuliko Ethani Mwezrahi, na Hemani, na Kalkoli, na Darda, wana wa Maholi; zikaenea sifa zake kati ya mataifa yote yaliyozunguka.
Ethani aliandika Zaburi moja tu nayo ni Zaburi 89
Hemani pia aliandika Zaburi moja ambayo ni Zaburi 88
4. MUSA
Mwandishi mwingine alikuwa ni Musa yeye pia aliandika Zaburi 1 ambayo ni ya 90.
5. ASAFU
Zaburi nyingine 12 ziliandikwa na Asafu na familia yake.
Ambazo ni
50, 73-83
6. WANA WA KORA
Wana wa Kora, waliandika Zaburi 11
42, 44-49,84-85, 87-88
7. WASIOTAMBULIKA
Na Zaburi nyingine 48, zilizobakia hazijulikani waandishi wake.
Hivyo Kwa ufupisho ni kwamba Daudi aliandika Zaburi 73, Sulemani 2, Musa 1, Ethani 1, Hemani 1, Asafu 12, Wana wa Kora 11, wasiotambulika ni 48.
Bwana akubariki.
Ikiwa utapenda kupata uchauzi zaidi ya kitabu Cha Zaburi pitia link hii >> https://wingulamashahidi.org/2020/11/27/vitabu-vya-biblia-sehemu-ya-9-kitabu-cha-zaburi/
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 11 (Mithali, Wimbo ulio bora, Mhubiri)
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA TITO.
Mwanazuoni ni mtu gani kibiblia?
NA TAA YA MUNGU ILIKUWA BADO HAIJAZIMIKA
JINSI YA KUPIGANA MAOMBI YA VITA.
MASOMO MAALUMU KWA WANAWAKE.
Kuhimidi ni nini?(Zaburi 31:21)
Rudi nyumbani
Print this post