Na ndivyo ilivyo kwetu, tunapokuwa wakristo tunapaswa tuwe makini sana, tunapaswa tujilinde sana, tunapokaa katikati ya ulimwengu, kwasababu biblia inasema tunakuwa kama Nuru katikati yao, Kwa mienendo yetu na matendo yetu. Lakini sasa matendo yetu yakiwa mabovu ni sawasawa na chumvi iliyoharibika. Tunapotazamwa na dunia tuwe na mienendo inayostahili na bora kuliko yao halafu tunaonekana ni walevi, watukanaji, waasherati, wasengenyaji, watoaji wa maneno ya mizaha, wagomvi, fitna, wivu, na chuki, tunakosa nidhamu katika jamii, je! Tutatiwa nini hata tukolee?. Kilichobaki ni kutupwa tu nje! Na kukanyagwa na watu. Hatua hiyo ni sawa na ile hatua ya kutapikwa, kwasababu unakuwa vuguvugu na si baridi wala si moto,..Ni chumvi iliyoingia mchanga.