Je!Sisi kama wakristo Tunaruhusiwa kuchangia ujenzi wa Imani nyingine?

Je!Sisi kama wakristo Tunaruhusiwa kuchangia ujenzi wa Imani nyingine?

SWALI: Naomba kuuliza kwamfano mimi ni mkristo mwenye uwezo wa kifedha, nikiombwa kuchangia ujenzi wa msikiti, Je! Ni halali kufanya hivyo?


JIBU: Tumeruhusiwa, kutoa misaada yoyote ile (Isiyokinzana na Neno la Mungu) kama tupendavyo kwa jinsi Bwana alivyotujalia bila kujali dini, Imani, jinsia au rangi, kabila n.k.. Kwamfano ukiombwa kujenga shule, au kutoa chakula, au kufadhili wazee wa Imani nyingine  waruhusiwa kufanya hivyo, tena ni vema Zaidi, kwasababu unaonyesha upendo ule wa ki-Mungu kwao, ambao hautoki kwa sababu Fulani.

Lakini ikiwa ni mambo yanayokinzana na Neno la Mungu  kama vile kusapoti  ujenzi wa kiwanda cha pombe, au kusapoti madhabahu nyingine tofauti na ile ya YEHOVA, tunayemwabudu katika Kristo Yesu, hapo hatujaruhusiwa.

Kwasababu upo uhusiano mkubwa sana kati ya sadaka na madhabahu. Kumbuka kiroho Sadaka ni Ibada kamili.

Mathayo 6:21 “kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako”.

Moyo wako hauwezi kuwepo katika kanisa la Kristo, na wakati huo huo uwepo katika msikiti, au katika hekalu la Buddha, au la Baniani ambao mungu wao ni ng’ombe,. Hapo utakachokuwa unakifanya ni uzinzi wa kiroho, unazini na miungu migeni, bila wewe mwenyewe kujijua.

Na biblia inasema Mungu wetu ni Mungu mwenye wivu. Anatufananisha sisi na wake zake. Mungu hatazami tu pale tunapoisujudia au kuitumikia miungu migeni ndio achukizwe hapana, bali anatazama pia na sadaka zetu tuzitoazo.. Je tunazielekeza wapi? Kwake yeye, au kwa miungu migeni. Hapo tunapaswa tuwe makini sana.

Hivyo, kwa kuhitimisha ni kuwa, sisi kama wakristo, hatupaswi kuchangia ujenzi wa madhabahu za wasioamini. Ukiulizwa ni kwanini? Jibu lako ni kuwa IMANI YAKO HAIRUHUSU. Hivyo tu,

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Je! Ni sahihi kwa mkristo kuoa/kuolewa na mtu wa imani nyingine?

JE KUNA UISLAMU KATIKA BIBLIA?

Maana Ya Maneno Katika Biblia.

Matoazi na Matari ni nini? (Kutoka 15:20)

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments