JE KUNA UISLAMU KATIKA BIBLIA?

JE KUNA UISLAMU KATIKA BIBLIA?

Je kuna uislamu katika biblia? na je Muhamadi  katika biblia katajwa wapi?

Japokuwa  Kristo anafahamika na kutajwa katika dini nyingi tofauti tofauti ulimwenguni ikiwemo uislamu lakini Biblia haijataja dini ya kiislamu ndani yake wala haijamtaja popote mtume wa waislamu ajulikanaye kama Muhamad.

Mstari ufuatao ndio unaotumiwa na wafuasi wa dini ya kiislamu kuamini kuwa Muhamad alitabiriwa katika biblia..

Kumbukumbu 18:15 “Bwana, Mungu wako, atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye.

16 Kama vile ulivyotaka kwa Bwana, Mungu wako, huko Horebu, siku ya kusanyiko, ukisema, Nisisikie tena sauti ya Bwana, Mungu wangu, wala nisiuone tena moto huu mkubwa, nisije nikafa.

17 Bwana akaniambia, Wametenda vema kusema walivyosema. Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.

19 Hata itakuwa, mtu asiyesikiliza maneno yangu atakayosema yule kwa jina langu, nitalitaka kwake.

20 Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa.

21 Nawe ukisema moyoni mwako, Tutajuaje neno asilolinena Bwana?

22 Atakaponena nabii kwa jina la Bwana, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena Bwana; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimwogope”

Lakini mstari huo haumzungumzii nabii wao anayeitwa Muhamad bali unamzungumzia Yesu Kristo. Yeye ndiye maneno hayo yanamhusu ambaye Mungu alitia maneno yake kinywani mwake, kwa ishara na uweza mwingi alizungumza vitu na kutabiri na vikaja kutimia na vingine vitatimia siku za mwisho karibia na kurudi kwake..na ndiye aliyepewa Huduma kama Musa ukisoma hapo ya kuwatoa watu katika utumwa wa dhambi.

Soma,

Waebrania 3:1 “Kwa hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu, Yesu,

2 aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemweka, kama Musa naye alivyokuwa, katika nyumba yote ya Mungu.

3 Kwa maana huyo amehesabiwa kuwa amestahili utukufu zaidi kuliko Musa, kama vile yeye aitengenezaye nyumba alivyo na heshima zaidi ya hiyo nyumba”

Huyu Yesu pia, kama maandiko yanavyosema hapo juu atatoka katikati ya jamii ya wana wa Israeli (ambao ndio ndugu zake Musa waliokuwa wanazungumziwa hapo)..Hivyo Muhamadi hakuwa mwisraeli bali alikuwa mtu wa Taifa lingine, na wala hajakidhi sifa hata moja hapo juu.

Kwa ishara na ajabu nyingi Yesu alithibitishwa na Mungu na kwasasa amekabidhiwa mamlaka yote ya mbinguni na duniani, na hakuna mtu anayeweza kufika kwa Baba isipokuwa kwa njia yake yeye.

Hivyo tunaonywa tusidanganyike kwa maneno ya watu wasio na elimu kamili ya kumjua Mungu, ambao wanatumika na roho zidanganyazo aidha kwa kujua au kwakutokujua…Roho hizi kazi yake ni kuyageuza maandiko ili kuwafanya watu wasimwamini Yesu Kristo hata kidogo, na hilo ndio lengo kuu la shetani..ili hatimaye wafe katika kutokuamini kwao na waende jehanamu ya moto..Hivyo tunaonywa tujihadhari sana.. kama biblia inavyosema katika kitabu cha Wakolosai..

Wakolosai 2:8 “Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.

9 Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili.

10 Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka”.

Sasa utauliza waislamu wote ni wabaya? Hapana!..Sio watu wote wabaya..kama vile ilivyo sio wakristo wote wazuri….Kuna baadhi ambao hawaujui ukweli bado lakini siku wakiujua watatoka katika makosa hayo…Hivyo ni  wajibu wetu kuwafundisha katika njia sahihi ili watoke katika mitego hiyo ya ibilisi na si kuwachukia, wala kuwatupia maneno ya dhihaka na laana, Kwasababu ndivyo Kristo anavyotufundisha kwamba tuwapende watu wote bila kuchagua, na Kristo alikufa kwaajili ya watu wote.

Ubarikiwe.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

UKristo Ni Nini?

JINA LA MUNGU NI LIPI?

MADHABAHU NI NINI?

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

FREEMASONS NI NINI? NA MTU ATATOKAJE HUKO?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Kimbe
Kimbe
1 year ago

Nimepend masomo