Sikio lisikialo, na jicho lionalo, BWANA ndiye aliyeyafanya yote mawili.

Sikio lisikialo, na jicho lionalo, BWANA ndiye aliyeyafanya yote mawili.

SWALI: Huu mstari una maana gani ?

Mithali 20:12
[12]Sikio lisikialo, na jicho lionalo,
BWANA ndiye aliyeyafanya yote mawili.


JIBU: Utajiuliza ni kwanini haijasema “Sikio na jicho” Bwana ndiye aliyeyafanya yote mawili..badala yake inasema ..

Sikio lisikialo, na jicho lionalo,
BWANA ndiye aliyeyafanya yote mawili.

Hii ni kuweka msisitizo katika kazi zao jinsi zinavyojitegemea…sikio haliwezi kuona, wala jicho kusikia, kwasababu kila moja limeundiwa mfumo wake tofauti wa kipekee..Lakini kutokufanana kwao haviwafanyi viwe na miungu miwili tofauti..bali ni Mungu yule yule mmoja aliyeviumba vyote.

Hata sasa tunapaswa tutambue kuwa Mungu ni Mungu anayeumba vitu katika mionekano tofauti tofauti..mmoja atamfanya mchina mwingine mwafrika, sio kwamba kuna itilafu au mapungufu katika jamii fulani ndio maana ikawa hivyo hapana.. ndivyo Mungu alivyotaka watu wake wasiwe na mionekano na maumbile yanayofanana, amependa tu iwe hivyo

Vilevile katika Kanisa Mungu ameweka vipawa mbalimbali..mwingine mwinjilisti, mwingine mwalimu, mwingine mchungaji..hata katikati ya hao wainjilisti au manabii bado kawatofautisha wote wasifanane..

Kutokuhubiri kwa kufoka au kwa utulivu kama yule hakukufanyi wewe usiwe na karama ile..

1 Wakorintho 12:4-6
[4]Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule.
[5]Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule.
[6]Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.

Hivyo tuonapo tofauti hizi, ndani ya kanisa lake, au ulimwenguni tusinyoosheane vidole na kusema yule sio Mungu, maadamu tupo katika mstari ule ule wa imani, hatupaswi kushangaa sana au kulazimisha mambo yote yafanane..bali tukumbuke tu huu usemi..

Sikio lisikialo, na jicho lionalo,
BWANA ndiye aliyeyafanya yote mawili.

Itambue nafasi yako, Mungu aliyokuchagulia, kisha isimamie hiyo kwa bidii kwasababu vyote ni kwa utukufu wake mwenyewe.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

https://wingulamashahidi.org/wp-admin/post.php?post=18939&action=edit#

Ni kweli hakuna mtu aliyewahi kuuona uso wa Mungu Zaidi ya Bwana Yesu?

Biblia ina maana gani inaposema akonyezaye kwa jicho huleta masikitiko?

Kama Mungu ndiye kaumba kila kitu, je ni yeye huyo huyo ndiye aliyeumba dhambi pia?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments