Maherodi walikuwa ni akina nani, Na kazi yao ilikuwa ni ipi?

Maherodi walikuwa ni akina nani, Na kazi yao ilikuwa ni ipi?

Enzi zile za Bwana Yesu kulikuwa na makundi makubwa matatu yaliyokuwa na nguvu sana katika jamii, ambayo  yalikuwa yanampinga  sana vikali Bwana Yesu, tukiachalia mbali Mafarisayo na masadukayo ambao habari zao tunazijua sana, kulikuwa na kundi lingine la tatu lililoitwa Maherodi. Kama jina lao lilivyo ni watu ambao walikuwa wanamsapoti Herode, na kumtambua kama ndiye kiongozi na mtawala pekee anayepaswa kupewa heshima zote za kifalme, na hata utukufu. Kundi hili la watu lilikuwa lipo kisiasa zaidi kuliko kiroho.

Watu hawa hawakuwa na mapatano yoyote na mafarisayo na Masadukayo, kwasababu Masarisayo tangu zamani hawakuukubali utawala wa kirumi, bali walimtazamia Masihi ambaye atatoka katika uzao wa Daudi, atakayewakomboa dhidi ya watawala wao Warumi. Hivyo hawakuwahi kupatana kwa lolote, lakini kwasababu ya wivu ambao walikuwa nao kwa Yesu, walipatana na maherodi, ili tu wapate kuwa na nguvu ya kutosha ya kumwangamiza Bwana Yesu. Kama tu vile  Herode alivyopatana na Pilato wakati ule, watu ambao walikuwa ni maadui wa muda mrefu, lakini kwasababu ya kutanga kumwangamizi mwokozi wakapatana.

Marko 3:6 “Mara wakatoka wale Mafarisayo, wakawa wakifanya shauri juu yake PAMOJA NA MAHERODI, jinsi ya kumwangamiza”.

Na ndio maana utaona, walikuwa wakituma watu kwao, na kumwandalia Yesu maswali ya mtego ambayo walijua majibu yake yatakinzana na sheria za Herode hivyo wapate sababu ya kumshitaki kwa majibu yake, lakini mipango yao wote ilishindikana mara nyingi. Utasoma habari hizo katika vifungu hivi;

Marko 12:13 “Wakatuma kwake baadhi ya Mafarisayo na MAHERODI, ili wamnase kwa maneno”.

Mathayo 22:16 “Wakatuma kwake wanafunzi wao pamoja na MAHERODI, wakasema, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, na njia ya Mungu waifundisha katika kweli, wala hujali cheo cha mtu awaye yote, kwa maana hutazami sura za watu. 17 Basi utuambie, Waonaje? Ni halali kumpa Kaisari kodi, ama sivyo”?

Marko 8:15 “Akawaagiza, akasema, Angalieni, jihadharini na chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode”.

Umeona, watu wa namna hii hata sasa wapo, kila taifa na kila nchi, tukiachilia mbali watu wa dini, ambao wanatumiwa na shetani, lakini wapo pia kundi lingine la watu ambao watakuwa tayari kupenda utukufu wa watawala kuliko utukufu wa Mungu. Kiasi kwamba wakiona jambo lolote hata la ki-Mungu linanyanyuka watataka tu kuliweka chini, hata kama halileti madhara yoyote au halisababishi vurugu yoyote katika  jamii, watataka kulishusha ili tu kuupendeza utawala.

Hawa pamoja na kiongozi wao Herode ndio waliohusika kumfunga na kumuua Yohana Mbatizaji, vilevile kumpeleka Bwana Yesu kwa Pilato.

 Watu kama hawa walikuwepo kipindi cha Bwana Yesu, na watakuwepo hata sasa. Na wakati wa dhiki kuu pia watakuwepo.

Biblia imetuonya tusipende kuwatumainia wanadamu zaidi ya Mungu.

Zaburi 118:8 “Ni heri kumkimbilia Bwana Kuliko kuwatumainia wanadamu”.

Kwasababu anayemtumainia mwanadamu kuliko Mungu, kibiblia watu kama hao wamelaaniwa (Yeremia 17:5).

Bwana atusaidie.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Matuoni ni nini katika biblia?

IMESALIA RAHA YA SABATO KWA WATU WA MUNGU.

KUSUDI LA MIMI KUWEPO DUNIANI NI LIPI?

Swali: Je Ni sahihi kwa Mkristo kupeleka kesi mahakamani?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments