SWALI: Nini maana ya hii mistari?
Isaya 42:19 “Ni nani aliye kipofu, ila mtumishi wangu? Au aliye kiziwi, kama mjumbe wangu nimtumaye? Ni nani aliye kipofu, kama yeye aliye na amani? Naam, kipofu kama mtumishi wa Bwana?
20 Unaona mambo mengi, lakini huyatii moyoni; masikio yake ya wazi, lakini hasikii”.
JIBU: Maneno hayo hayamaanishi kuwa watumishi wa Mungu wote ni vipofu na viziwi kwamba wanaona mambo mengi lakini hawayatilii maanani, hapana.
Bali Isaya kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu aliandika kwa wayahudi, Ambao hao ndio waliokuwa kwanza kumjua Mungu, kufahamu sheria zake, kuona miujiza yake na matendo yake makuu, tangu zamani, na ndio maana akawafananisha na watumishi / wajumbe wake. Lakini kinyume chake wao ndio wakawa wa kwanza kukimbilia kuabudu miungu mingine, na kufuata mambo maovu, kuliko hata mataifa ambayo hayamjui Mungu.
Jambo kama hilo liliendelea mpaka kipindi cha kutokea kwa Masihi duniani(Yesu Kristo), mafarisayo na waandishi ambao ndio wangepaswa wawe wa kwanza kumtambua Kristo wao, na kumwamini, kutokana na kuwa walishajua unabii wake katika torati tangu zamani, lakini kinyume chake ndio waliokuja kumpinga, na kumuua.
Na ndio maana Bwana Yesu akawaambia maneno haya..
Yohana 9:39 “Yesu akasema, Mimi nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu, ili wao wasioona waone, nao wanaoona wawe vipofu. 40 Baadhi ya Mafarisayo waliokuwapo pamoja naye wakasikia hayo, wakamwambia, Je! Sisi nasi tu vipofu? 41 Yesu akawaambia, Kama mngekuwa vipofu, msingekuwa na dhambi; lakini sasa mwasema, Twaona; basi dhambi yenu inakaa”.
Yohana 9:39 “Yesu akasema, Mimi nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu, ili wao wasioona waone, nao wanaoona wawe vipofu.
40 Baadhi ya Mafarisayo waliokuwapo pamoja naye wakasikia hayo, wakamwambia, Je! Sisi nasi tu vipofu?
41 Yesu akawaambia, Kama mngekuwa vipofu, msingekuwa na dhambi; lakini sasa mwasema, Twaona; basi dhambi yenu inakaa”.
Unaona? Hata sasa, inasikitisha kuona baadhi ya watu wanaojiita ni watumishi wa Mungu ni vipofu rohoni. Kwasababu kama tutashindwa kujua kiini cha Kristo kuja hapa duniani ni nini. matokeo yake tunaigeuza injili ya Kristo kuwa sehemu ya biashara, na mahali pa kutafutia tu mafanikio, na sio wokovu tena, hakuna cha kukemewa dhambi, wala mafundisho ya mbinguni. Huo ni upofu wa hali ya juu sana.
Tunakuwa hatuna tofauti na wale mafarisayo na masadukayo, na wale watumishi wa mishahara ambao Bwana Yesu aliwataja katika. Yohana 10:12-13
Bwana atusaidie sana, tusiwe vipofu na viziwi, kwa kubaki katika misingi ya Neno la Mungu..
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
WANA WA MAJOKA.
WAPE WATU WANGU RUHUSA ILI WAPATE KUNITUMIKIA.
Ngome ni nini? Kwanini Mungu anafananishwa na ngome?
TAFAKARI SANA KABLA YA KUAMUA HATIMA YAKO.
Mharabu ni nani katika biblia?
Rudi nyumbani
Print this post