MWANAMKE UKITAKA KIBALI, USIWE MTU WA KUPENDA VITU. (Esta 2:17)

by Admin | 24 April 2024 08:46 pm04

(Masomo maalumu kwa wanawake).

Kama wewe ni mwanamke na unatamani kupata kibali cha ndoa, au kupata mtu sahihi wa atakayekupenda, basi kuwa kama Esta, ambaye alikuwa na tabia ya kutokupenda-penda vitu!… Wengi wanadhani ubikira ndicho kigezo cha juu ya kupata kibali… Nataka nikuambie sivyo!.. walijitokeza mabikra wengi mbele ya Mfalme Ahasuero, lakini ni mmoja tu aliyechaguliwa..

Sasa ni kigezo gani cha juu kilichompa Esta umalkia??….Turejee maandiko tutapata majibu..

Esta 2:15 “Hata ilipowadia zamu yake Esta, binti Abihaili, mjomba wake Mordekai, ambaye alimtwaa kuwa binti yake, ili aingie kwa mfalme, YEYE HAKUTAKA KITU, ila vile vilivyoagizwa na Hegai, msimamizi wake mfalme, mwenye kuwalinda wanawake. Naye huyu Esta alikuwa amepata kibali machoni pa wote waliomwona.

16 Basi Esta alipelekwa kwa mfalme Ahasuero, katika nyumba ya kifalme, mwezi wa kumi, ndio mwezi wa Tebethi, mwaka wa saba wa kumiliki kwake.

17 MFALME AKAMPENDA ESTA KULIKO WANAWAKE WOTE, NAYE AKAPATA NEEMA NA KIBALI MACHONI PAKE KULIKO MABIKIRA WOTE; BASI AKAMTIA TAJI YA KIFALME KICHWANI PAKE, AKAMFANYA AWE MALKIA BADALA YA VASHTI”.

Esta hakuwa na tabia ya kupenda-penda vitu (kwa ufupi hakuwa na tamaa) na wala hakuwa na mambo mengi!!.. aliingia kwa mfalme yeye kama yeye, katika uhalisia wake!.. wakati wengine walitaka waingie kwa mfalme na marashi yao, na mitindo yao, na wapambe wao, ili wakubalike, Esta yeye hakutaka hayo yote, aliona ni ulimbukeni, aliingia yeye kama yeye, isipokuwa vitu vichache ambaye yule msimamizi aliyeitwa Hegai alimshauri.

Hata leo ni hivyo hivyo, Biblia bado ni Neno la Mungu lililo hai, kupitia hilo tunajifunza kanuni nyingi.. kama wewe ni binti!, au mwanamke!.. ukitaka kibali na Neema.. basi KUWA WEWE!!!... Usianze kujibadili maungo yako, au sauti, au chochote kile katika mwili wako ambacho umeumbwa katika ualisi wake, vile vile usiwe mtu wa tamaa ya vitu (kila unachokiona unakitamani)..

Ukiwa mtu wa namna hiyo ni rahisi sana kupata kibali.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Mistari ya biblia kuhusu kibali.

USIWE NA HAKI KUPITA KIASI.

APENDAYE FEDHA HASHIBI FEDHA.

Sadaka ya Moyo ipoje? (Walawi 22:21).

ESTA: Mlango wa 4

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/04/24/mwanamke-ukitaka-kibali-usiwe-mtu-wa-kupenda-vitu-esta-217/