Sadaka ya Moyo ipoje? (Walawi 22:21).

Sadaka ya Moyo ipoje? (Walawi 22:21).

Jibu: Tusome..

Walawi 22:21 “Na mtu awaye yote atakayemtolea BWANA dhabihu katika sadaka za amani, ili kuondoa nadhiri, au SADAKA YA MOYO WA KUPENDA, katika ng’ombe, au katika kondoo, atakuwa mkamilifu, apate kukubaliwa; pasiwe na kilema ndani yake cho chote”.

Sadaka ya Moyo wa kupenda, ni sadaka ambayo wana wa Israeli walimtolea Mungu wao wenyewe kwa kupenda (yaani pasipo kuagizwa wala masharti).

Zilikuwepo sadaka zilizokuwa na sababu, kwa mfano sadaka ya Shukrani, tayari sadaka hiyo inatolewa kwa lengo la kushukuru, kutokana na mambo fulani ambayo mtu kafanyiwa na Mungu.

Lakini sadaka ya Moyo wa kupenda, haikuwa na sababu yoyote nyuma yake… ni mtu tu anapenda  kumtolea Mungu kwasababu amependa tu kufanya hivyo..na wala si kwasababu Mungu kaagiza.

Mfano wa sadaka hiyo ni ile ambayo baadhi ya wana wa Israeli waliipeleka mbele za Bwana wakati wa ujenzi wa Maskani ya Bwana.

Wakati huo Mungu hakuwaagiza wana wa Israeli wachangie gharama za ujenzi huo wa maskani ya Mungu…lakini baadhi ya watu waliguswa na kumtafuta Musa na  kudhamiria kubeba gharama za  kazi hiyo kwa mapenzi yao wenyewe…

 Kutoka 35:29 “Wana wa Israeli WAKALETA SADAKA ZA KUMPA BWANA KWA MOYO WA KUPENDA; wote, waume kwa wake, AMBAO MIOYO YAO ILIWAFANYA KUWA WAPENDA KULETA KWA HIYO KAZI, ambayo BWANA aliamuru ifanywe kwa mkono wa Musa”.

Kutoka 35:21 “Wakaja kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza, na kila mtu ambaye roho yake ilimfanya kuwa apenda, nao wakaleta sadaka za kumpa BWANA, kwa kazi ya hema ya kukutania, na kwa utumishi wake, na kwa hayo mavazi matakatifu”.

Soma pia Kutoka 25:2 na 2Nyakati 29:31.

Swali ni je! katika Agano jipya bado tunazo sadaka kama hizi?..

Jibu ni Ndio! Bado Zipo na ndizo zinazompendeza Bwana, na tunazopaswa kutoa.

Utauliza katika agano jipya tunasoma wapi hayo…??.

2 Wakorintho 9:7 “Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu”.

Umeona sadaka ya Moyo wa kupenda ni sadaka Bwana anayoikubali.

Je na wewe unayo desturi ya kumtolea Bwana kwa moyo wa kupenda au kwa sababu tu ya shinikizo fulani?.

Kamwe usiache kumtolea Mungu, lakini katika kumtolea hakikisha unamtolea kwa Moyo.

Sadaka ya namna hii ni sadaka bora na inayompendeza Mungu

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

APENDAYE FEDHA HASHIBI FEDHA.

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1

Sadaka ya Amani ilikuwaje?

TOA SADAKA ISIYO NA KASORO KWA BWANA.

YAFAHAMU MAPENZI KAMILI YA MUNGU KWA MAADUI ZAKO.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments