Yakobo 1:13 “Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu”
Hapo Neno linasema kuwa Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, kinyume chake ni kweli kwamba yeye anajaribiwa na MEMA tu!. Maana yake tunapofanya mema hapo tunakuwa tunamweka Mungu kwenye jaribu la kutubariki.. Na hivyo ni lazima aachie baraka kwetu.
Lakini tukienda kinyume na Neno lake na huku tunataka atubariki, hapo maana yake tunamjaribu yeye kwa Maovu.. Mfano wa watu waliomjaribu Mungu kwa maovu ni Wana wa Israeli kipindi wapo jangwani, Walitaka Bwana awashushie chakula kile cha kimiujiza, huku mioyoni mwao wamemwacha Mungu, ni watu wenye viburi, ni watu wa kunung’unika, ni watu wasio na heshima wala staha kwa Mungu na mwishowe wakaangukia hukumu.
Waebrania 3:7 “Kwa hiyo, kama anenavyo Roho Mtakatifu, Leo, kama mtaisikia sauti yake,8 Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha, Siku ya kujaribiwa katika jangwa,9 Hapo baba zenu waliponijaribu, wakanipima, Wakaona matendo yangu miaka arobaini.10 Kwa hiyo nalichukizwa na kizazi hiki, Nikasema, Sikuzote ni watu waliopotoka mioyo hawa; Hawakuzijua njia zangu;11 Kama nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia rahani mwangu”.
Waebrania 3:7 “Kwa hiyo, kama anenavyo Roho Mtakatifu, Leo, kama mtaisikia sauti yake,
8 Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha, Siku ya kujaribiwa katika jangwa,
9 Hapo baba zenu waliponijaribu, wakanipima, Wakaona matendo yangu miaka arobaini.
10 Kwa hiyo nalichukizwa na kizazi hiki, Nikasema, Sikuzote ni watu waliopotoka mioyo hawa; Hawakuzijua njia zangu;
11 Kama nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia rahani mwangu”.
Na maandiko yanasema Mungu ni yeye Yule jana na leo na hata milele, alilolikataza miaka elfu 2 iliyopita analitakata hata leo.. Akisema “yeye hajaribiwi na Movu, ni kweli hajaribiwi na hayo”.. Lakini kinyume chake anajaribiwa na Mema yaliyoandikwa katika Neno lake.
Kwamfano unapomtolea Mungu sadaka isiyo na kasoro (Maana yake iliyo sawasawa na Neno lake, na kwa nia njema) Hilo ni jaribu kwa Mungu kukubariki wewe, na hapo utakuwa umemjaribu kwa Mema.
Malaki 3:8 “Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. 9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote. 10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi”.
Malaki 3:8 “Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.
9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.
10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi”.
Na mambo mengine yote mema, ambayo tunayafanya yaliyo sawasawa na Neno la Mungu, mambo hayo ni TANZI kwa Mungu, kutumwagia Baraka zake, au kuzungumza na sisi.
Lakini kama moyoni mwako umemwacha Bwana, halafu unatafuta kuisikia sauti yake, unaenda kwa nabii ili usikie Mungu anasema nini kuhusu wewe, hapo unamjaribu Mungu kwa mabaya na hivyo unajitafutia laana badala ya Baraka.
Ezekieli 14:4 “Basi sema nao, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Kila mtu wa nyumba ya Israeli atwaaye vinyago vyake na kuvitia moyoni mwake, na kuliweka kwazo la uovu wake mbele ya uso wake, na kumwendea nabii; mimi, Bwana, nitamjibu neno lake sawasawa na wingi wa sanamu zake; 5 ili niwakamate nyumba ya Israeli kwa mioyo yao wenyewe, kwa sababu wamefarakana nami kwa vinyago vyao. 6 Kwa sababu hiyo uwaambie nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi; Rudini ninyi, mkageuke na kuviacha vinyago vyenu; mkageuze nyuso zenu zisielekee machukizo yenu yote. 7 Kwa maana kila mtu wa nyumba ya Israeli, au wa wageni wakaao katika Israeli, ajitengaye nami, na kuvitwaa vinyago vyake na kuvitia moyoni mwake, na kuliweka kwazo la uovu wake mbele ya uso wake, kisha kumwendea nabii, na kuniuliza neno kwa ajili ya nafsi yake; mimi, Bwana, nitamjibu, mimi mwenyewe8 nami nitaukaza uso wangu juu ya mtu yule, na kumfanya kuwa ajabu, awe ishara na mithali, nami nitamkatilia mbali, asiwe kati ya watu wangu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.”
Ezekieli 14:4 “Basi sema nao, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Kila mtu wa nyumba ya Israeli atwaaye vinyago vyake na kuvitia moyoni mwake, na kuliweka kwazo la uovu wake mbele ya uso wake, na kumwendea nabii; mimi, Bwana, nitamjibu neno lake sawasawa na wingi wa sanamu zake;
5 ili niwakamate nyumba ya Israeli kwa mioyo yao wenyewe, kwa sababu wamefarakana nami kwa vinyago vyao.
6 Kwa sababu hiyo uwaambie nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi; Rudini ninyi, mkageuke na kuviacha vinyago vyenu; mkageuze nyuso zenu zisielekee machukizo yenu yote.
7 Kwa maana kila mtu wa nyumba ya Israeli, au wa wageni wakaao katika Israeli, ajitengaye nami, na kuvitwaa vinyago vyake na kuvitia moyoni mwake, na kuliweka kwazo la uovu wake mbele ya uso wake, kisha kumwendea nabii, na kuniuliza neno kwa ajili ya nafsi yake; mimi, Bwana, nitamjibu, mimi mwenyewe
8 nami nitaukaza uso wangu juu ya mtu yule, na kumfanya kuwa ajabu, awe ishara na mithali, nami nitamkatilia mbali, asiwe kati ya watu wangu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.”
Bwana Yesu atusaidie.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Je Adamu na Hawa, walikuwa hawafanyi mema kabla ya kula tunda?
TOA HUDUMA ILIYO BORA.
DAMU YA YESU INANENAJE MEMA KULIKO YA HABILI?
LAKINI NINYI, NDUGU, MSIKATE TAMAA KATIKA KUTENDA MEMA.
KWANINI MIMI?
Rudi nyumbani
Print this post