Kipaku ni nini kama tunavyosoma katika biblia?

Kipaku ni nini kama tunavyosoma katika biblia?

Kipaku ni kipele kidogo kinachochipuka kwenye ngozi ya mwanadamu au mnyama. Kipele hichi kinaweza kusababishwa na mabadiliko ya mazingira, au aleji au magonjwa mbalimbali.

Hivyo Neno hili katika biblia linaonekana sehemu nyingi, hususani pale unapotajwa ugonjwa wa ukoma. Kwani ugonjwa huo kabla huujakolea kwenye mwili, huwa unaanza kwanza kama kipeleke kidogo king’aacho kekundu (ndio hicho kipaku). Hivyo katika hatua za awali ilikuwa ni ngumu kukitambua kama ni cha ukoma au cha ugonjwa mwingine wa kawaida. Hivyo ili kuepusha maambukizi zaidi kwa wengine, Mgonjwa Yule alitengwa kwa muda wa siku saba.

Na baada ya siku saba, kuhani huja na kuangalia, kama kipaku kile kimeenea zaidi kwenye mwili na kuzama kwenye ngozi basi ulikuwa ni ugonjwa wa ukoma. Hivyo mtu huyo alitengwa daima, kama hakutakasika.

Walawi 13:1 “Kisha Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,

2 Mtu atakapokuwa na kivimbe katika ngozi ya mwili wake, au kikoko, au kipaku king’aacho, nalo likawa pigo la ukoma katika ngozi ya mwili wake, ndipo atakapoletwa kwa Haruni kuhani, au kwa wanawe, makuhani mmojawapo;

3 na huyo kuhani ataliangalia hilo pigo lililo katika ngozi ya mwili; na kwamba malaika yaliyo katika hilo pigo yamegeuka kuwa meupe, na hilo pigo kuonekana kwake limeingia ndani kuliko ile ngozi ya mwili wake, ni pigo la ukoma hilo; na kuhani atamwangalia na kusema kuwa yu mwenye unajisi.

4 Na hicho kipaku king’aacho, kwamba ni cheupe katika ngozi ya mwili wake, na kuonekana kwake si shimo la kuingia ndani kuliko ngozi, na malaika hayakugeuka kuwa meupe, ndipo kuhani atamweka mahali muda wa siku saba huyo aliye na hilo pigo;

5 kisha kuhani atamwangalia siku ya saba; naye akiona ya kuwa pigo limeshangaa, na pigo halikwendelea mbele katika ngozi yake, ndipo kuhani atamweka mahali muda wa siku saba tena;

6 kisha siku ya saba kuhani atamwangalia tena; na tazama, ikiwa hilo pigo limeanza kufifia, wala pigo halikwendelea mbele katika ngozi yake, ndipo kuhani atasema kuwa yu safi; ni kikoko; naye atazifua nguo zake, kisha atakuwa yu safi”.

Ni fundisho gani lipo nyuma ya pigo hili la ukoma?

Zamani za agano la kale ukoma uliwakilisha pigo kutoka kwa Mungu,. Na sikuzote Mungu kabla hajaleta mapigo hutanguliza kwanza ishara na dalili, Kama vile KIPAKU tu kidogo.. Lakini baada ya siku SABA, huenea mwili wote.

Kufunua nini?

Yesu alipokuwa duniani alisema tubuni kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia, akasema pia kabla ya ule mwisho wa dunia kufika ambapo Mungu ataleta mapigo makubwa sana juu ya ulimwengu huu wa dhambi..Zitatangulia kwanza dalili na ishara, ambazo yeye aliziita ‘mwanzo wa utungu’..Ndio haya matetemeko, majanga, magonjwa, tetesi za vita, n.k.  tuliyoyana tangu enzi za Bwana hadi sasa, (Ndio kipaku chenyewe rohoni, ila ukoma wenyewe kuenea bado).

Lakini aliruhusu kipindi cha neema cha NYAKATI SABA kipite kwanza, ili watu watengeneze mambo yao, watubu dhambi zao, Bwana awaepushe na uharibifu huo. Ndio hii miaka 2000, sasa ambapo ndani yake nyakati saba za kanisa zinapita, na sisi watu wa kizazi hiki ndio tupo katika kanisa la mwisho kabisa la saba, lijulikanalo kama LAODIKIA (Ufunuo 3:14-22).

Hivyo ni kama dalili za ukoma tu, mwisho wa siku saba, uhakika unapatikana. Na ndivyo ilivyosasa, hivi karibuni Unyakuo utapita, Bwana atawaondoa kwanza watu wake ulimwenguni.  Na baada ya hapo atatusha laana yake ya mwisho juu ya huu ulimwengu, ndio vile vitasa saba vinavyozungumziwa katika kitabu cha Ufunuo 16.

Jiulize ndugu yangu, je huu ukoma ulioanza ndani yako, kama kipaku, je umeshaupatia tiba? Kumbuka tiba ni Bwana Yesu, usisubiri unyakuo ukupite, au ufe katika dhambi zako, mguekie Masihi akuoshe na kukusafisha.

Maandiko yanasema kipindi cha Elisha, kulikuwa na wakoma wengi, Israeli, lakini hakutumwa kwa mmojawapo wao, ila Naamani mtu wa shamu (Luka 4:27). Kwasababu gani? Kwasababu alikubali kutii maagizo aliyopewa na Elisha kwenda kujichovya mtoni mara saba..Leo hii watu hatutaki kusoma kitabu cha Ufunuo, ambapo ndani yake tutakutana na ujumbe wa makanisa saba na nyakati zao. Ambazo kwa kuzielewa hizo tutaweza kuepukana na ukoma huu wa rohoni ambao Mungu anawapiga watu sasa.. Badala yake tunapenda kusikia habari ya kutabiriwa, na mafanikio ya mwilini.. Hii ni hatari kwasababu tunaweza kujikuta tunaachwa katika unyakuo, kama sio kufa katika dhambi.

Bwana atusaidie tulipende Neno lake.

Maran Atha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Ukoma wa nyumba ulifunua nini zamani?

Hawa ndege katika Walawi 11:13-19 ndio ndege gani kwasasa?

BWANA alimaanisha nini kwenye mstari huu Marko 2:21″ Hakuna mtu ashonaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kukuu?

Je mke wa Musa alikuwa ni Mweusi?

Hawa ndege katika Walawi 11:13-19 ndio ndege gani kwasasa?

Ni lini na wapi Ibrahimu aliioona siku ya Bwana akashangilia?

Nini tofauti ya Majira na Wakati?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments