Mistari ya biblia kuhusu kibali.

Mistari ya biblia kuhusu kibali.

Ifuatayo ni baadhi ya mistari ambayo itamsaidia mtu kupata kibali aidha KWA MUNGU au kwa WANADAMU, au KWA WAKUU Au vyote kwa pamoja (Mungu pamoja na wanadamu).

KIBALI CHA MUNGU:

Mwanzo 4:6 “Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?

7 Kama ukitenda vyema, HUTAPATA KIBALI? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde”

1Samweli 1:17 “Ndipo Eli akajibu, akasema, Enenda kwa amani; na Mungu wa Israeli akujalie haja yako uliyomwomba.

18 Naye akasema, Mjakazi wako na AONE KIBALI MACHONI PAKO. Basi huyo mwanamke akaenda zake, naye akala chakula, wala uso wake haukukunjamana tena”. 

KWA WATU:

Kutoka 11:3 “Bwana akawapa watu hao KIBALI MACHONI PA WAMISRI. Zaidi ya hayo, huyo Musa alikuwa ni mkuu sana katika nchi ya Misri, machoni pa watumishi wa Farao, na machoni pa watu wake”

Esta 2:15 “Hata ilipowadia zamu yake Esta, binti Abihaili, mjomba wake Mordekai, ambaye alimtwaa kuwa binti yake, ili aingie kwa mfalme, yeye hakutaka kitu, ila vile vilivyoagizwa na Hegai, msimamizi wake mfalme, mwenye kuwalinda wanawake. Naye huyu Esta alikuwa amepata kibali machoni pa wote waliomwona”

KWA WAKUU NA WAFALME:

Mwanzo 39:21 “Lakini Bwana akawa pamoja na Yusufu, akamfadhili, AKAMPA KIBALI machoni pa mkuu wa gereza.

22 Mkuu wa gereza akawatia mkononi mwa Yusufu watu wote waliofungwa, waliomo gerezani; na yote yaliyofanyika humo ndiye aliyeyafanya”

1Samweli 16:22 “Kisha Sauli akapeleka watu kwa Yese, akasema, Tafadhali, mwache Daudi asimame mbele yangu; maana AMEONA KIBALI machoni pangu”.

1Samweli 27:5 “Daudi akamwambia Akishi, Sasa kama nimeona KIBALI MACHONI PAKO na nipewe mahali katika miji hii mmojawapo mashambani, nipate kukaa huko; mbona mtumwa wako akae katika mji wa kifalme pamoja na wewe?”

Nehemia 2:4 “Ndipo mfalme akaniambia, Una haja gani unayotaka kuniomba? Basi nikamwomba Mungu wa mbinguni.

5 Nikamwambia mfalme, Mfalme akiona vema, na ikiwa mimi, mtumishi wako, NIMEPATA KIBALI MACHONI PAKO, tafadhali unipeleke mpaka Yuda, niuendee mji wa makaburi ya baba zangu, nipate kuujenga”

Esta 5:2 “Ikawa, mfalme alipomwona malkia Esta amesimama uani, yeye AKAPATA KIBALI machoni pake; naye mfalme akamnyoshea Esta fimbo ya dhahabu aliyokuwa nayo mkononi. Basi Esta akakaribia, akaigusa ncha ya fimbo”

KWA MUME:

Ruthu 2:10 “Ndipo aliposujudia, akainama mpaka nchi, akamwambia, Jinsi gani NIMEPATA KIBALI machoni pako, hata ukanifahamu, mimi niliye mgeni?

11 Naye Boazi akajibu, akamwambia, Nimeelezwa sana yote uliyomfanyia mkweo, tangu alipokufa mumeo; na jinsi ulivyowaacha baba yako na mama yako, na nchi yako uliyozaliwa, ukawafikilia watu usiowajua tangu hapo”.

Esta 2:17 “Mfalme akampenda Esta kuliko wanawake wote, naye AKAPATA NEEMA NA KIBALI machoni pake kuliko mabikira wote; basi akamtia taji ya kifalme kichwani pake, akamfanya awe malkia badala ya Vashti”

KWA MUNGU PAMOJA NA WANADAMU:

1Samweli 2:26 “Na yule mtoto, Samweli, akazidi kukua akapata kibali kwa Bwana, na kwa watu pia”

Mithali 3:4 “Rehema na kweli zisifarakane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.

4 Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu.

5 Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe”

BWANA AKUBARIKI.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

NJIA NYINGINE YA KUPATA REHEMA NA KIBALI KUTOKA KWA MUNGU.

Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe;(Mithali 16:2)

MAPAMBO YA WANAWAKE WALIOUKIRI UCHAJI WA MUNGU.

WAANDAA MEZA MBELE YANGU, MACHONI PA WATESI WANGU

JE! NINAWEZA KUPOTEZA FURAHA YA WOKOVU?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments