Maneno ya mchongezi ni kama vitoweo; Nayo hushukia pande za ndani za tumbo

Maneno ya mchongezi ni kama vitoweo; Nayo hushukia pande za ndani za tumbo

SWALI: Nini maana ya huu mstari?

Mithali 18:8 “Maneno ya mchongezi ni kama vitoweo; Nayo hushukia pande za ndani za tumbo”.


JIBU: Mchongezi kibiblia ni mtu anayesambaza habari mbaya za wengine, au msengenyaji, na mlalamikiaji wa wengine. Jambo ambalo Mungu kalionya tangu zamani, hata kipindi wana wa Israeli wakiwa jangwani.

Walawi 19:16a “Usiende huko na huko katikati ya watu wako, kama mchongezi;..”

Usengenyaji ni dhambi iliyostahili adhabu kali ya ukoma, kama yaliyomkuta Miriamu alivyofanya kwa Musa. Kwasababu hapo maandiko yanaeleza kuanza kwake ni kama kitoweo, yaani ni kama chakula kizuri sana kinachovutia mdomoni mwa anayekisikia.. Lakini madhara yake ni kwamba kinashuka mpaka pande za ndani za tumbo, ikiwa na maana kuwa huingia ndani kabisa ya moyo wa msikiaji, na kuzaa maumivu makali, Ni heri kingekuwa kinaishia pale mdomoni.

Ni jambo la kuwa nalo makini sana katika kanisa, kwasababu wengi wameacha imani kwasababu ya maneno, wengine wamewekeana chuki kwasababu ya kupokea taarifa zao Fulani kutoka kwa wengine. Vita vya chini chini baina ya mshirika na mshirika, upendo umepoa kwasababu tu ya uchongezi.

Pale mtu anapokufuata na kukwambia.. “nimesikia Fulani na Fulani”…”Unahabari Yule amefanya hivi au vile”…Taarifa kama hizi ngumu kukataa kuzisikia, zinakuja kama kitoweo kizuri sana, kinachovutia kukisikia, lakini hutoa chuki na hasira na uchungu ndani. Kwa mtoaji anaweza kuona kaleta habari njema, lakini kwa mpokeaji, au atakayekuja kusikia baadaye huchimbua matatizo mengi sana.

Hivyo hatupaswi kuruhusu minong’ono yoyote katikati yetu, hata kama tutaona haina madhara yoyote makubwa. Ni kudhibiti huo mnyororo haraka sana, tukiona taarifa Fulani zinaletwa  kwetu zenye maudhui ya masengenyo ni kuzipinga muda huo huo, ili tuepuke madhara zaidi. Roho Mtakatifu alilionya kanisa juu ya jambo hili, hususani kwa wanawake akasema;.

Tito 2:3  “Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji..”

1Timotheo 5:13  “Tena, pamoja na hayo, hujifunza kuwa wavivu, wakizunguka-zunguka nyumba kwa nyumba; wala si wavivu tu, lakini ni wachongezi na wadadisi, wakinena maneno yasiyowapasa”.

Soma 1Timotheo 3:11, 2Timotheo 3:1-3.

Kama mkristo, ni jambo la kujiepusha sana, kuulinda ulimi wako.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

WAMWENDEA YESU KWA KUSAFIWA lyrics na historia

LEO WOKOVU UMEFIKA NYUMBANI HUMU

Kuwaogopa wanadamu huleta mtego,(Mithali 29:25)

Aibusu midomo atoaye jawabu la haki (Mithali 24:26)

KUWA MWOMBOLEZAJI.

Kula uzao wa tumbo lako maana yake nini? (Kumbukumbu 28:53)

MWENDO UNAOSHANGAZA SANA!

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments