WAMWENDEA YESU KWA KUSAFIWA lyrics na historia

WAMWENDEA YESU KWA KUSAFIWA lyrics na historia

WAMWENDEA YESU KWA KUSAFIWA lyrics (Are you washed in the Blood?)


Wimbo huu uliandikwa na ndugu mmoja aliyeitwa Elisha Hoffman mwaka 1878, huko Ohio Marekani. Baada ya kuhitimu katika chuo cha biblia alisimikwa na kuwa mchungaji na kutumika kwa miaka mingi katika huduma hiyo, katika maisha yake yote ya huduma alifanikiwa kuandika nyimbo za kikristo zaidi ya 2000. Na huu “Wamwendea Yesu kwa kusafiwa,

” Ulikuwa ni mmojawapo.

 Wimbo huu umechukia maudhui yake kutoka katika sehemu nyingi za biblia ikiwemo;

Ufunuo 7:14 “Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo”.

Wamwendea Yesu kwa kusafiwa.

****

Wamwendea Yesu kwa kusafiwa,
Na kuoshwa kwa damu ya kondoo?
Je, neema yake umemwagiwa?
Umeoshwa kwa damu ya kondoo?
 
Kuoshwa, kwa damu,
Itutakasayo ya kondoo;
Ziwe safi nguo nyeupe mno;
Umeoshwa kwa damu ya kondoo?
 
Wamwandama daima Mkombozi,
Na kuoshwa kwa damu ya kondoo?
Yako kwa Msulubiwa makazi,
Umeoshwa kwa damu ya kondoo?
 
Kuoshwa, kwa damu,
Itutakasayo ya kondoo;
Ziwe safi nguo nyeupe mno;
Umeoshwa kwa damu ya kondoo?
 
Atakapokuja Bwana-arusi,
Uwe safi kwa damu ya kondoo!
Yafae kwenda mbinguni mavazi,
Yafuliwe kwa damu ya kondoo.
 
Kuoshwa, kwa damu,
Itutakasayo ya kondoo;
Ziwe safi nguo nyeupe mno;
Umeoshwa kwa damu ya kondoo?
 
Yatupwe yalipo na takataka,
Na uoshwe kwa damu ya kondoo,
Huoni kijito chatiririka,
Na uoshwe kwa damu ya kondoo?
 
Kuoshwa, kwa damu,
Itutakasayo ya kondoo;
Ziwe safi nguo nyeupe mno;
Umeoshwa kwa damu ya kondoo?
 

****

Je na wewe uimbapo wimbo huu, maisha yako kweli yameshwa kwa damu ya mwana-kondoo (Yesu Kristo), Je unajua kuwa hukumu haikwepeki kwako ikiwa bado upon je ya Kristo. Hivyo kama hujatubu ni heri ufanye hivyo sasa, Bwana akusafishe uwe safi.

Shalom.

Tazama historia ya tenzi nyingine chini.

Mada Nyinginezo:

NI SALAMA ROHONI MWANGU Lyrics

YESU KWETU NI RAFIKI

USINIPITE MWOKOZI Lyrics

 

UNYAKUO.

EPUKA MUHURI WA SHETANI

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator