KUOTA UPO MAKABURINI.

KUOTA UPO MAKABURINI.

Kuota upo makaburini kuna maanisha nini kibiblia?

Makaburini sikuzote ni mahali wanapolazwa wafu, ikiwa unaota ndoto hii mara kwa mara upo makaburini ni ishara kuwa hali yako ya rohoni ni mfu. Upo mfano mmoja katika biblia wa mtu ambaye makao yake yalikuwa ni makaburini tu maisha yake yote haondoki pale.. Na biblia inatoa sababu kwamba ni nguvu za giza za mapepo zilikuwa zimemfunga..Na mapepo yale yalikuwa hayana lengo lingine zaidi ya kumuua..

Utasema umejuaje hilo? Tumejua hilo pale tulipoona baada ya kukemewa na Yesu, yalimpotoka na kuwaingia wale nguruwe, na moja kwa moja yale mapepo yakawakimbiza wale nguruwe kwenye maji kuwaangamiza..Hiyo yote ni kuonyesha kuwa lengo lao lilikuwa kuua tu na si kingine..Embu tusome kidogo..

Marko 5 :1-15

“1 Wakafika ng’ambo ya bahari mpaka nchi ya Wagerasi.

2 Na alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu;

3 makao yake yalikuwa pale makaburini; wala hakuna mtu ye yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa minyororo;

4 kwa sababu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa pingu na minyororo, akaikata ile minyororo, na kuzivunja-vunja zile pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda.

5 Na sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikata-kata kwa mawe.

6 Na alipomwona Yesu kwa mbali, alipiga mbio, akamsujudia;

7 akapiga kelele kwa sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese.

8 Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu.

9 Akamwuliza, Jina lako nani? Akamjibu, Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi.

10 Akamsihi sana asiwapeleke nje ya nchi ile.

11 Na hapo milimani palikuwa na kundi kubwa la nguruwe, wakilisha.

12 Pepo wote wakamsihi, wakisema, Tupeleke katika nguruwe, tupate kuwaingia wao.

13 Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale nguruwe; nalo kundi lote likatelemka kwa kasi gengeni, wakaingia baharini, wapata elfu mbili; wakafa baharini.

14 Wachungaji wao wakakimbia, wakaieneza habari mjini na mashambani. Watu wakatoka walione lililotokea.

15 Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, naye ndiye aliyekuwa na lile jeshi; wakaogopa”.

Unaona, Vivyo hivyo ikiwa unaota upo makaburini ni ishara kuwa hali yako ya kiroho ni mbaya sana, Lakini habari njema ni kuwa YESU Yule Yule wa zamani ndio huyo huyo wa leo.

Siwezi jua maisha yako upo katika hali gani sasahivi kiroho, pengine upo katika vifungo vya dhambi, au vyovyote vile, lakini Nataka nikuambie ni Yesu pekee tu, ndiye anayeweza kukupa raha maishani mwako, haijalishi wewe ni muislamu au nani, ni Yesu peke yake ndio anayeweza kukupa tumaini la maisha mema, ya hapa duniani na mbinguni.

Yeye (Bwana Yesu) mwenyewe alisema..

Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu”;

Unachopaswa kufanya ikiwa unahitaji kumkaribisha Yesu leo maishani mwako, akutengeneze upya, basi uamuzi huo utakuwa ni wa busara sana kwako, Kumbuka sio hilo tu, yapo na mengine usiyoyajua wewe, Yesu anataka kuyarekebisha katika maisha yako, ni wewe tu kuufungua moyo wako,. Hivyo kama upo tayari leo kutubu, dhambi zako kwa kumaanisha kabisa, na kusema kuanzia leo nitamfuata Yesu, basi ni uhakika kuwa leo leo, atakuja ndani yako na kukuokoa, na utaanza kuona mabadiliko makubwa sana kwenye maisha yako ya rohoni na mwilini..

Ikiwa upo tayari sasa kufanya hivyo basi, na kuanza safari mpya ya wokovu, basi fungua hapa, kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba >>>>KUONGOZWA SALA YA TOBA

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo

TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.

BWANA SI MWEPESI WA HASIRA, LAKINI BWANA NI MWINGI WA HASIRA.

UNYAKUO.

DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.

YESU MPONYAJI.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator