NI SALAMA ROHONI MWANGU Lyrics

NI SALAMA ROHONI MWANGU Lyrics

Ni salama rohoni mwangu lyrics- It is well with my soul.


Nyimbo hii ilitungwa na mwanasheria mmoja mkristo aliyeitwa Horatio Spafford, alitunga wimbo huu kutokana na mambo mazito aliyoyapitia katika maisha yake, Matatizo yake yalianza kwa kufiwa na mtoto wake wa pekee wa kiume aliyekuwa na miaka minne, hiyo ilikuwa ni mwaka 1870

Muda mfupi baadaye (mwaka 1871) moto mkubwa uliozuka huko Chicago Marekani mjini kwake, ukaharibu mali zake nyingi ukizingatia alikuwa ni mwanasheria aliyekuwa amefanikiwa sana. Hilo likafuatana na biashara zake pia kuporomoka kutokana na anguko la uchumi lililotokea mwaka 1873, Hivyo ikambidi apange safari ya kwenda Ulaya pamoja na familia yake, Lakini aliahirisha safari kwa ajili ya kuweka mambo yake ya vibiashara vizuri yaliyokuwa yameathiriwa na moto, hivyo ikambidi msafirishe kwanz mkewe na mabinti zake wanne,akiahidi kuwa atawafuta baadaye.

Lakini Meli ilipokuwa inakatisha bahari ya atlantiki, ilizama ghafla kwa kugongana na meli nyingine na mabinti zake wote wanne wakafariki kwenye ajali hiyo akasalimika mke wake tu, akiwa kule Marekani alipokea ujumbe wa telegrafu kutoka kwa mke wake unaosema “Nimepona peke yangu” ndipo Spafford akaondoka kumfuata mkewe, na huko huko akauandika wimbo huu..

https://www.high-endrolex.com/15

Baadaye vina vingine vya mashairi viliongezwa ndipo ukazaliwa wimbo huu, Ni salama Rohoni Mwangu.

****

Nionapo amani kama shwari,

Ama nionapo shida;

Kwa mambo yote umenijulisha,

Ni salama rohoni mwangu.

Salama, Salama,

Rohoni, Rohoni,

Ni salama rohoni mwangu.

Ingawa Shetani atanitesa,

Nitajipa moyo kwani;

Kristo ameona unyonge wangu,

Amekufa kwa roho yangu.

Salama, Salama,

Rohoni, Rohoni,

Ni salama rohoni mwangu.

Dhambi zangu zote, wala si nusu,

Zimewekwa Msalabani;

Wala sichukui laana yake,

Ni salama rohoni mwangu.

Salama, Salama,

Rohoni, Rohoni,

Ni salama rohoni mwangu.

Ee Bwana himiza siku ya kuja,

Panda itakapolia;

Utakaposhuka sitaogopa,

Ni salama rohoni mwangu.

Salama, Salama,

Rohoni, Rohoni,

Ni salama rohoni mwangu.

****

Hata sisi Je! Tunapopitia shida na magumu tunazo nguvu za kusema ni salama rohoni mwangu?, Tunapopitia njaa, tunapopitia misiba, tunapopitia matatizo mazito Je! Bado Tunaweza kumwambia shetani ni Salama rohoni mwangu? Kama ilivyokuwa kwa Ayubu?

Siku zote kumbuka hili Neno..

Mithali 24: 10 Ukizimia siku ya taabu, Nguvu zako ni chache.

Hivyo jipe moyo songa mbele ikiwa wewe ni mkristo, Kwasababu mwisho wa Mungu sikuzote ni mzuri, kama ilivyokuwa kwa Yusufu, kama ilivyokuwa kwa Ayubu, na ndivyo itakavyokuwa na kwako.

Yakobo 5:11 “Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma”.

Shalom.

Tazama chini historia ya nyimbo nyingine za Tenzi:

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP

Kwa maombezi/ubatizo/ Kumpokea Yesu. Wasiliana nasi kwa namba hizi; +255789001312/+255693036618

Mada Nyinginezo:

MWAMBA WENYE IMARA

CHA KUTUMAINI SINA lyrics

BWANA MUNGU NASHANGAA KABISA lyrics

TENZI ZA ROHONI

YATAMBUE MAJIRA YA KUJILIWA KWAKO.

YESU AKALIA KWA SAUTI KUU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments