TENZI ZA ROHONI

TENZI ZA ROHONI

Maana ya Neno “Tenzi” ni Tungo zilizokaa katika mfumo wa “Mashairi”..Kwahiyo Mashairi yote ni Tenzi…Na Tenzi zipo za aina mbili. Kuna Tenzi za Mwilini na TENZI ZA ROHONI.

TENZI ZA MWILINI.

Haya ni mashahiri yote ambayo yametungwa na watu kwa kufikisha ujumbe wa mambo yahusuyo ulimwengu huu…Nyimbo zote zinazoimbwa na wasanii wa kidunia ni tenzi za mwilini…Mashairi yote yanatungwa na Wanafalsafa wa ulimwengu huu ni tenzi za mwilini…

TENZI ZA ROHONI.

Pamoja na kuwepo kwa tenzi za Mwilini,..zipo pia Tenzi za rohoni. Tenzi hizi ni nyimbo za mashahiri ambazo zinatungwa kwa uongozo wa Roho Mtakatifu kwa lengo la kuzinufaisha roho za watu.

Madhara ya Tenzi za rohoni yapo katika roho. Nyimbo hizi hazijatungwa kwa lengo la kuinufaisha dunia, wala kisisimua dunia.Ni nyimbo zilizobeba maonyo na mahubiri ya rohoni. Kiasi kwamba mtu akisikia kama alikuwa hajampa Kristo Yesu maisha yake anaguswa moyo na kumgeukia Kristo.

Kadhalika kama alikuwa amevunjika moyo, au amejeruhiwa rohoni basi anajengeka upya na kufarijika na kupata amani mpya tena na nguvu mpya ya kuendelea mbele.

Kadhalika kama kulikuwa na mtu ambaye amerudi nyuma kiimani basi kwa kupitia nyimbo hizo zinamrejesha upya kwenye mstari..Na kumwonya kuhusu hatari za kupotea njia. n.k

Kama Biblia inavyosema katika..

Wakolosai 3:16 “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu”.

Hivyo tunaonyana kwa Zaburi,  kwa Nyimbo (Ambazo hizi ni nyimbo za kawaida kama mapambio, sifa nk)..Na pia kwa Tenzi za Rohoni (Yaani Nyimbo za rohoni ambazo ni tofauti na sifa).

Katika Ukristo, kipo kitabu kimoja kijulikanacho kama TENZI ZA ROHONI.

Kitabu hichi kimebeba mkusanyiko wa baadhi ya Nyimbo hizo za rohoni (yaani tenzi za rohoni)..Wengi wa watunzi wa nyimbo hizo ndani ya kitabu hicho hawakuzitunga kwa lengo la kupata fedha au kwa lengo la kusisimua watu..Au hawakuamka asubuhi na kuamua kuzitunga tu..

Wengi waliziimba hizo nyimbo kwa ufunuo wa Roho kutokana na mambo fulani ya kiroho waliyopitia katika maisha yao…Wengine walipokuwa matatizoni na Bwana akawaokoa au akaonyesha mkono wake Ndipo wakasukumwa kuziimba…

Kwamfano mwandishi wa wimbo wa tenzi unaoitwa “Yesu kwetu ni Rafiki”…aliyeitwa Joseph Scriven huyu baada ya mpenzi wake kufa kwa kuzama bahati mbaya kwenye maji..siku moja kabla ya harusi yao..alihamia Canada na huko akapata taarifa mama yake kuwa ni mgonjwa sana..Hivyo katika hali ile ya matatizo anayoyapitia akamwandikia shairi la kumfariji mama yake linalosema “omba bila kukata tamaa”..shahiri hilo likaja kubadilishwa jina na kuwa “Yesu Kwetu ni Rafiki”..ambalo ndilo tunaloliimba leo katika vitabu vyetu vya tenzi..

Kwamfano tena wimbo wa tenzi unaoujulikana kama “NI SALAMA ROHONI MWANGU”..

Wimbo huu ulitungwa na mtu anayeitwa Horatio Spafford.. Huyu alikuwa ni Mwanasheria aliyefanikiwa sana..Mambo yalimbadilikia ghafla baada ya moto mkubwa kuzuka katika mji aliokuwa anafanyia kazi wa Chicago mwaka 1871..ukasababisha kuchoma nyaraka zake zote za kazi na hivyo kubaki bila nyaraka yoyote ya kazi…Baada ya tukio hilo akaanza kuporomoka kiuchumi kwani kibarua chake kiliota nyasi… na hivyo kuazimia kuhamia Ulaya.

Wakati anawatanguliza mkewe na wanawe wakike wanne Ulaya yeye alibaki Chicago kumalizia kuweka mambo yake sawa ndipo awafuate wanawe na mkewe huyo Ulaya..Wakati wanawe na mkewe wapo safarini kwenye meli,.. Meli yao ilipata ajali na kuzama na kusababisha kifo cha wanawe wote wanne…Kwa bahati nzuri mkewe aliwahiwa kuokolewa lakini alikuwa katika hali ya mahutihuti.. Horatio alipozipata hizo habari alihuzunika sana, ikambidi afunge safari akamwangalie mkewe hali yake katika hali ya huzuni sana…Wakati yupo kwenye meli akapita lile eneo ambalo ajali ilitokea…Msukumo fulani ndani ukamjia kuimba huu wimbo “

NI SALAMA ROHONI MWANGU

1.Nionapo amani kama shwari, Ama nionapo shida; Kwa mambo yote umenijulisha, Ni salama rohoni mwangu.

Salama rohoni, Ni salama rohoni mwangu.

2.Ingawa shetani atanitesa, Nitajipa moyo kwani Kristo ameona unyonge wangu, Amekufa kwa roho yangu.

Umeona?..Ni wimbo wa kuganga roho…na sio kuburudisha..Ni wimbo wa kutia nguvu roho zetu katika tabu tunazopitia au tutakazopitia, shetani anapotutesa tunajipa moyo na kusema, ijapokuwa nimepoteza vyote lakini ni salama rohoni mwangu, Ninaye Kristo, ingawa nje hakuna usalama lakini Rohoni mwangu kuna usalama n.k…Huo ndio mfano wa Tenzi za rohoni.

Na watunzi wengine wote waliosalia wa tenzi za rohoni…walisukumwa na nguvu fulani ya kiMungu kuziandika.(Tazama historia ya nyimbo nyingine chini mwisho wa somo hili)

Hivyo Ni nyimbo njema ambazo Neno linatuagiza tuwe tunaziimba..sio tuziimba kwa kutimiza wajibu fulani..hapana bali kwa kuzifaidisha roho zetu…Kwasababu lengo la nyimbo hizo siokuijenga Roho ya Mungu bali roho zetu. Na pia zipo nyimbo nyingi za rohoni (yaani tenzi za rohoni)…Tofauti na hizo tunazozijua za kwenye kitabu cha Tenzi..Hivyo zozote zile Roho atakazokuongoza kuzitumia zina matokeo yale yale katika roho.

Bwana akubariki sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Tafadhali share na wengine.


Mada Nyinginezo:

CHA KUTUMAINI SINA lyrics

USINIPITE MWOKOZI Lyrics

MWAMBA WENYE IMARA

MATESO YA MWENYE HAKI

UWE MWAMINIFU HATA KUFA.

TULICHUNGUZE UMBO LA YESU NA MWENENDO WAKE.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
9 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
James Mwansyemela
James Mwansyemela
1 year ago

Nashukuru kwa elimu hii njema.

Esther Mwanisi
Esther Mwanisi
1 year ago

Habari.
Ninafanya utafiti kuhusu nyimbo za kitabu cha “Tenzi za Rohoni.” Kwa hiyo, ninaomba kujua kama nyimbo za kitabu hiki zilianza kutungwa kwa lugha ya Kiingereza kisha zikaja kutafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili? au asili yake ni lugha ya Kiswahili moja kwa moja?

BARAKA PAUL
BARAKA PAUL
2 years ago

NAOMBA KUJIUNGA NA KIKUNDI HIKI

Gideon Mumo
Gideon Mumo
3 years ago

Great God Bless

Yohana Bahame
Yohana Bahame
3 years ago

May God bless you

God Freelancers
God Freelancers
4 years ago

Ubarikiwe sana Mtumishi. Umechambua vema sana