Na ulimi laini huvunja mfupa.(Mithali 25:15)

Na ulimi laini huvunja mfupa.(Mithali 25:15)

SWALI: Biblia ina maana gani kusema “Na ulimi laini huvunja mfupa”? (Mithali 25:15)

Mithali 25:15 “Kwa uvumilivu mwingi mkuu husadikishwa; Na ulimi laini huvunja mfupa”.


JIBU: Ulimi ni kiungo kilaini kuliko vyote katika mwili. Lakini biblia inatupa ufunuo wake, kuwa kinauwezo  wa kuvunja mifupa?

Je kinavunjaje mifupa?

Hiyo ni lugha ya ki-mithali tu, kuonyesha kwamba ulimi unaweza kuleta matokeo au madhara makubwa ya nje, kuliko hata kinavyoweza kudhaniwa.

  1. Ulimi ukitumika vyema unaweza kuleta suluhu ya matatizo makubwa yaliyoshindikana…

    2.  Vilevile ukitumika isivyopasa unaweza kuleta, matatizo makubwa kupita kiasi.

Tutazame kwenye biblia mfano wa pale ulimi ulipotumika vibaya:

Mtoto wa Sulemani, alilisababishia taifa la Israeli kugawanyika mara mbili, kwasababu  tu ya ulimi wake, usiokuwa na busara, kwa wana wa Israeli. Na hilo alilisema kutokana na malalamika ya baadhi ya wayahudi ambao waliomba wapunguziwe utumwa ambao baba yake Sulemani aliwatwisha.. Lakini yeye badala ya kusikiliza mashauri ya wazee, akasikiliza mashauri ya vijana wanzake, Na kibaya Zaidi badala awapooze kwa maneno mazuri akawaambia, utumwa wangu utakuwa ni Zaidi hata ya ule utumwa wa baba yangu.

Hivyo maneno hayo yakawakasirisha sana wayahudi wengi, mpaka, wakakataa kutawaliwa na uzao Daudi wakajitenga, ndio hapo pakawa mwanzo wa mataifa mawili kuundwa ndani ya nchi moja (yaani Israeli na Yuda), kwa miaka mingi sana.

1Wafalme 12:13 “Mfalme akawajibu watu wale kwa ukali, akaliacha shauri lile wazee walilompa;

14 akawajibu kama vile walivyomshauri vijana, akasema, Baba yangu alilifanya zito kongwa lenu, bali mimi nitaongeza kongwa lenu; baba yangu aliwapiga kwa mijeledi, bali mimi nitawapigeni kwa nge.

15 Basi mfalme hakuwasikia wale watu; maana jambo hili lilitoka kwa Bwana, ili alitimize neno lake, Bwana alilomwambia Yeroboamu mwana wa Nebati kwa kinywa cha Ahiya Mshiloni.

16 Basi Israeli wote walipoona ya kuwa mfalme hakuwasikia, hao watu walimjibu mfalme, wakasema, Tuna sehemu gani katika Daudi? Wala hatuna urithi katika mwana wa Yese. Haya! Nendeni zenu hemani kwenu, enyi Israeli; sasa itunze nyumba yako mwenyewe, Ee Daudi. Hivyo Israeli wakaenda zao hemani kwao”.

Huo ni mfano wa mahali ambapo ulimi ulitimika vibaya;

Mahali pengine ambapo ulimi ulitumika vizuri, na ukabatilisha mashauri mabaya;

Ni pale Daudi alipoonyesha fadhila zake nyingi kwa mtu mmoja aliyeitwa Nabali, lakini pale naye alipotaka chakula, Nabali alimjibu kwa maneno ya kukasirisha na kashfa, hivyo Daudi akaapa kuwa atakwenda kuwaangamiza watu wote wa nyumbani mwake, japokuwa aliwasaidia hapo kabla. Lakini alipokuwa njiani, mke wa Nabali alipata taarifa hizo kuwa Daudi na jeshi lake wanakuja kuwaangamiza, hivyo akamwendea Daudi, kwa kujinyenyekeza na kumpa maneno malaini ya kutuliza hasira. Ndipo Daudi akaghahiri uuaje wake aliokusudia, kwa ukoo mzima wa Nabali.

1Samweli 25:21 “Basi Daudi alikuwa amesema, Hakika ni bure nilivyokuwa nikilinda nyikani yote aliyo nayo mtu huyu, asipotewe na kitu cho chote cha mali yake yote; naye amenilipa mabaya badala ya mema.

22 Mungu naye awafanyie hivyo adui za Daudi, na kuzidi, nikimwachia katika wote walio wake hata mtoto mume mmoja, kutakapopambazuka asubuhi.

23 Ndipo hapo Abigaili alipomwona Daudi, alifanya haraka kushuka juu ya punda wake, akamwangukia Daudi kifulifuli, akainama mpaka nchi.

24 Akamwangukia miguuni pake, akasema, Juu yangu, bwana wangu, juu yangu mimi na uwe uovu; tafadhali mjakazi wako na anene masikioni mwako, nawe uyasikilize maneno ya mjakazi wako.

25 Nakusihi, bwana wangu, wewe usimwangalie huyu mtu asiyefaa, yaani, Nabali; kwa maana kama lilivyo jina lake ndivyo alivyo yeye; jina lake ndilo Nabali, na upumbavu anao; lakini mimi, mjakazi wako, sikuwaona hao vijana wa bwana wangu aliowatuma.

26 Basi sasa, bwana wangu, aishivyo Bwana, na iishivyo nafsi yako, kwa kuwa Bwana amekuzuia usimwage damu, tena usijilipize kisasi mkono wako mwenyewe, basi sasa adui zako, na hao wamtakiao bwana wangu mabaya, wawe kama Nabali.

27 Na sasa zawadi hii, mjakazi wako aliyomletea bwana wangu, na wapewe vijana wamfuatao bwana wangu.

28 Nakuomba ulisamehe kosa lake mjakazi wako, kwa kuwa hakika Bwana atamfanyia bwana wangu nyumba iliyo imara, kwa sababu bwana wangu anavipiga vita vya Bwana; tena uovu hautaonekana ndani yako siku zako zote.

29 Na hata ijapokuwa binadamu angeinuka akuwinde, na kuitafuta nafsi yako, hiyo nafsi ya bwana wangu itafungwa katika furushi ya uhai pamoja na Bwana, Mungu wako; na nafsi za adui zako ndizo atakazozitupa nje, kama kutoka kati ya teo.

30 Tena itakuwa, hapo Bwana atakapokuwa amemtendea bwana wangu sawasawa na mema yote aliyoyanena juu yako, na kukutawaza juu ya Israeli;

31 hili halitakuwa kwazo, wala chukizo la moyoni kwa bwana wangu, ama ya kuwa umemwaga damu bure, ama ya kuwa bwana wangu amejilipiza kisasi mwenyewe; tena hapo Bwana atakapokuwa amemtendea bwana wangu mema, ndipo umkumbuke mjakazi wako.

32 Naye Daudi akamwambia Abigaili, Na ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye amekuleta hivi leo kunilaki;

33 na ibarikiwe busara yako, na ubarikiwe wewe, uliyenizuia hivi leo nisimwage damu, wala kujilipiza kisasi kwa mkono wangu mwenyewe.

34 Kwa kuwa ni kweli, aishivyo Bwana, Mungu wa Israeli, aliyenizuia nisikudhuru, kwamba hungefanya haraka kuja kunilaki, hakika huyu Nabali asingaliachiwa hata mtoto mume mmoja, kutakapopambazuka asubuhi.

35 Basi Daudi akapokea mkononi mwake vitu vile alivyomletea; akamwambia, Haya! Kwea kwa amani kwenda nyumbani kwako; tazama, nimeisikiliza sauti yako, nami nimeukubali uso wako”.

Ndio maana Biblia inamalizia kwa kusema..

Yakobo 3:5 “Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.

6 Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum.

7 Maana kila aina ya wanyama, na ya ndege, na ya vitambaavyo, na ya vitu vilivyomo baharini, vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa na wanadamu.

8 Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.

9 Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu”.

Hivyo tujifunze kutumia ndimi zetu vizuri. Kwasababu kwa hizi tutajibariki wenyewe na kwa hizi tutajiangamiza wenyewe.

Kumbuka; ulimi laini huvunja mfupa.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Nini maana ya kilichotarajiwa kikikawia kuja moyo huugua (Mithali 13:12)?.

DORKASI AITWAYE PAA.

CHANGIA SASA.

UTAONA MAMBO MAKUBWA KULIKO HAYA.

MKAMCHUKUE SALAMA.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Floribert Mwamba
Floribert Mwamba
1 year ago

Nitumiye Somo mbali mbali za Neno la Mungu.