Zipo tabia au mienendo ambayo inaweza kurithishwa kutoka kwa wazazi au mababu/mabibi kwenda kwa watoto au wajukuu. Kama vile jinsi sura, maumbile, rangi, kimo, na mwonekano vinavyoweza kurithishwa kutoka kwa mzazi kwenda kwa mtoto, kiasi cha kwamba mtoto anazaliwa na anakuwa amefanana na baba yake vile vile au bibia yake au mama yake….halikadhalika mambo ya ndani kama vile tabia au mienendo, mtu anaweza kurithi kutoka kwa wazazi wake au mababu zake/mabibi zake.
Ikiwa na maana kuwa kama Mzazi alikuwa na tabia ya ulevi kuna uwezekano na mwana wake naye akaja kuichukua hiyo tabia kama hatashughulika nayo, vile vile kama Mama alikuwa ni kahaba kuna uwezekano na binti naye akaja kuwa kahaba vile vile.
Ezekieli 16:44 “….KAMA MAMA YA MTU ALIVYO, NDIVYO ALIVYO BINTI YAKE”.
Kama mzazi alikuwa ni mtu wa hasira, au mwuaji ni rahisi na mwanae kuja kuwa mtu wa namna hiyo hiyo, kama mzazi au babu alikuwa mwizi, au mkorofi ni rahisi na mtoto wake au mjukuu wake kuja kuchukua hiyo tabia.
Hivyo ni muhimu sana kushughulika na Mienendo ya kurithi!… Ukiona una tabia fulani ambayo pia ipo au ilikuwepo kwa wazazi wako basi shughulika na hiyo tabia mapema.
Zifuatazo ni njia za kushughulika na tabia za Kurithi.
1. ZAMA KATIKA AGANO LA DAMU YA YESU.
Damu ya Yesu pekee ndio inayovunja na kufuta maagano yote ya ukoo na tabia zote za kurithi. Utauliza kivipi?..tusome maandiko yafuatayo..
1Petro 1:18 “Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; MPATE KUTOKA KATIKA MWENENDO WENU USIOFAA MLIOUPOKEA KWA BABA ZENU; 19 bali kwa DAMU YA THAMANI, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo”.
1Petro 1:18 “Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; MPATE KUTOKA KATIKA MWENENDO WENU USIOFAA MLIOUPOKEA KWA BABA ZENU;
19 bali kwa DAMU YA THAMANI, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo”.
Hapo anasema “MPATE KUTOKA KATIKA MWENENDO USIOFAA MLIOPOKEA KWA BABA ZENU”..Kumbe kuna mienendo inatoka kwa mababa na si yetu!, bali tumepokea!.. na sasa ni kitu gani kinaweza kuifuta hiyo mienendo?..si kingine bali ni Damu ya Yesu pekee sawasawa na huo mstari wa 19.
Na tunaoshwaje kwa Damu ya Yesu?..
Si kwa njia nyingine bali ile ya KUTUBU, kwa kumaanisha kuacha hiyo mienendo tuliyoirithi na hatua ya pili ni KUBATIZWA katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana Yesu na hatua ya tatu nay a mwisho ni KUPOKEA ROHO MTAKATIFU. (sawasawa na Matendo 2:38).
Baada ya hapo ile damu ya Yesu ambayo mpaka leo inatiririka pale Kalvari katika ulimwengu wa Roho, itakutakasa kwa namna isiyoweza kuonekana kwa macho na utakuwa safi, na mizizi ya tabia zote za kurithi itakuwa imekufa hapo..tabia za hasira, vinyongo, chuki, ukahaba, uhuni, vita, wizi, ulevi, uchoyo, ubinafsi n.k zitakuwa zimeondoka.
2.DUMU KATIKA UTAKASO
Baada ya kupokea utakaso wa Damu ya Yesu kwa njia ya kutubu na kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu sawasawa na Matendo 2:38, hatua inayofuata si kulala tu!, na kusubiria matokeo!!…bali ni kudumu katika agano hilo la Damu ya Yesu, kwanjia ya kuomba mara kwa mara na kuondokana na vichocheo vyote vya dhambi, pamoja na kumtumikia Mungu.
Usitubu na kubatizwa halafu ukaendelea kwenda kwa waganga, au kufanya matambiko ya ukoo, au kutenda dhambi..(hapo zile tabia hazitakuondoka bali ndio zitakita mizizi zaidi)
Lakini ukizingatia hayo maandiko yanayotufundisha kwa moyo wote, basi fahamu kuwa hakuna tabia yoyote ya kurithi itakayosalia ndani yako, bali utakuwa safi daima na hivyo hata kufanyika baraka kwa vizazi vyako vilivyopo na vitakavyokuja. Na Zaidi sana badala ya watoto wako kurithi tabia za kishetani kutoka kwako watarithi tabia za kiungu, kwasababu tabia za kurithi zinakuwa pia zinabeba laana na baraka nyuma yake..
Maran atha.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?
UMUHIMU WA KUZALIWA MARA YA PILI.
TABIA KUU TATU ZA WAHUBIRI WALIORUDI NYUMA NA KUMWACHA MUNGU.
NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA.
MAZUNGUMZO MABAYA HUHARIBU TABIA NJEMA.
Rudi nyumbani
Print this post